Membe, honestly hatukuelewi!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Ulikuwa mgombea wa kiti cha urais, wengine walienda mbali kudai ulikuwa wa mfukoni!
Bahati haikuwa yako, dhoruba za yule kada maarufu, Eddo, zilikupulizia mbali.
Hukuwa peke yako, vumbi zili ziliwapuliza wengi.

Ulipoukosa urais ukawa kama umeingia kauzezeta fulani hivi.
Ni kama hukuamini kilichotokea, Mwenyekiti aliyekubeba alizidiwa kete.

Kaingia mzee wa Push Up, yeye hata ukatibu wa chama wa kijiji hakuwahi kuukwaa.
Sasa leo ndo Rais.
Tena Rais mtumbuaji majipu.

Mengine ya hayo majipu ni yale Membe and co. waliyoyalea na kukomaa.
Kwa kauli yake Membe alisema watu wanapaa angani kuelekea majuu, utafikiri nchi inaungua moto!!
Aliyekuwa kinara wa kupaa angani tunamjua, our very own Mkulu wa Msoga.
Sijui Membe alimshauri vipi bosi wake!

Sasa leo sijui Membe kala maharagwe ya wapi vile, utafikiri kaamka nazo.
Mara Baraza la Mawaziri hakuna kilichofanyika, mara kuzuia kusafiri nje hamna lolote!
Sasa ati uchaguzi Zanzibar ungefutwa kwa nafungu!

Hivi? vikao vya chama kuongelea haya masuala vilikufa?
Au siku hizi ni siasa huria?
Au Membe naye anataka mageuzi nje ya chama?

Maswali ni mengi, honestly Membe hatukuelewi!
 
Hela huwa haina adabu, hasa inapoanza kutoweka.
Na kukaa Mtama kuchunga mbuzi na kuandika vitabu hailipi sana.
Lazima wanasiasa wawe mjini, si unajua tena Bunge wiki lijalo?
 
Well....hata kama ana mawazo mazuri kwanini hakuyatoa on time?
mi nadhani aache walioko kazini wafanye kazi...hizi mambo za u-kamilioni zinetugharimu sana..watu wasio na misimamo...aagh!
 
Anatapatapa...hajakubali wala kuamini kilichotokea...anasema rais atake asitake lazima aende nje...kwani nani alisema rais hataenda nje...
 
Well....hata kama ana mawazo mazuri kwanini hakuyatoa on time?
mi nadhani aache walioko kazini wafanye kazi...hizi mambo za u-kamilioni zinetugharimu sana..watu wasio na misimamo...aagh!
Umenena mkuu, si ajabu ana fundo kooni ambalo hajalitoa.
Lakini chama si kina utaratibu wake?
 
Membe ni kada mkubwa CCM na chochote anachofanya akiwa humo ni kwa ajili ya CCM na wale anaokubaliana nao ndani ya chama.

Hivi mmeshasahau kuwa strategy ya ku pre empty hoja za wapinzani imefanya vizuri sana in CCM's favor?? Hizi ni sarakasi kuelekea uchaguzi wa marudio subirieni complimentary ya sarakasi hizi
 
Sio Membe peke yake tu.
Yeye akili zimeanza kumrudia mapema.

Wengi wako nyuma yake,ni suala la muda tu
 
tatizo la ccm hamtaki kushauriwa wala kukosolewa. na sasa tangu aingie magufuli uki kusoa serekeli unaonekana wewe sio mtanzania mzalendo.. kila anachofanya magufuli lazima wote tukiunge mkono hata kama ni ujinga... kwani magufuli yeye ni mungu hakoseagi? membe ana uhuru wa kutoa maoni yake na hii inaonesha jinsi gani ccm ni chama dhaifu kwani hawako tayar kumsikia mtu ambae haungi mkono sera zao
 
Nadhani anatumia haki yake kikatiba kueleza yaliyoko moyoni mwake hivo sioni kama kuna haja ya kumlaumu "muungwana"
 
Membe au Mtanzania mwingine yeyote ana haki ya kimsingi na ya kikatiba ya kuhoji, kukosoa au kutoa maoni yake wakati wowote kuhusu maamuzi na utendaji wa serikali. Ni jambo la ajabu sana kwa mwanachama wa jukwaa hili lenye kauli mbiu, "Pale tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi" kumbeza Membe kwa kutoa maoni yake 'kwa uwazi'. Ni makosa pia kutazama kila ukosoaji wa serikali kwa jicho la mpambano wa kisiasa (political rivalry) kati ya wakosoaji na walio madarakani. Lakini pia demokrasia imara haiwezi kuwepo nchini bila migongano ya aina hii.
 
Back
Top Bottom