Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,505
113,620
Wanabodi, naomba kukiri nimeandika thread hii, baada ya kuwa inspired na post hii ya mkuu huyu kwenye thread hii Udhaifu na unafiki wa vyombo vya habari!
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , kwanza asante kwa hii!, na kwa vile mimi ni mwandishi wa habari, nimeguswa, hivyo nachangia, ambapo nitajibu hoja zako tano ulizo raise, pia nitaelimisha kidogo na mwisho kutoa maoni yangu!.

Majibu ya hoja zako 5 za msingi.

  1. Baada ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernad Membe,kukanusha tuhumu za ndege ya raisi wa China kubeba meno ya tembo,vyombo vyote vya habari leo vimeipa kipaumbele habari hiyo.
  • Habari ya Membe kupewa umuhimu wametumia kanuni ya proximity, prominence na big names makes news. Habari ile ilitangazwa na vyombo vya mbali, hivyo tukio likitokea mbali hata kama linatuhusu, due to proximity sio big deal sana kama taarifa ya Membe, habari ile ilipatikania mtaani tuu, taarifa ya Membe imetolewa bungeni kwenye the official channel hivyo taarifa ya Membe ina more prominance kuliko taarifa ya Al Jazeera!, na mtoa taarifa ile ya Aljazera kwa uoudience ya Tanzania, ni no body!, wakati mjibu tuhumu huku kwetu Membe ni somebody!, hivyo bignames makes news!.
2. Cha kushangaza ni hivi hivi vyombo vyetu vya habari ambayo vilishindwa kuripoti habari hii na hata Television zetu hazikuthubutu kuonyesha video clip hiyo.
Habari za nje zinageuzwa habari za ndani kwa kutumia monitoring!, kila chombo kina vyombo vya habari ambavyo zinaviamini na hivyo hufanya monitoring kupia the the media they can trust!, TBC wanafanya monitoring Xinhua, ITV wanamonitor BBC na CNN, Star TV wana monitor BBC na VOA, Chanel Ten wao wana monitor Sky News!. Habari ile ilitangazwa na Aljazeera!, hakuna news TV bongo ambayo in a monitor Aljazeera, hivyo hakuna kosa kwa TV zetu kutoionyesha hiyo habari ila naungana na wewe kuwa hata kama Aljazeera sio news source kwetu, kufuatia kanusho la Membe, media zetu zilipaswa kuitafuta ile clip na kuiweka as background source!.
3. Sasa kwa hali hii,hii si ni sawa na kuripoti habari ya upande mmoja tu.Je, huyu mwananchi ambae hajaona hiyo video wala kusikia kwa undani kuhusu hujuma hiyo,atawezaje kupima na kujua nani mkweli na nani muongo?.
  • Hili la one sided reportage, nakubaliana na wewe 100%.
4. Nimalizie kwa kusema waandishi na pengine hata wamiliki vyombo vya habari wa kitanzania ni waoga na kwakweli hamuitendei haki taaluma yenu.
  • Hili la uoga pia lipo na lipa kwa maeneo mawili: Vyombo vya Habari wa Umma, na Vyombo vya Habari Binafsi. Nkianzia na Vyombo vya habari vya umma, ikiwemo TBC, hivi vinapaswa kuwa Public Media kwa kutanguliza maslahi ya umma, na viko paid by tax payers money kutokea serikali, hivyo "he who pays the piper!, may call the tune!", vyombo vyetu vya umma badala ya kuutumia umma na kutanguliza maslahi ya umma, vimegeuka ni vyombo vya serikali kuitumikia serikali!. Tido alijaribu kidogo, ila sote tunakijua kilichomkuta!. Baada ya kilichomkuta TIDO, Mshana hawezi kufanya kosa lile lile la kulikata tawi alilokalia!. Tukija kwenye vyombo binafsi, vyote vinategemea survival kwa kufanya biashara, mtangazji mkubwa kabisa ni taasisi za umma wadhamini wakubwa ni makampuni ambayo nayo yanaitegemea serikali kufanya biashara. Kifo cha kile kipindi cha "Kiti Moto", kimenifundisha kama serikali haiko happy, wadhamini watakukimbia!. Na hata ikitokea ukadhaminiwa, wenye TV wao wakihisi serikali won't be happy!, hawakubali kupokea kipindi!.
5. Kuripoti habari hii kwa mtindo huu,si uzalendo hata kidogo bali ni "ukanjanja" of the highest order.
  • Hili la mwisho la uzalendo na ukanjanja sio kweli na nimeumia kidogo umetutukana media zetu zote kuwa ni kanjanja!. Kwenye news za kimataifa, media zetu zinapaswa kutanguliza uzalendo kwa nchi yetu kwanza, hivyo zikipatikana habari mbaya kuhusu nchi yetu, hatuziripoti, na vivyo hivyo ndivyo wanavyofanya vyombo vya mataifa mbalimbali. Mfano ilipotokea genocide ya Rwanda, CCN walionyesha mutilated bodies za Waafrika zikielea Ziwa Victoria, na kwenye September 11, huna picha ya dead body yoyote ilionyeshwa kwenye TV zao zaidi ya black bags!, hata kwenye vita vya Irak au Afghanistan, inaonyeshwa jinsi majeshi ya wavamizi yanayoteketeza!, lakini wao hawaonyeshi chochote kuhusu vipigo vyao!. Hivyo vyombo vyetu vya habari kutoonyesha "uwongo" wa wenye vivu, ndio uzalendo wenyewe na sio ukanjanja!.
My Take.
Sisi wengine wenu, intellect ya mtu, unaiona usoni, machoni na anapozungumza, hivyo hata fool kabisa akinyamaza kimya, huwezi kumjua he is a fool mpaka atakapoongea ndio foolishness yake inajulikana!. Membe ni just a fool fulani aliyebahatika kuukwaa u MFA, akiongea, ukimsikiliza na kumtazama usoni, hiyo foolishness yake inaonekana wazi, na wanaoweza kudanganya wengi ni wale majuha, tuliowajaza kwenye lile jumba/mjengo kule Dodoma ambao sijawasikia wakihoji the subject matter ya kadhia hii, zaidi ya kupiga tuu makofi!.

