Membe kuongoza Harambee Kanisani Ukonga Jumapili

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe Jumapili ijayo tarehe 14/7/2013 anatarajiwa kuogoza harambee na uzinduzi wa kwaya ya Kanisa Katoliki jimboni Ukonga.

Waziri Membe atazindua kwaya ya Mtakatifu Thomas Akwino ya Kigango cha Thomas Akwino Parokia ya Mji Mpya Relini.

Maandalizi ya Uzinduzi huo yamepamba moto na shughuli hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza Ukonga.

Waziri Membe ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki anatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa CCM watakaogombea Urais 2015.
 
Hivi jamani kwa nini Siku hizi dini zimekubali kutumiwa kisiasa? Badala ya kumuomba Kardinal Pengo au Askofu yeyote kutoka sehemu yoyote wanamuita mwanasiasa.
Huu utaratibu aliouanzisha lowassa utatupeleka pabaya
 
..na viongozi wa makanisa wanavyowawezea Membe, Sitta na Lowasa!
 
Had I been him I would not have taken the bait at this time and with the speculation that is going around..he will be seen as just an ambitious politician playing a"Maasai" jump.
 
Hakuna ubaya wowote, hasa ukizingatia naye ni muumini wa madhehebu hayo. Makanisa ni ya watu. Watu ni pamoja na viongozi.
 
Mhhh... Duu nowdayz ni mambo mazito, wenda huko ndiko kwenye kura.
 
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe Jumapili ijayo tarehe 14/7/2013 anatarajiwa kuogoza harambee na uzinduzi wa kwaya ya Kanisa Katoliki jimboni Ukonga.

Waziri Membe atazindua kwaya ya Mtakatifu Thomas Akwino ya Kigango cha Thomas Akwino Parokia ya Mji Mpya Relini.

Maandalizi ya Uzinduzi huo yamepamba moto na shughuli hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza Ukonga.

Waziri Membe ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki anatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa CCM watakaogombea Urais 2015.

....Yaani sasa hakuna kingine ......ni Harambee kwa kila kona .. kila kukicha ... imeshakuwa fashion !!
 
kadri mda unavyozidi kwenda ndiyo nazidi kuiamini chadema kwa kweli maana haina mambo kama ya kina membe na lowasa kila kukicha kiguu na njia makanisani kisa madaraka,kipindi cha kikwete walizunguka misikitini na matokeo yake lipumba kalalamika kuwa mkuu hakufuata makubaliano,na sasa hawa nao wanazunguka makanisani tutegemee malalamiko mengine tena 2020 endapo mmoja wao kati ya L,na M watafanikiwa kuwa madarakani
 
Ingekuwa Slaa ameenda kuongoza harambee, ungesikia chama cha kidini na wangeleta hii kuwa ushahidi.

Sasa hivi Membe na Lowassa wanajijenga kwa kutumia makanisa. Wanajaribu kuvuta wapendwe na WAKRISTO!!!
 
..na viongozi wa makanisa wanavyowawezea membe, sitta na lowasa!

ndugu umesha wahi kuona yesu akiyabariki majambazi? Bblia inasema hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakapo kuwepo, sasa ndugu tegemea hata watumishi kuvaliwa na maroho ya ufisadi,maana fisadi anapotoa fedha wao wanambariki sikualalisha wizi ndugu,huku ni kumdhalilisha bwana yesu,na hawa watumishi wa namna ihi hawamtumikii mungu bali matumbo yao,warudi watubu na kuhubiri kweli ya kristo,na kukemea dhambi,
 
Wanaweza wakasema kuwa hakuna ushahidi uliothibitishwa kuwa wahusika ni mafisadi.
 
Waacheni tu 2015 ndo watagundua kuwa kumbe kura ya askofu/shekhe/mchungaji/padri/ au Imamu ni moja tu!
So ukienda kanisa fulani ukatoa milioni kadhaa kama lengo lako ni 2015 tegemea kura za hao viongozi wa hapo tu tena sio wote!

WAUMINI HATUDANGANYIKI!!!!!!
 
Hivi jamani kwa nini Siku hizi dini zimekubali kutumiwa kisiasa? Badala ya kumuomba Kardinal Pengo au Askofu yeyote kutoka sehemu yoyote wanamuita mwanasiasa.
Huu utaratibu aliouanzisha lowassa utatupeleka pabaya

kwasababu pengo au askofu mwngne hana uwezo wa kutoa 10 million kwenye harambee
 
Nafikiri baada ya kuona mwenzao ameukwaa uraisi kupitia misikitini 2010,nao wanadhani makanisa ni njia 'rahisi' ya kuukwaa 'urahisi' 2015.Waumini tushabumbuluka sasa nyie leteni tu hela zote mlizokwiba na kuhongwa na wakwepa kodi na mafisadi,2015 kura zote CHADEMA!Bye bye CCM!!!!!
 
Hivi jamani kwa nini Siku hizi dini zimekubali kutumiwa kisiasa? Badala ya kumuomba Kardinal Pengo au Askofu yeyote kutoka sehemu yoyote wanamuita mwanasiasa.
Huu utaratibu aliouanzisha lowassa utatupeleka pabaya

kwasababu pengo au askofu mwngne hana uwezo wa kutoa 10 million kwenye harambee

mbaya zaidi Membe naogopa hizo harambee zitammaliza, mwezake lowasa hatoi mfukoni anavisima vyake vya pesa ambavyo ni ROSTAM,KARAMAGI n.k
 
kwasababu pengo au askofu mwngne hana uwezo wa kutoa 10 million kwenye harambee

Acha vituko milioni 10 kitu gani kwa roman emperor ? haujui unachosema ! Waache kutoa waone kama uzinduzi haufanyiki! Harambee ni kushirikishana baraka sio nani katoa kipi
 
mungu atatushindia tu kila jambo huwa na mwanzo na mwisho pia.
 
Back
Top Bottom