Membe kuwania urais 2015...

Membe kuwania urais 2015...

MADA nyingi humu JF zinahusiana na UDINI hivi waTANZANIA nani? ameturoga hadi kuamini UDINI ndio mtaji wa UONGOZI? Tuamke toka usingizini amasivyo TUTAKWISHA
 
Membe yuko chama gani vile? sio CCM?
au hujui kuwa ccm hawana nafasi tena baada ya kumaliza Mkwele? na sijui kama hata atakimaliza kipindi chake cha pili
maana nchi inaelekea ku-collapse and seems like there isnt any direction to rescue it.
 
Ila mwambie asife moyo bado Membe anaweza kuwa raisi wa Tanzania, kwa sababu watanzania tuna ushabiki wa kijinga na wa vyama, ukichanganya na ukosefu wa Elimu kwa watanzania wengi (USISAHAU KWAMBA MTAJI MKUBWA WA CCM, ni ujinga wa watanzania. Hata hivyo Membe ili agombee, si mpaka apitishwe na chama chake, na uwezekano wa kupitishwa yeye 2015 ni mdogo au hauopo, hii ni kuzingatia utaratibu waliojiwekea CCM wa wagombea kubadilisha, kutoka MKRISTO, MUISLAM NA WA BARA, WA ZANZIBA. kwa sasa ianaoneka kabisa atakua Shamsi Vuai Nahodha. Na CCM wakilazimisha kumpitisha membe, atakumbana na uasi wa wana CCM watakaokuwa hawajakubaliana na kuvuruga utaratibu wao wa siku nying.

hapa tu umechemka
 
Huyu Nahodha atawaongoza akina anai?
Ila mwambie asife moyo bado Membe anaweza kuwa raisi wa Tanzania, kwa sababu watanzania tuna ushabiki wa kijinga na wa vyama, ukichanganya na ukosefu wa Elimu kwa watanzania wengi (USISAHAU KWAMBA MTAJI MKUBWA WA CCM, ni ujinga wa watanzania. Hata hivyo Membe ili agombee, si mpaka apitishwe na chama chuyu hake, na uwezekano wa kupitishwa yeye 2015 ni mdogo au hauopo, hii ni kuzingatia utaratibu waliojiwekea CCM wa wagombea kubadilisha, kutoka MKRISTO, MUISLAM NA WA BARA, WA ZANZIBA. kwa sasa ianaoneka kabisa atakua Shamsi Vuai Nahodha. Na CCM wakilazimisha kumpitisha membe, atakumbana na uasi wa wana CCM watakaokuwa hawajakubaliana na kuvuruga utaratibu wao wa siku nying.

hapa tu umechemka
 
Hii thread imejaa ujinga mwingi na mambo mengi ya kufikirika. In fact, tunayoishuhudia hapa ni mob justice ya watu ambao wana chuki na personality ya mtu badala ya kujadili hoja. kiinachosikitisha ni kwamba hoja hii ya "urais wa Membe" imekuwa ikijirudia na kila mara hakuna kipya kinachoibuka. Wengi wa wanaorukia hoja hii wanasukumwa na chuki zao za kidini (kutoka pande zote mbili) na phobia isiyo na maana kwa watu.

Hakuna popote ambapo Membe amewahi kutamka au kukiri kwamba anautaka urais wa nchi hii. In fact amewahi kuulizwa hivi karibuni na akakanusha kwamba hana mpango huo na hafikirii. Sasa hiyo habari ya kwamba anataka kugombea imetoka wapi? lakini hata tuki-assume kwamba anafikiria kugombea kwani ni dhambi? Si ni bora wale wenye "hoja nzuri za kumpinga" wasubiri muda ukifika ndipo wafanye hivyo kuliko kugeuka wapiga ramli na kumuadhibu mtu kwa misingi ya hisia?

Lakini jambo linalonishangaza ni huu mwendelezo wa uongo usio na sababu kwamba eti anawapeleka mahujaji Macca kuhiji kama sehemu ya maandalizi ya ubunge na vile vile kusaidia ujenzi wa msikiti mkubwa. Huu ni upotoshaji usion na maana. Membe amekuwa akiwapeleka mahujaji Macca (kwa waislam) na Israel (kwa wakristo). Amejenga pia misikiti na kanisa. Lakini haya yote ameyafanya jimboni kwake kama sehemu ya ahadi zake na kufanikisha mipango ya maendeleo ya jimbo lake. Sasa kama hayo ndiyo kigezo cha kugombea urais, hivi kuna urais mtu anaweza akaupata kwa kutegemea mambo aliyoyafanya jimboni kwake tu?