Kwa tunaiojua sheria ya diplomatic bags, tunajua inaratibiwa na The Vienna Convention, host country haiwezi kujua chochote kinachobebwa na diplomatic bags ya nchi nyingine!, hivyo only fools tuu ndio wata believe kanusho la Membe!.

The fact is hata rais wetu anaposafiri, mizigo ya msafara wote hupitia diplomatic bag, kama safari ni kesho, leo jioni watu wote kwenye msafara hupeleka mizigo yao ikulu, mkifika mnaletewa hotelini!. Nakumbuka nikiwa media journalist niliwahi kuwapo kwenye misafara, jamaa wa "Ilala" si wakaniletea "mizigo" yao niwabebe kwa pesa ndefu kweli kweli, kama unapenda pesa!, you can't say no!. Dhamira yangu haikunituma, niliwagomea! wakanicheka kuwa nitakufa masikini!.

Only the fools and the insane ones ndio wanaoweza kukanusha kilichobebwa kwenye diplomatic bag ya nchi isiyo yako!. Kwa wanaokikumbuka kisa cha Umaru Dikko wa Nigeria, kilichochotea mwa 1984 wakati serikali ya kiraia ilipinduliwa siku ya mkesha wa mwaka mpya, mawaziri wengi wa serikali hiyo wakatiwa nguvuni, Dikko aliyekuwa waziri wa usafirishaji alifanikiwa kutorokea London Uingereza. Serikali ya Nigeria ikaomba arudishwa, serikali ya Uingereza ikagoma!. Serikali ya Nigeria ikawakodi makomandoo 3 wa Israel, wakamteka Dikko na kumdunga sindano ya kupoteza fahamu, wakamuweka kwenye box na kulilebel ni diplomatic bag, tayari kusafirishwa kupelekwa Nigeria!, thank to Scotland Yard na anti terrorist squad ya UK, mpango huo ulimbumbulukia airport, serikali ya Uingereza ilipopangua kwa nguvu hiyo parcel, kilichofuatia ni kuvunjika kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Nigeria na Uingereza.

