MY ANALYSIS: CCM, Rais JK, Lowassa, Membe, Magufuli na Matokeo ya Dodoma!

Apr 27, 2006
26,588
10,375
- HAKUNA BAHATI MBAYA KWENYE SIASA KILA KITU HUWA KINAPANGWA KIONEKANE BAHATI MBAYA NA NDIO SIASA

- Kwa mara nyingine tena Rais JK amethibitisha kile nilichokuwa ninakisema siku nyingi sana Mnyonge Mnyongeni yaani he is the master of local politics anakuwa Rais wa kwanza katika historia ya Taifa letu kumuachia Urais Mtu anayemtaka, wengine wote Kuanzia Mwalimu, Mwinyi, mpaka Mkapa walishindwa kwa maneno mafupi Rais JK ndiye the best politician we have ever had katika hili Taifa.

Mwalimu alikuwa the best Leader ever ila not a true Politician kwa sababu after what JK did in Dodoma yaani kumpitisha mgombea wake bila kuacha a serious maumivu kwa Wagombea JK anakuwa Mwanasiasa mzuri kuliko Mwalimu ambaye kila alipojaribu kumpitisha mgombea wake yoyote yule siku zote alikuwa akiacha maumivu makubwa sana nyuma.

Kwa mara ya kwanza Wananchi tunatakiwa kujifunza kuwa kuna tofauti kubwa sana baina ya Kiongozi na Mwanasiasa na huenda ni vitu viwili tofauti, kwa sababu for sure we can debate on Strength za JK as Kiongozi lakini as a Politician ninasema hapana he is the master, kwa mfano jinsi alivyoweza kulimaliza tatizo la CCM na CUF Zanzibar bila kuacha maumivu kama enzi za MWalimu na wengine wote waliofuata isipokuwa yeye tu amekuja kulituliza bila makelele tena.

1. MTANDAO:-

- Wamethibitisha kwamba they were good only for the fight for power lakini sio keeping the power wameshindwa vibaya sana ni kwa sababu wakati wa vita yao walishindwa kumuelewa Kiongozi wao JK as a Human Being na as a Politician kwamba sio mtu anayependa Makuu ila alishirikiana nao sana na hata kufumbia mambo mengi asiyoyakubali ambayo waliyafanya kwenye mbio za kutafuta madaraka ingawa kimsingi kama binadam hakuyapenda kabisa.

Wafuasi wake Lowassa na Membe wangekuwa na akili kubwa ya siasa wangemsoma mapema na kujiepusha kabisa na asiyoyapenda ili kuwa na nafasi ya kumrithi baada ya Miaka 10, lakini wao na washauri wao walishindwa kabisa kumsoma JK wakadhani ni mwenzao 100% kumbe hakuwa na amethibitisha haya majuzi Dodoma kwa kumpitisha mtu wake Magufuli mbele yao huku wao wakibaki wanalaumiana na kuilaumu CCM, ingawa so far Membe amekubali matokeo na ninaamini kwamba ameelewa ujumbe mzito wa Dodoma kwamba hakuwa mtu wake kama alivyoamini huko nyuma na wengi wetu tulivyoamini baada ya kuaminishwa na ambao tuliwaamini sana.

2. CCM:-

- Chama Cha Mapinduzi, kwa kumchagua Magufuli kimejisaidia sana kurudi kwenye mstari wa Mwalimu kwa sababu ninaamini as a FACT kwamba Magufuli ametumia sio zaidi ya Tsh. Millioni 2 tu kushinda nafasi ambayo baadhi ya Wafuasi wa JK huko Mtandao walishatuaminisha kwamba haiwezi kupatikana bila kutumia Mabillioni ya Pesa, CCM imewafanya watumie Mabillioni yao kuja kumpitisha aliyetumia only 2 Million kwa ajili ya fomu na mafuta ya Gari la kumfikisha mikoani kutafuta wadhamini.

