Membe amshukia KITINE, amfananisha na "Kingwendu"

Kiranga, Membe naye na hii sauti kila akiulizwa utagombea anasema hajasikia sauti ikimwita! Hivi hii sauti itatoka wapi kwamba akilala asikie sauti akitembea asikie sauti. Nikisoma vitabu vitakatifu huwa nakutana na sauti zikiwaita mitume wakafanye kazi ya Mungu kama vile Sauli alivyoitwa. Sauti kama anayoisema Membe huwa inatoka kwa Mungu kwensa kwa wateule wake ili wamfanyie kazi. Ina maana anasubiri sauti toka kwa Mungu?
Inamaana hata jk kuna sauti ilimtokea? Mbona mpaka 2015 lazima kuna gamba litajitangaza ni nabii
 
Membe ....bado yupo na senior wake ...kumuita kingwendu.....nadhani ,Kitine hakumpa majina ya kashfa wala kumtaja jina .....sasa kajihisi ...ukirusha jiwe gizani atakayelia limempata!!!! ...

Ikumbukwe kuwa kazi kubwa ya Membe "mzee wa fitina " mwaka 2000 kuelekea 2005 ,ilikuwa ni kuwachafua watu wote waliokuwa na nia ya urais ili kumsaidia KIkwete ...mhanga wa kwanza wa wanamtandao alikuwa..
Hassan ( hassy ) Kitine
iddi Simba
Frederick Sumaye
Salim Ahmed Salim

Hawa kwa wakati tofauti walichafuliwa vibaya na wana mtandao.......Huyu Membe urais ...hafai kabisa....eti anasema ...kuna watu ..wanataka agombeeee ...mbona hatuwaoni....au CCJ?

Wanasemaga "mwosha huoshwa!"

....asubiri zamu yake ya kuoshwa, asijerusha ngumi tu!
 
Sijaona kosa la Membe hapa.
Unatuhumu, basi grow a pair na kuelezea kila kitu, otherwise shut up and don't waste wavuja-jasho's time. It is that simple.
 
nilimsikiliza huku namtazama Mzee Hassy kwa umakini sana.
Ktk taarifa yake hakutaja mtu...na kilichofuata ni kundi la watu kuaminishana kuwa aliyezungumziwa pale ni Waziri Membe.

Kwa kifupi nilimpunguzia Maksi Mzee Kitine, kwani kama angekuwa na uzalendo kisha awe na ushahidi wa uhakika wa aliyoyaongea nadhani angemtaja huyo mtu ili tumjue na ikiwezekana Sheria ifuate mkondo wake...na kama ikishindikana kisheria basi tumjue mtu anayetuhujumu kama tulivyowajuwa wale waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga.

Kiukweli kitendo cha mzee Kitine ni cha kinafiki, na ni mbumbumbu tu ndio wanaweza kumuona Mzee huyu ni shujaa.
Kwangu mimi namuona mkurupukaji na Mshambenga tu.

MAFAHARI WAKIGOMBANA WE CHUKUA JEMBE UKALIME! Hapa wanaumbuana wao kwa wao, nae membe kilichomfanya ajibu lile swali ni nini? Kwani alikuwa na haja ya kujibu tena mpaka aite watu VINGWENDU? Ukirusha jiwe gizani ujue limempata. Watanzania wenzangu nimeamini viongozi wenye maadili ya uongozi kwa nchi hii hatuna labda tumuache mzee Dr. Shein labda.
 
“mtu yeyote anayetaka kuomba urais 2015 anahitaji kusikia sauti ikimwambia kila saa omba, yani akilala sauti hiyo anaisikia na hata akitembea … kama akikurupuka lazima awe ameteuliwa na chama chake na kukubalika.

“kwa upande wangu mimi sijaisikia hiyo sauti ikiniambia omba urais ila kwa ubunge niliisikia, hivyo nikiisikia nitawaambia,” alisema.

huu ndio uking'wendu wenyewe!! Hakuna uhusiano wa nafasi ya rais wa nchi na kujipigia ramli/utabiri kama anavyodai huyu membe.
 
kitine,.once tiss always tiss,he still got those spying techniques!kitine is right,membe is fisadi
Wajua wizi aliofanya kitine kwa nchi hii?
Membe ndio alimuumbua na sasa kitine anakurupuka tu
Kwa nafasi aliyokuwa nayo kitine haitakiwi kuzungumzia tuhuma kama hizo bila kumtaja muhusika moja kwa moja ili hatua zichukuliwe
OTIS
 
huu ndio uking'wendu wenyewe!! Hakuna uhusiano wa nafasi ya rais wa nchi na kujipigia ramli/utabiri kama anavyodai huyu membe.

Kuielewa hiyo kauli ya membe ni kazi sana, ukikurupuka hutamuelewa, katumia fasihi kali sana! Nasikitika wengi hamjamuelewa.
 
nilimsikiliza huku namtazama Mzee Hassy kwa umakini sana.
Ktk taarifa yake hakutaja mtu...na kilichofuata ni kundi la watu kuaminishana kuwa aliyezungumziwa pale ni Waziri Membe.

Kwa kifupi nilimpunguzia Maksi Mzee Kitine, kwani kama angekuwa na uzalendo kisha awe na ushahidi wa uhakika wa aliyoyaongea nadhani angemtaja huyo mtu ili tumjue na ikiwezekana Sheria ifuate mkondo wake...na kama ikishindikana kisheria basi tumjue mtu anayetuhujumu kama tulivyowajuwa wale waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga.

Kiukweli kitendo cha mzee Kitine ni cha kinafiki, na ni mbumbumbu tu ndio wanaweza kumuona Mzee huyu ni shujaa.
Kwangu mimi namuona mkurupukaji na Mshambenga tu.

Mkuu,
Nitake radhi, hata mi simuoni Kitine ni shujaa kama ulivyonitaja..
 
Wajua wizi aliofanya kitine kwa nchi hii?
Membe ndio alimuumbua na sasa kitine anakurupuka tu
Kwa nafasi aliyokuwa nayo kitine haitakiwi kuzungumzia tuhuma kama hizo bila kumtaja muhusika moja kwa moja ili hatua zichukuliwe
OTIS

Kumbuka Dr. Kitine alituhumiwa na akasulubiwa, yawezekana ilikuwa fundisho kwake. Kwa mantiki hiyo taarifa yake yaweza kuwa na mashiko sana katika hali ya uchumi wa nchi yetu.

Whether alifanya chochote hapo nyuma hiyo haituhusu, cha kujiuliza ni kwamba je taarifa au tuhuma hizo ni za kweli? Kama ni kweli then ataje ni nani anamtuhumu. Naamini mtu kama yule kwa status yake hawezi kuwa amekurupuka tu, na hata kama ameongea eti kisa ya ugomvi wake na membe kama inavyosemekana hiyo sisi haituhusu cha muhimu ni authenicity of the allegations!

Kitine hebu ita waandishi utupe uhondo zaidi. Ila usijiumeume tena, mwaga radhi mzee we yako yalimalizwa na pesa ulilipa na uwaziri ukang'oka you have paid the price kwa nini wengine nao wasifanye hivyo. We walete tuwasulubu. Ukishindwa we mpatie hizo evidence Dr. Silaa! Moto uwake.
 
Kweli kabisa Bondpost umenena...
 
Du kumbe uongozi mpaka usikie sauti? sauti kutoka wapi? manake kwa dagama,membe,na sita nahsi zinatoka kwa shetani na sio mungu...malecela anadai kitine mwizi vp zile mln 500 alizopewa babake na mama kutoka kwa j.patel nazo zilikua alalI jaribu kuacha unafiki na fitina.
 
Kweli kabisa Bondpost umenena...

Ngoja tumsikilizie mzee labda atafunguka, ila asipokuwa muwazi atakuwa amegaragaza P yake kwa kiwango cha juu sana! Kwa ubosi wa kule chiriku na akimbwela nitamshangaa maana aliamua kufunguka sasa kapewa go ahead na mzee wa vingwendu sasa isijekuonekana yeye kitine ndo kingwendu.
 
- Mkuu PM vipi tena Kitine amemuita Membe, mwizi anayeficha hela nje agombee urais nazo, sasa akiitwa kingedu hutaki vipi? Una tatizo na Membe nini mkuu wangu, hafai kwa kosa gani hasa alilofanya kwenye policies zake akiwa Wizara ya nje?

- Kwenye kampeni za siasa kuchafuana ni kawaida, lakini hukalii kukumbatia ya zamani unasahau unaanza upya, I mean wacha chuki na Waziri Membe, kama ana makosa kwenye policies zake ziseme, lakini ya kampeni za siasa yalishapita sasa yupo kwenye kutawala, onyesha mapungufu yake kiutawala,

- Kitine hana u-senoir wowote ni simply muongo sana na ni mwizi, tena yeye na mkewe, ila kwa vile system yetu ni ya kusameheana ndio maana ana ubavu hata wa kuita wengine wezi, nashangaa mtu makini kama wewe kumuita a proven thief wa hela za wananchi kwamba ni senior, senior wa nini hasa? labda wizi wa hela za wananchi, wananchi wanakufa Muhimbili pale kwa kukosa dawa, wengine wanadanganya na kuiba hela za wananchi hao hao na kwenda nje kufanya shopping, wewe unamuita senior pleaseee!

- Waziri Membe na wananchi wote wa nchi hii wana haki ya kugombea anything, hawa kina Kitine ndio tatizo kubwa sana kwa taifa letu, maana ni majungu majungu tu alipokuwa usalama aliwahi kumakamata nani? PM wewe nakuheshimu sana kwani najua ni mtu makini sana lakini huwa una tatizo sana na mtu yoyote anayetaka uongozi CCM, isipokuwa Lowassa tu, huwa sikuelewi!

William.

Unaendelea kunisikitisha sana. Jaribu kumtumia mzee wako kwa ushauri mkuu. Namuamini sana mzee wako katika medani za usalama. Kaa nae vizuri usije muaibisha naamini he expects of you a lot.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
- Mkuu PM vipi tena Kitine amemuita Membe, mwizi anayeficha hela nje agombee urais nazo, sasa akiitwa kingedu hutaki vipi? Una tatizo na Membe nini mkuu wangu, hafai kwa kosa gani hasa alilofanya kwenye policies zake akiwa Wizara ya nje?

- Kwenye kampeni za siasa kuchafuana ni kawaida, lakini hukalii kukumbatia ya zamani unasahau unaanza upya, I mean wacha chuki na Waziri Membe, kama ana makosa kwenye policies zake ziseme, lakini ya kampeni za siasa yalishapita sasa yupo kwenye kutawala, onyesha mapungufu yake kiutawala,

- Kitine hana u-senoir wowote ni simply muongo sana na ni mwizi, tena yeye na mkewe, ila kwa vile system yetu ni ya kusameheana ndio maana ana ubavu hata wa kuita wengine wezi, nashangaa mtu makini kama wewe kumuita a proven thief wa hela za wananchi kwamba ni senior, senior wa nini hasa? labda wizi wa hela za wananchi, wananchi wanakufa Muhimbili pale kwa kukosa dawa, wengine wanadanganya na kuiba hela za wananchi hao hao na kwenda nje kufanya shopping, wewe unamuita senior pleaseee!

- Waziri Membe na wananchi wote wa nchi hii wana haki ya kugombea anything, hawa kina Kitine ndio tatizo kubwa sana kwa taifa letu, maana ni majungu majungu tu alipokuwa usalama aliwahi kumakamata nani? PM wewe nakuheshimu sana kwani najua ni mtu makini sana lakini huwa una tatizo sana na mtu yoyote anayetaka uongozi CCM, isipokuwa Lowassa tu, huwa sikuelewi!

William.

Much as ambavyo nitashangazwa na kushtushwa pale mtu anapopinga kwamba mathalan Jaji Warioba, Dr. Salim, Mzee Butiku, Mzee Kaduma, ama Mzee Malecela si ma-senior ndivyo ambavyo vile vile nitashangazwa pale mtu anapopinga kwamba Mzee Kitine si senior kwa kigezo ati ni mwizi. Hivi Nchi hii watu wakianza kuzungumzia waizi ni nani atakayepona ama ni nani atakaye kuwa na ujasiri wa kumtupia mawe mzee Kitine??

Tunarudi kule kule kwenye kauli na matamko unaweza tamka kitu ukakuta kinaathiri kizazi chako cha kwanza hata cha mwisho. Kwa hiyo wizi wa Kitine (kama upo) ndio usio mpa uhalali wa kuwa senior?? Ama wizi huo (kama upo) ndio usiompa Kitine uhalali wa kutaja wezi wengine wa Nchi hii??

William umenishtua sana nawe kuhusisha na kutaja mpaka mke wa Kitine humu kama vile ambavyo jana nimeshtushwa na namna ambavyo watu walikuwa wakichangia thread yako kwa kuhusisha Familia yako very disappointing. Gonga hoja moja kwa moja wake, watoto, sijui marafiki kama tumeamua kufikiri beyond our scope hawana nafasi humu ni sawa na vile ambavyo tunachanganya hoja na mimatusi na kashfa mbali mbali.

Pale juu umekubali mwenyewe kwamba kwenye siasa mambo ya kuchafuana ni ya kawaida, hapa chini unasema tena watu kama kina Kitine wamejawa na majungu sasa nani awezaye kuthibitisha kuwa hayo majungu ya Kitine yaweza kuwa moja kati ya hizo siasa za kuchafuana??

Iwe iwavyo ni lazma ifikie mahali tujue namna ambavyo ushabiki na mapenzi vinaweza kuathiri uzalendo pamoja na utu wa mtu.

MEITINYIKU L. Robinson
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mzee Kitine hajataja jina, au Membe anamjua mtu anayemzungumzia Mzee Kitine?

Naona tunasahau kuwa kikulacho ki nguoni mwako....when spies fight you better watch out. Hapo hakuna interest za nchi wala nini...ni namna ya kupata ukubwa, sifa na madaraka. But this Membe..naye...mhhhh!
 
- Mkuu PM vipi tena Kitine amemuita Membe, mwizi anayeficha hela nje agombee urais nazo, sasa akiitwa kingedu hutaki vipi? Una tatizo na Membe nini mkuu wangu, hafai kwa kosa gani hasa alilofanya kwenye policies zake akiwa Wizara ya nje?

- Kwenye kampeni za siasa kuchafuana ni kawaida, lakini hukalii kukumbatia ya zamani unasahau unaanza upya, I mean wacha chuki na Waziri Membe, kama ana makosa kwenye policies zake ziseme, lakini ya kampeni za siasa yalishapita sasa yupo kwenye kutawala, onyesha mapungufu yake kiutawala,

- Kitine hana u-senoir wowote ni simply muongo sana na ni mwizi, tena yeye na mkewe, ila kwa vile system yetu ni ya kusameheana ndio maana ana ubavu hata wa kuita wengine wezi, nashangaa mtu makini kama wewe kumuita a proven thief wa hela za wananchi kwamba ni senior, senior wa nini hasa? labda wizi wa hela za wananchi, wananchi wanakufa Muhimbili pale kwa kukosa dawa, wengine wanadanganya na kuiba hela za wananchi hao hao na kwenda nje kufanya shopping, wewe unamuita senior pleaseee!

- Waziri Membe na wananchi wote wa nchi hii wana haki ya kugombea anything, hawa kina Kitine ndio tatizo kubwa sana kwa taifa letu, maana ni majungu majungu tu alipokuwa usalama aliwahi kumakamata nani? PM wewe nakuheshimu sana kwani najua ni mtu makini sana lakini huwa una tatizo sana na mtu yoyote anayetaka uongozi CCM, isipokuwa Lowassa tu, huwa sikuelewi!

William.

Acha uwongo wewe,

Ni wapi Kitine amemtaja Membe?
 
MAFAHARI WAKIGOMBANA WE
CHUKUA JEMBE UKALIME! Hapa wanaumbuana wao kwa wao, nae membe
kilichomfanya ajibu lile swali ni nini? Kwani alikuwa na haja ya kujibu
tena mpaka aite watu VINGWENDU? Ukirusha jiwe gizani ujue limempata.
Watanzania wenzangu nimeamini viongozi wenye maadili ya uongozi kwa nchi
hii hatuna labda tumuache mzee Dr. Shein labda.

aliulizwa swali kwenye press conference!
 
- mkuu pm vipi tena kitine amemuita membe, mwizi anayeficha hela nje agombee urais nazo, sasa akiitwa kingedu hutaki vipi? Una tatizo na membe nini mkuu wangu, hafai kwa kosa gani hasa alilofanya kwenye policies zake akiwa wizara ya nje?

- kwenye kampeni za siasa kuchafuana ni kawaida, lakini hukalii kukumbatia ya zamani unasahau unaanza upya, i mean wacha chuki na waziri membe, kama ana makosa kwenye policies zake ziseme, lakini ya kampeni za siasa yalishapita sasa yupo kwenye kutawala, onyesha mapungufu yake kiutawala,

- kitine hana u-senoir wowote ni simply muongo sana na ni mwizi, tena yeye na mkewe, ila kwa vile system yetu ni ya kusameheana ndio maana ana ubavu hata wa kuita wengine wezi, nashangaa mtu makini kama wewe kumuita a proven thief wa hela za wananchi kwamba ni senior, senior wa nini hasa? Labda wizi wa hela za wananchi, wananchi wanakufa muhimbili pale kwa kukosa dawa, wengine wanadanganya na kuiba hela za wananchi hao hao na kwenda nje kufanya shopping, wewe unamuita senior pleaseee!

- waziri membe na wananchi wote wa nchi hii wana haki ya kugombea anything, hawa kina kitine ndio tatizo kubwa sana kwa taifa letu, maana ni majungu majungu tu alipokuwa usalama aliwahi kumakamata nani? Pm wewe nakuheshimu sana kwani najua ni mtu makini sana lakini huwa una tatizo sana na mtu yoyote anayetaka uongozi ccm, isipokuwa lowassa tu, huwa sikuelewi!

William.
hahahah toto la fisadi limeahidiwa uongozi linatetea upumbavu!
Membe hafai na mnafiki tunalijua hilo!
 
Back
Top Bottom