Kwa maoni yangu, kanusho la Membe ni just nothing!, lakini kwa jinsi Wachina walivyo wakombozi kwetu, sioni hata kwa nini tusiwakabidhi tuu ile Ivory Room!, wenzetu Wakenya Ivory zikikamatwa zinateketezwa, sisi tukizikamata, tunazihifadhi kule Ivory Room na kila siku zinapungua!, nani anaweza kudai eti rais wetu hajui Ivory huko Ivory Room zinapunguaje?!. Kwa vile Wachina ndio wakombozi wetu, na sisi tunazo Ivory hatuzihitaji lakini tumezihifadhi for what?!, tuwape tuu Wachina wanaozihitaji, tujue moja na sio kuja na haya makanusho ya Kitoto!.

Mabingwa wa diplomasia, tuelimisheni, jee Mhe. Membe kama MFA, anao uwezo wa kujua kilichomo ndani ya "Diplomatic Bag" ya mzigo wa nchi yoyote?!. Kama Waingereza iliwabidi wavunje sheria na kuvunja uhusiano wa kibalozi na Nigeria kisa ni kujua tuu kilichomo ndani ya Diplomatic Bag ya Nigeria, jee huyu Membe wetu, uwezo huo anao?, ameupata wapi?, anawezaje kukanusha kitu ambacho hana uwezo nacho?!.

Na tukianza kudanyanyana hivi sasa, na wadanganyifu hawa, sio tuu wanatudanganya sisi, bali wanalidanya Bunge letu tukufu!, ikiwa hivi ni MFA, danyanya zenyewe ni hizi, hiyo 2015, atakapokuwa ndiye yeye hali itakuwaje?!

"Tusidanganyane kabisa!. kuna watu hawatufai kabisaa!, hata wawe na sura nzuri vipi, na nywele zao nyeusi vipi kwa kupaka kanta ili waonekane vijana ila ndani ni mvi tupu!, huku wakiongea uwongo kwa mapozi mengi mchana kweupe!" Kama hawafai, ni hawafai tuu!.

Paskali


Sikiliza kwa makini hizi clips 2.
Update 12/05/2023
Bernard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Imani umeitunza,
Mwendo umeumaliza!.
Bwana alileta
Bwana ametwaa
Jina lake Lihimidiwe
RIP Bernard Cammilus Membe
Paskali
 
Bro Pasco mara kadhaa ITV wamekua wakiripot habar kupitia Aljazeera ni mara nyingi tu.

Suala la Ukanjanja na kukosa uzalendo kwa waandishi lipo tena lipo sana tunao jamaa zetu au ndugu zetu ni waandishi hakuna haja ya kutajana hapa ila 'Makanjanja' wapo sana,na waandishi wakosa uzalendo pia wapo,waandishi ni moja ya watu corrupt sana 'wazee wa BAHASHA ZA KAKI' so kwa suala la Pembe za ndovu kutoandika ai kutoipa kipaumbel pia kunahusishwa na kukosa uzalendo?
 
Uzi mzuri lakini nataka nikupe tuu hili ONYO alilolitoa Membe kuwa Maadui zake 2015 watahamia Kenya

Hivyo basi Pasco ningependa kukutahadharisha kuwa Membe kupitia connections zake za Usalama wa Taifa (TISS) ambako japo alifukuzwa kazi bado ana connections atakutumia watu wa kukuhamishia Kenya kwa sababu una m criticize na moja kati ya sifa kubwa za rais wetu mtarajiwa ni kupenda visasi na pia mtu wa kuwamaliza maadui zake

Threads kama hii ni uthibitisho tosha kuwa unamharibia njia yake ya kuelekea Ikulu mwakani na jiulize Ikifika Novemba utakuwa ndani ya ardhi ya Tanzania au nje?

kama huamini soma hili ONYO alilolitoa Ndugu Membe Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya!

ukweli ndio huo
 
"Tusidanganyane!. Kuna watu hawatufai kabisaa!, hata wawe na sura nzuri vipi, huku wakiongea uwongo kwa mapozi mengi mchana kweupe!" Kama hawafai, ni hawafai tuu!.

Mkuu Pasco kwa ufafanuzi ijapokuwa wewe siyo mwana diplomasia lakini mmetoa mchango wako kuhusu diplomatic bag.kanusho halijaishia kwa membe limendelea kwa balozi wa China,Nyalandu na Lembeli wote kwapamkwapamoja ukiwauliza mliofungua hiyo diplomatic bag watakuambia hata hawajawahi kuiona wao wamemsikia membe vijana wangu walikesha Serena hotel kufanya staffing ya hizo bidhaa usiku kucha.
 
Agag order(also known as agagging orderorsuppression order) is an order, typically a legal order by a courtor government, restricting information or comment from being made public, or in some cases, passed onto any unauthorized third part.a 'gag law' may limit freedom of the press, by instituting censorshipor restricting access to information.

Sijui hata hivyo kama gag order inatumika hapa tz.
 
Uzi mzuri lakini nataka nikupe tuu hili ONYO alilolitoa Membe kuwa Maadui zake 2015 watahamia Kenya

Hivyo basi Pasco ningependa kukutahadharisha kuwa Membe kupitia connections zake za Usalama wa Taifa (TISS) ambako japo alifukuzwa kazi bado ana connections atakutumia watu wa kukuhamishia Kenya kwa sababu una m criticize na moja kati ya sifa kubwa za rais wetu mtarajiwa ni kupenda visasi na pia mtu wa kuwamaliza maadui zake...

Membe anautaka Urais kwa Gharama yeyote ile Yale Mapesa ya Marehemu Gadafi atayafukua toka kwenye Mahandaki alikoyaficha baada ya kumdhulumu Barozi wa Libya kisha akampiga kipapai akajiua ili Siri isifichuke lakini kwa uwezo wa Mungu sasa kila kitu kipo wazi Pesa za Gadafi zimeandaliwa kununua njia ya kuelekea ikulu huku akitatibu na kugharamia watu wa kumchafua Lowasa kwenye mitandao baada ya kubaini Kuwa Kati ya wale wanaowania kwenda ikulu Lowasa Pekee ndiyo Tishio kwake.

Membe Hana mda wa kuhangaika na kazi zingine , mda wote yupo busy akiwaza jinsi ya kufanya ili aje awe Rais.
 
Membe mda wote huwa anawaza jinsi ya kufanya ili awe Rais Hana time ya kuhangaika na mengine, Mapesa ya Gadafi yanamzuzua hataki kusikia mtu anawania Urais anatamani awe Mgombea pekee Kama ilivyokuwa kwa Ally Hassan Mwinyi Enzi zile ambapo aligombea na Kivuli.
 
Ndugu Pasco

Wewe unadai Mhe. Membe hana uwezo wa kufahamu kilichoko kwenye diplomatic bag kwa sababu ya uwepo wa The Vienna Convention halafu hapo hapo unadai Scotland yard walifahamu kilichokuwa kwenye diplomatic bag.

Sasa kama Scotland Yard walifahamu kilichoko kwenye Diplomatic bag kwa nini vyombo vya ulinzi nchini wasifahamu kisichokuwa kwenye diplomatic bag.

Pasco unaposema fulani ni muongo lazima ulete ushahidi wa uongo wake nje ya hoja za kimazingira bali ndani ya vithibiti.

Ni ajabu kwa mtu kukubali kile kinachosemwa bila ushahidi lakini kinakataliwa kile kinachosemwa kama kanusho.

Jengeni hoja zenye ushahidi na siyo hoja zenye hearsay.
 
Ndugu Pasco

Wewe unadai Mhe. Membe hana uwezo wa kufahamu kilichoko kwenye diplomatic bag kwa sababu ya uwepo wa The Vienna Convention halafu hapo hapo unadai Scotland yard walifahamu kilichokuwa kwenye diplomatic bag.

Sasa kama Scotland Yard walifahamu kilichoko kwenye Diplomatic bag kwa nini vyombo vya ulinzi nchini wasifahamu kisichokuwa kwenye diplomatic bag...
Mkuu Mwanadiwani, kwanza heshima mbele, pili asante kuutembelea uzi wangu, naamini mkuu Mwanadiwani, hukuiona hiyo main story ya Aljazeera bali umelisikia tuu kanusho la Membe!, ukiangalia kilichosemwa na kanusho ni vitu viwili tofauti!.

Kwenye tuhuma kuna facts na uthibitisho, kwenye kanusho ni blah blah tupu!.

Sina uhakika hata kama unaijua hiyo Viena Convention, na inazumgumzia nini kuhusu diplomatic bag, ndio maana nikauliza Mhe. Membe anao uwezo wa kujua the content ya diplomatic bag?!. Kisa cha Umaru Dikko unakijua?!.

Kwa kukusaidia wewe na wengine wasio jua, hebu google Umaru Dikko uone mazingira ya kufunguliwa kwa diplomatic bag na consequences zake!.

Sisi wengine wenu, uongo tunaosoma machoni na usoni na sio kutegemea matamko kuwa hiki na kile ni uongo!.

Alichosema Membe ni uongo mtupu ukweli ni kuwa pembe za ndovu zimeondoka!.

Naamini uko well connected, find out kuhusu maximum security ya Ivory Room yetu!, then jiulize hizo pembe za ndovu zinapungua kivipi kutoka humo?!. Wenzetu Kenya wakizishika tuu, wanaziteketeza!, sisi tukizishika, tunazihifadhi Ivory Room!, for what?!, find out hizo Ivory zinazotoweka Ivory Room kama kuna yeyote aliyewahi kuulizwa au kuchukuliwa hatua zozote!.

Nakuhakikishia hata wale Twiga, kama wangeweza ku fit kwenye diplomatic bag that big!, wangeshafirishwa under diplomatic bag, na kusingekuwa na kelele zozote hizi!.

Pasco.
 
Membe anautaka Urais kwa Gharama yeyote ile Yale Mapesa ya Marehemu Gadafi atayafukua toka kwenye Mahandaki alikoyaficha baada ya kumdhulumu Barozi wa Libya kisha akampiga kipapai akajiua ili Siri isifichuke lakini kwa uwezo wa Mungu sasa kila kitu kipo wazi Pesa za Gadafi zimeandaliwa kununua njia ya kuelekea ikulu huku akitatibu na kugharamia watu wa kumchafua Lowasa kwenye mitandao baada ya kubaini Kuwa Kati ya wale wanaowania kwenda ikulu Lowasa Pekee ndiyo Tishio kwake.Membe Hana mda wa kuhangaika na kazi zingine , mda wote yupo busy akiwaza jinsi ya kufanya ili aje awe Rais.

Our level of tolerance for corruption in Tanzania is just amazing. One of the great Greek Philosopher once said "......it is in the nature of minds to harm the small thieves and to elect the greater ones in public offices..."
 
Asante Pasco! Nilipata shida kuamua kukubaliana na Mh Membe au la. Sasa umenirahisishia, ni kweli haya mambo yalitokea na Membe anaficha. Au Pengine haikutokea ila Kwa uzoefu wa kutoa maelezo Rena Rena basi Membe aka tokes maelezo yanayozidi kuaibisha taifa.

Hvi Kwanini tunakubali kujidhalilisha hivi! Hebu angalia TPDC wamengangania kutoweka mikataba hadharani kumbe kulikuwepo na doubling of the contract price - inflating from $600m to $1,200m if Mbowe is be believed!
 
Jana nilili lalamika kuhusu uharaka wa Membe kukanusha bila kuwa na uchunguzi wa kina....! Jamaa fulani hapa JF wakanishambulia. Ingawa uzi huu umeletwa kumkandamiza Membe zaidi ikizingatiwa mwanzisha uzi ana msapoti 'mh' fulani kuelekea 2015, haikuwa sahihi kwa Membe kutoa kanusho lile na kwa staili ile.
 
Mkuu Mwanadiwani, kwanza heshima mbele, pili asante kuutembelea uzi wangu, naamini mkuu Mwanadiwani, hukuiona hiyo main story ya Aljazeera bali umelisikia tuu kanusho la Membe!, ukiangalia kilichosemwa na kanusho ni vitu viwili tofauti!.

Kwenye tuhuma kuna facts na uthibitisho, kwenye kanusho ni blah blah tupu!.

Sina uhakika hata kama unaijua hiyo Viena Convention, na inazumgumzia nini kuhusu diplomatic bag, ndio maana nikauliza Mhe. Membe anao uwezo wa kujua the content ya diplomatic bag?!. Kisa cha Umaru Dikko unakijua?!..

imekaa kizalendo!
 
Mlinganishe huyu uliemtaja jina, uulinganishe umakini wake kwa kumcompare na huyu mpiga firimbi wetu wa hamelini (bungeni)!.

Pasco.

kumfanisha Lowassa na Membe ni sawa na kumfanisha Makonda na Warioba.

Lowassa ni kiongozi, Membe ana ongoza.
 
Membe ni mzee wa "Kanusha kanusha", kama ile issue ya Rada na Andrew Chenge. Anajitahidi sana kutetea wizi.
 
Back
Top Bottom