Inasemekana kuna baadhi ya Ofisi za CCM Mkoani baada ya kutopata pesa za rushwa mapema toka kwa Magufuli kama Wagombea wengine waliamua hata kufunga Ofisi na kumataka aje kesho yake as opposed na wagombea waliowatangulizia rushwa, walienda kuwapokea mipakani mwa maeneo yao kwa shangwe kubwa sana. -HOWEVER!!-

Ninaomba kukiambia chama changu CCM na Magufuli kwamba wakati ni sasa please fix your process ya uchaguzi it is rotten, kilichofanyika Dodoma it is a revolution within now keep that revolution spirit ya kubadilisha the whole system kwa kuanza na kuachana na Viongozi wote wabovu waondolewe now ili uchaguzi ujao tusirudie tena matatizo ya kupoteza muda mwingi kuwaongelea Wagombea badala ya records za kazi zao kwa Taifa na CCM kwanza. Ninarudia kwa CCM please fix the process now.

3. LOWASSA

- Kilichomtokea ni matokeo ya uwezo wake mdogo kama politician na washauri wenye uwezo mdogo kisiasa na hasa political strategies za kuweza kushinda huu uchaguzi ambao alituaminisha wananchi wengi kwamba aliutaka kwa udi na uvumba na sasa ameishia kuukosa.

Wazungu wanasema tatizo sio kuanguka isipokuwa umeangukia wapi. Kambi yake wamefanya makosa mengi sana ambayo usingetegemea Mwanasiasa yoyote anayetafuta Urais angeyafanya akijua kwamba ni Rais aliyepo madarakani sasa ndiye mwenye uamuzi mkubwa wa nani wa kumuachia.

Washauri wake na yeye mwenyewe walishindwa kabisa kumuelewa JK kama binadam, Kiongozi Mkuu wa Taifa na kama Mwanasiasa. Wakafanya makosa left and right ya kumu undermine na kumu under estimate Mwanajeshi aliyeacha Jeshi akiwa Kanali, wakamfanyia vitimbi vingi sana vya kisiasa kama kutaka kumvua Uenyekiti wa CCM mara kadhaa Kiongozi waliyetegemea siku moja aje awaachie Madaraka, I mean looking back now inashangaza sana kwamba exactly what were they thinking?

Lowassa hana wa kumlaumu kama kweli nia yake ilikuwa kuwa Rais maana huwezi kukubalika na Viongozi wengi wa chini wa chama chako ukakataliwa na Wakuu wa chama hicho hicho. Je Lowassa hakuona dalili mapema ambazo wengine tuliziona mapema sana, mfano kwenye uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Arumeru ambapo washiriki wengi wa mchakato mzima walisema kuziona dalili zikiwa wazi kabisa kwamba uchaguzi ule ulikuwa ni ujumbe tosha kwa mwenye akili kubwa kisiasa.

Sio siri kwamba Lowassa hakubadili kitu chochote alichokifanya kwenye kampeni za Mtandao kushika power, lakini tatizo aliloshindwa kuelewa ni kwamba JK was not happy na njia zote walizozitumia then kushika power, now as a serious Politician like Lowasa alitakiwa kujua mapema na kuanza kubadili mwenendo, wote tunajua kwamba the process ya CCM kuchagua Rais ndani ya Chama ipo kama ilivyo debatable kama ni fair au unfair ingawa to me haipo open enough kukidhi matakwa ya Demokrasia, lakini ni the same process iliyowapa Lowasa na Mtandao Madaraka huko nyuma.

So leo Lowassa anapolia kuumizwa na hii same Process inachekesha kidogo ukizingatia kwamba huko nyuma amekuwa a beneficiary wa kukatwa majina ya wengine through the same process hakuiona ina tatizo ila amekuja kuona tatizo leo baada ya kukatwa yeye ndipo anapojivua nguo kama ni Mwanasiasa wa kweli au muigizaji!

Lowassa hana wa kumlaumu ila yeye mwenyewe na washauri wake na busara ni avumulie tu na kubaki CCM na kama ameumizwa sana na hii process basi ajitoe muhanga kuirekebisha kwa manufaa ya Taifa na wengine mbele ya safari kama vile Marehemu Kolimba, kabla ya kufikia mauti alikuwa kwenye mbio za kuongoza Kamati Maalum ya CCM ya marekebisho ya yale aliyoyapigia kelele kuwa hayapo sawa ndani ya chama chake.

4. MEMBE

- Tatizo kubwa zaidi yake mwenyewe lilikuwa ni kambi yake, wengi wa washauri wake walikuwa sio wakweli na walijiamini sana kupita kiasi na hawakuwa na muda sana na wasiowataka au wasiowaelewa na walijibagua sana kakikundi fulani ka wateule. Wengi wao ni marafiki zangu wa karibu sana sasa hivi looking back inajisema very clear kwamba aidha walikuwa wanapewa wrong information au walikuwa wanazitunga wenyewe lakini in the end zilikuwa wrong informations.

Sijui kama Membe alijua kwamba hana uwezo wa kupenya NEC, lakini for sure JK alijua sana na mapema kwani kwenye uchaguzi wa NEC through Kapu Membe alipita kwa taabu kidogo kwa hiyo ujumbe pale ulikuwa inahitajika kazi ya ziada sana kwake kupita NEC kwenye uchaguzi wa Rais.

Membe kama mgombea Urais ilikuwa ni vigumu sana kumuona au hata kuongea naye kwenye simu, niliwahi kuwaambia sana washauri wake kuhusu hili tatizo kwamba wananchi wengi walikuwa wakilalamika, lakini ilikuwa ni kama kuongea na ukuta.

Kosa lingine la Membe ni kwamba hata yeye alishindwa kumsoma vizuri JK na in his case akashindwa kuwasoma hata Viongozi wengi wakuu wa CCM aliokuwa nao karibu sana, ambao nyuma yake hawakuwa na imani kama anaweza kupita NEC lakini na wao kama yeye wakajiaminisha kama walivyoaminishwa kwamba ni mtu wa JK aliyepanga kumuachia nafasi yake kitu ambacho hakikuwa kweli.

Tatizo kubwa nililoliona majuzi ni kwamba Membe na kambi yake waliongozwa sana na wrong information je ni nani aliyekuwa anawa mislead? Mpaka leo sijajua ni nani na sitaki kuamini kwamba ni JK mwenyewe ndiye aliyekuwa anawa-mislead kwa sababu haiwezekani mimi niwe a serious politician nishindwe kujua kwamba una mpango wa kuniachia au hapana ina maana I am not a politician.

So kama Lowasa, Membe hana wa kumlaumu isipokuwa yeye mwenyewe kwa kushindwa kusoma vizuri kilichokuwa kinaendelea, ingawa in the end ameonyesha ustaarabu mkubwa sana wa kisiasa kwa kukubali kushindwa bila tatizo, ila na yeye ningemuomba apiganie kurekebisha process ya kupitisha majina bado ninasema haiko sawa sana.

5. MAGUFULI:-

- Dunia nzima tunapenda Washindi ndiye mshindi wa hivi vita na hapa ndiye Mwanasiasa wa kweli hapa, kwa sababu aliweza kuisoma picha nzima ya kuelekea kwenye uchaguzi unaokuja na akaweza kuji position mpaka kushinda bila kuamsha hisia za Taifa.

Hakutumia pesa kabisa zaidi ya malipo ya fomu na mafuta ya safari kwa gari nchi nzima kutafuta wadhamini tena kimya kimya sana na akaweza kujiweka mbali sana na rada zote za utabiri wa kisiasa nchini. Dalili zilianza kujionyesha siku nyingi sana lakini kwa sababu he is a good politician aliweza kuzificha klijua mazingira ya kisiasa nchini na hasa tabia za anayetaka kumuachia yanataka kuwa kimya na pole pole sana.

Hakuwa na team ya kampeni wala hakuchangiwa na mtu na hakufanya kitu chochote cha kuweza kuwafanya wananchi au wahusika wawe na wasi wasi naye kwamba ndiye mrithi wa JK, infact hata alipoingia 5 Bora bado washiriki wengine walishindwa kuona kwamba ndiye mshindi na ndiye anayetakiwa.