Mimi naona thread za aina hii zina nia ya kutuondoa kwenye mada muhimu za ufisadi wa nchi hii ambao unaangamiza mamilioni ya Watanzania maskini kwa kukosa elimu bora, matibabu bora, huduma muhimu za jamii na kuwaweka gizani katika karne hii ya 21. Destractions za namna hii zisipewe nafasi hapa JF. na hii shutuma dhidi ya Iran utadhani uhusiano wetu na Iran umeanza jana au juzi kumbe hawa wamekuwa ni marafiki zetu toka miaka ya themanini walipoendesha mapinduzi yao dhidi ya Shah. Kulikoni leo mtu kwenda Iran ionekane issue? This stooping too low!
 
Pasco,

Yeye pamoja na ufitini wake na kujipendekeza kiunafiki, anaweza kweli kuwa Rais wa JMT? Kwa ruhusa ya Lowassa na Rostum? I doubt!!!

Insiders wanasema EL na RA wanamwandalia zengwe JK ampige chini kabla ya 2013 ili apotee kabisa kwenye mbio za u-rais!



....MEMBE ndio alikuwa one of architect wa urais wa Kikwete .....ni mfitini mkubwa aliye tayari hata kuuwa kimwili hadi kisiasa ili tu awe rais..alimsaidia Kikwete kuwauwa kisiasa watu kama IDD simba,HASSY KITINE,SUMAYE,SALIM etc.....Siku hizi amegombana na kina lowassa na Rostam....pamoja na kuwa inahisiwa kuwa wako pamoja ila kugombana ni kama strategy yao ...ili waonekane ni kambi mbili tofauti....itakuwa vigumu sana Watanzania kukwepa kambi yao 2015.
Juzi kwenye tamko la waislamu sheikh baswaleh alimsifia.....ni wazi inajulikana kuwa membe ndie alieenda Iran kuchukua fuko la pesa,,,[mnakumbuka mwandishi Mkongwe Rajab wa london alivyomuumbua].....

Kusema mwaka 2015 kuweka rais mwenye hulka hizi ....basi tuhesabu miaka mingine 10 ya usanii na maumivu.......huyo ndio membe ...aka..Joka la mdimu ..anayeamini hata mpaka cream kama yeye anaweza kuwa rais....
 
Maendeleo hayaletwi na ujenzi wa Misikiti na Makanisa - no, never on earth...

Kiongozi yeyote anayetumia Makanisa na Misikiti kama njia ya kufanikisha maendeleo ni mbaya sana na anastahili kuogopwa kama ukoma (Nyerere) .. Makanisa na Misikiti hujengwa na Waumini na siyo viongozi wa kisiasa - unless watoe usaidizi kama Waumini wa dini hiyo, of which hawezi kuwa muumini wa dini zaidi ya moja!

.....Amejenga pia misikiti na kanisa. Lakini haya yote ameyafanya jimboni kwake kama sehemu ya ahadi zake na kufanikisha mipango ya maendeleo ya jimbo lake. Sasa kama hayo ndiyo kigezo cha kugombea urais, hivi kuna urais mtu anaweza akaupata kwa kutegemea mambo aliyoyafanya jimboni kwake tu?
 
Ni mmoja ya wanasiasa wanaotajwa kumrithi JK.
Niliwahi kusoma kwenye Vyombo vya habari tayari anasaidia ujenzi wa Mskiti Mkubwa mmoja hapa nchini.
Pia kwa njia isiyorasmini ametoa ahadi za kusaidia baadhi ya waumini wa kiislam kwenda kuhiji Makka.Pia aliahidi bungeni mambo ya msingi waumini wa dini hiyo.
Lkn kwa upande mwengine sasa analaumiwa kwamba anaendeswa na maaskofu.
Serikali ilipofanya utafiti wa kina ilijiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote na Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), alitamka hilo bungeni lakini Serikali ilibadili msimamo wake, baada ya Mh membe kuitwa na askofu mmoja anaeheshimka”
Lkn pia baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam walimfuata ofisni na kuwakimbia baada ya kuwakimbia walimuomba kwa maandishi kuktana nao kuhusu Oic kama alivyokutana na mwenzao, hadi leo Mh Membe anawapiga Chenga , yaani hataki kabisa kukaa nao meza moja .
jee kwa mfumo huu anaoenda nao maswala ya kitaifa kama ni waziri wa mambo ya nje, atapokuwa Ikulu kuu hali itakuwaje?
jee kwa mantiki hii, anafaa kutuongoza?au atazidi kuweka Nyufa kati ya Watanzania?

Kama tunataka kula maembe anafaa kuongoza
 
hamna haja ya kujadili ndoto za abunwasi maana hamana raisi atakayetoka chama cha mafisadi tena. Mkwere kafunga!
 
Ni mmoja ya wanasiasa wanaotajwa kumrithi JK.
Niliwahi kusoma kwenye Vyombo vya habari tayari anasaidia ujenzi wa Mskiti Mkubwa mmoja hapa nchini.
Pia kwa njia isiyorasmini ametoa ahadi za kusaidia baadhi ya waumini wa kiislam kwenda kuhiji Makka.Pia aliahidi bungeni mambo ya msingi waumini wa dini hiyo.
Lkn kwa upande mwengine sasa analaumiwa kwamba anaendeswa na maaskofu.
Serikali ilipofanya utafiti wa kina ilijiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote na Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), alitamka hilo bungeni lakini Serikali ilibadili msimamo wake, baada ya Mh membe kuitwa na askofu mmoja anaeheshimka”
Lkn pia baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam walimfuata ofisni na kuwakimbia baada ya kuwakimbia walimuomba kwa maandishi kuktana nao kuhusu Oic kama alivyokutana na mwenzao, hadi leo Mh Membe anawapiga Chenga , yaani hataki kabisa kukaa nao meza moja .
jee kwa mfumo huu anaoenda nao maswala ya kitaifa kama ni waziri wa mambo ya nje, atapokuwa Ikulu kuu hali itakuwaje?
jee kwa mantiki hii, anafaa kutuongoza?au atazidi kuweka Nyufa kati ya Watanzania?

wewe tatizo lako ni udini huna lolote, na kwa maelezo yako akitokea mtu hata kama ni zezeta au jambazi la kisiasa akasema waislam watapata makahama ya kadhi, na kujiunga na oic kwa uwezo wako wa kufikiri ni kwamba lazima atapata kura zote za urais toka kwa waislam.

Mkuu mambo hayako hivyo, kwa watu wote ni watanzania na maisha yao hayawi bora kwa kuendekeza udini au kuwa na mahakama ya kadhi au kujiunga oic. mwenye mawazo ya hivyo ni mtu mwenye fikira potofu, finyu na masikini wa mawazo na fikra.
 
napenda kujua orodha ya maaskofu wanaoendesha nchi hii badala ya ccm.
 
Watanzania wenzangu kama CCM itaendelea kushika madaraka hata Makamba anaweza kuwa rais msishangae, mimi najua Slaa ndiye rais 2015 hayo mengine sijui kabisaa ni ndoto wanazoota.
 
Kwanza ktk nchi hii hakuna binadamu anayenichefua kama huyu baba jamani. Nadhani hata JK haingii... Nikiwasha TV nikamkuta huwa nabadili chanel..
 
Suala la OIC alilisema wazi Bungeni. Report aliyoisoma pale iliandaliwa na Waziri aliyemuachia Wizara. Alichokisema pale ni ukweli, kosa lake ni lipi? Kumchukia mtu huwa kunasabishwa na vitu vingi, moja wapo ni hali ya ujauzito kwa akina mama, na chuki huwa inazidi pale mama anakuwa hajui baba wa mtoto aliye tumboni ni nani? Hivyo nisingependa kumshambulia huyu aliyesema kuwa hampendi Membe kabisa, hata akimuona ktk TV huwa anazima, huenda amepatwa na moja ya vijitabia. Nina imani hali hiyo ikiisha, utarudi ktk upendo wako wa kawaida aliokupa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom