Kama kuna Mzandiki kati ya Membe na Mdhihiri basi ni Mdhihiri!! Jamaa ni mtu asiyejiamini!! Nakumbuka nilipomaliza chuo nilienda kwa Mdhihiri wakati akiwa ni waziri wa kazi. Nilienda pale kwa ajili ya kofia zake mbili, Ni mbunge wangu ( Mchinga) na alikuwa ni waziri wa kazi. Bahati mbaya jina langu la ukoo inaelekea alishawahi kulisikia. Basi ile nagusa ofisi yake tu, mazungumzo yetu yalikuwa hivi:
Mdhihiri: Unataka ni kijana?
NasDaz: Mheshimiwa mimi naitwa......!
Mdhihiri: Sema Unataka ?
In short hakutaka hata nijitambulishe!!!!
Hata pale nilimweleza shida yangu kama angeweza kunisaidia kwa namna yoyote, majibu yake yalikuwa : " Sikiliza wewe kijana, nani kakuambia ofisi hii ina kazi ya kuwatafutia kazi watu? Mimi mwenyewe mwanangu kasoma India kaja hapa hamna kazi nimempeleka Uganda kusoma!! Kuna mwanangu mwingine ameamua kuwa mkurugenzi wa Mchinga Sound! hamna kazi hapa....!" Akabwabwaja sana!!
Nikajiuliza sijui mambo ya wanawe mimi yananihusu nini!!! Anyway, inawezekana sikuwa na sababu za kwenda kuomba msaada kama huo lakini nilitarajia basi angalau angenijibu kiungwana!! Ajabu, pale tulienda watu wawili. Yule mwenzangu aliongea nae kwa zaidi ya nusu saa wakati mimi sikutumia hata dakika tatu, akanitoa baru!!! Niliporudi home na kumsimulia uncle wangu, akaniambia hakutaka tu kuniambia kwavile ingekuwa kama ananikatisha tamaa na kwamba alijua hatatoa ushirikiano!!! Nilipomuuliza ni kwanini akasema kwamba mdhiri ana bifu na watu wa bush kwangu kwavile wa2 wa bush kwetu chaguo lao lilikuwa ni Merehemu Mama wa Tondoa!!! Aidha, alikuwa na wasiwasi na huyu uncle wangu kwamba anataka ubunge wa Mchinga kv alikuwa na tabia za kutaka kuwasaidia wa2 pale bush!! Akawa na bifu nae wakati uncle na siasa ni vi2 viwili tofauti!!! Kwahiyo, ni mtu ambae hana confidence!! Asikuambie mtu, wenyewe watu wa Lindi tunajua Membe ni nani kuliko huyo Mdhiri na si kwa sababu ni minister!!!
Tukija kwenye hoja ya kiwanda, hata kama kweli Membe alitaka kukitoa kiwnda Mchinga basi alikuwa right kwavile am sure alitaka kiwe Lindi Mjini. Mji wa Lindi wa Lindi unakufa kifo cha kawaida kwahiyo vinahitajika vitu vitakavyosaidia mji huu, na viwanda ndio vitu muhimu. Likewise, ikiwa Wabongo hata hapo Lindi Town hawataki kwenda je, mchinga? Naamini hata kama ni kweli basi Membe alitumia busara badala ya kuangalia siasa!!