Ukweli ni kwamba kwa kampeni aliyoamua kuifanya hakuwa na sababu ya kuongea na mtu yoyote wala kuonana na mtu zaidi tu ya kufanya mambo yake na kuendelea kufanya kazi zake kumuongelea kwa kirefu kuliko maneno yake.

Ni matumaini yangu kwamba atairekebisha process ya CCM na Viongozi wa Taifa kwa kuwaondoa wabovu mapema badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi kama ilivyo sasa.

-HITIMISHO:-

- Kwa uchaguzi huu wa Magufuli, CCM imepiga bao tena la ushindi wa kishindo kizito sana kwa sababu hatimaye hata Wananchi waliokuwa wamepoteza imani na CCM sasa wanataka kurudi na sasa wanatafuta kadi za chama hicho kikongwe.

Ninasema Magufuli ni Kiongozi na ni Mwanasiasa kwa sababu kazi zake zipo wazi tayari kwa public, hakuna binadam mkamilifu najua anayo mawili matatu ya kujibu lakini ukweli ni kwamba yanajibika kulinganisha na wenzake wengi huko CCM. Ni muhimu sana CCM kama chama ikampa nafasi na uhuru mkubwa wa kukibadilisha chama hicho ili kukirudisha kwenye mstari wa katiba yake yenyewe.

Magufuli anachagulika tena kwa kishindo unless CCM wenyewe waharibu kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo sasa Magufuli anatakiwa kuvimaliza kwa kuwapumzisha wale wote wanaokivuruga chama hicho na kuwapa nafasi wafuasi wao zaidi wenye muelekeo wa kuelewa kwamba time has changed. Ninawaomba CCM wamtumie Magufuli kuhakikisha Wagombea ubunge wanaopitishwa kupitia chama hicho wana muelekeo wa mabadiliko kama alivyo Magufuli, sio wabunge wa kwenda kulala usingizi tu bungeni na kusubiri posho.

Ninampa hongera sana JK kwamba kwa alichokifanya Dodoma majuzi inafuta mapungufu yake yote aliyowahi kukifanyia chama hiki, Wapinzani wana kazi kubwa sana kushindana na record ya kazi ya Magufuli ambaye wao wenyewe mara kwa mara wamekuwa wakisifia kazi zake na msimamo wake wa kiuongozi.

Again, Lowassa na Membe hawana wa kumlaumu isipokuwa wao wenyewe na honestly speaking wakubali kwamba uwezo wao mdogo wa akili za kisiasa umewafikisha walipoishia na sio mtu yoyote mwingine. Magufuli amewashinda kwa sababu baina yao 3 ndiye aliyekuwa na akili kubwa sana ya kisiasa pamoja na kwamba alikuwa ndiye mtu wa JK lakini bado aliweza kuwa na nidhamu ya kuficha siri kama ilivyotakiwa mpaka kufikia kushinda, angekuwa mwingine tungeweza kujua mapema kutokana na mdomo wake mrefu na marafiki zake kama wengine tuliokuwa tunawasikia kila siku hapa mjini kwamba JK amewaambia atawaachia.

- NINARUDIA TENA ni muhimu sana Magufuli akawapumzisha kabisa Viongozi wengi ndani ya CCM ambao siku zote wamekuwa ni mzigo na tatizo kubwa kwa chama, au itakuwa vizuri sana wakijiondoa wenyewe kama tunavyotishiwa sana huku mtaani kwamba wanajitayarisha kujitoa, hahahahaha sijawahi kusikia mtu mwenye nia ya kujitoa popote pale Duniani akipiga kelele mapema kuwa jamani ninajitoa! jamani nitajitoa mimi nishikeni nisije nikajitoa jamani! hahahahah kama unajitoa jitoe lakini usituvuruge na makelele ya kujitoa! Na kama hawajitoi please CCM na Magufuli watoeni sasa, CCM inatakiwa kuwa kubwa kuliko wanachama sio otheriwise!!

-MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Nation
 
Sumu ya CCM bado ni ile ile! Ni chupa tu imebadilishwa! Mwananchi zinduka, chukua tahadhari mapema!
 
Sawa baba AGapeo umetixha ndo maana unajiita le akili kubwaz... Xalute man umetixha bonge la analysis
 
CCM hawana jipya! Sera zake chakavu ndizo zimeleta umaskini katika taifa hili! Sasa ni wakati wa wananchi kuamka na kufanya maamuzi magumu kwa njia ya box la kura!
 
Kikwete sii wa kumuamini ktk jambo lolote au makubaliano!Maghufuli ni chaguo au pendekeZo la wazee Mwinyi,Mkapa na Msekwa sii wazo la Kikwete

- Well, ni mawazo yako ila ni Rais na Mwenyekiti wa CCM ndiye mwenye uamuzi wa mwisho, JK ni mtu wa kuaminiwa sana ndio maana ametimiza ahadi yake kwa Magufuli.

Le Mutuz
 
- I am me multi-Talented man unajua kuacha Degree zangu 3 za Marine Engineering, Cirminology na Political Science bado naweza hata kupiga muziki hahahaha, now turudi kwenye mada mimi sio ishu hapa!!,

Le Mutuz

He he he he degree tatu? hebu nitumie ile picha uliyoweka wkati unatfta ubunge wa eac, kuna upuuzi mkubwa uliandika kwenye picha ile
 
Membe ni mtu mzuri sana ila tatizo wapambe wake bwana yaani ni balah..wapambe wake ni hopeless kabisa! Walikua wanajitapa sanaa hadi wakamtengenezea chuki baba wa watu..wapambe wa Membe mlikua too much kwakweli!!

Anyways lesson learnt.. Matumaini yangu ni kwamba huyu mzee atapewa uwaziri mkuu sababu naamini anafaa sana.
 
Nothing was planned at all.

Kilichotekea Dodoma ni udikteta wa hali ya juu ambao tunajaribu kuufunika tukidhani tz ni ya mazuzu.

Nashangaa hakuna mwandishi makini aliyeweza kuzungumzia kwa kina udikteta wa Dodoma. Jinsi alivopatikana magufuli hapaswi kuongoza hili taifa.Sintoandika hekaya kama ya mtoa mada naamini great thinkers wameelewa na zaidi
 
It seems you are less informed, chaguo la Kikwete halikuwa Magufuli bali Membe the second runner up wake alikuwa Mingiro then January, what happened zile zilikuwa kura za maruhani tukose wote, Kikwete hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali yaishe na kujikaza kisabuni.
 
Well said mkuu ccm.Hinaitaji Transformation kubwa sana hasa kwa viongozi wake..kama kuna uwajibikaji ndani ya chama upinzani utatoka wapi?
 
Tuanze na Dogo tuu kwa Magufuli.
Nini msimamo yake juu ya maoni ya katiba ya wananchi yaliyochakachuliwa na maccm??
 
Nimeona Instagram leo ulikua na Mama Kilango. Ndo mliongea haya? Anyway kwa upeo wng mdogo tu Kikwete Magufuli ilikua si pendekezo lake pale kachezea za uso baada ya Sapporters wa Lowassa kushtukia na Kumpigia kura Magufuli ili kumtupa nje Membe ambaye ndio ililua pendekezo la Kikwete. Kwaio Kikwete kachemka tu
 
- Well, ni mawazo yako ila ni Rais na Mwenyekiti wa CCM ndiye mwenye uamuzi wa mwisho, JK ni mtu wa kuaminiwa sana ndio maana ametimiza ahadi yake kwa Magufuli.

Le Mutuz
Le mutuz uchambuzi wako mzuri ila ulipokosea ni kusema Magufuli alikuwa ni chaguo la JK this is wrong JK's family ilikuwa ni Team Membe from mama To Ridhiwani up to Rashid usijidai hujui hili le big show na waliomchagua Magufuli ni wale wa Lowassa baada ya kuapa kwamba Membe hatakaa achukue nchi so kwa hili ndio Magufuli akaokota dodo chini ya mbuyu...you know
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom