Membe ajikaanga kwa mafuta yake

Membe ajikaanga kwa mafuta yake

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Katika hali ambayo inaonyesha dhahiri shahiri suala la mbio za urais ndani ya CCM linampa wakati mgumu Waziri wa mambo ya nchi za nje, Mhe. Bernad Membe amezidi kutoa kauli zenye maswali mengi.

Hiyo imetokea wakati akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM mjini Dodoma Membe amesema akifanikiwa kuwa Rais atapambana na rushwa kwa kuhakikisha anawaajibisha wapokea rushwa na kuwasamehe watoa rushwa wote ambao watakiri kutoa rushwa.

Kauli ya Membe anaitoa kinyume kabisa na sheria za nchi zinavyosema, kinyume kabisa na sheria ya rushwa nchini ilivyoainishwa kisheria.

Kwa mujibu wa sheria ya PCCA sheria No. 11/2007 section 15 inaeleza wazi kuwa "Anayetoa na kupokea rushwa wote ni wahalifu". Hivi ndivyo sheria inavyosema.

Leo hii Membe anaposema akiwa Rais atahakikisha wanaopokea rushwa ndio watakuwa wahalifu, hii sheria kaitolea wapi? Ni nani amempa madaraka Membe ya kuvunja sheria za nchi zilizotungwa na Bunge? Membe anataka kutuambia akiwa Rais hatafuata utawala wa kisheria, hapo utawala bora utatoka wapi? Bila ya kuwepo mtoaji rushwa, mpokeaji angetokea wapi?

Membe anataka kutuambia atakuwa mvunja katiba ya nchi atakayoiapa kuilinda endapo atafanikiwa kuwa Rais? Ina maana hata zile ahadi zake anaweza kuja kuzipindua na kufanya anayoyajua yeye kwani ameshaanza kutuonyesha dalili za kubadilika mbele ya safari. Hakika huku ni kuchanganyikiwa kwa wazi wazi anakoendelea kuonyesha Membe.

Membe hakuishia hapo bali ametoa kauli nyingine za kuchanganyikiwa wakati akielezea suala lake kuwa na undugu na Rais Jakaya Kikwete.

Membe amesema suala la yeye kuwa ndugu na Rais Kikwete endapo ni kweli au si kweli haliwahusu Watanzania ambao asilimia kubwa wamemjua wakati huu wa kuisaka Ikulu.

Membe ameonyesha wazi wazi kushindwa kukana undugu wake na JK na hivyo kushindilia maneno yanayozagaa mitandaoni ya JK na Membe kuwa ni ndugu wa damu.

Wapo baadhi ya watu wanaodai Baba yake halisi Membe ni Mzee Mrisho Kikwete ambaye alizaa na Cecilia John Membe ambapo kwa kabila la Wamwera uchukua jina la ukoo wa Mama na kulifanya ndio jina la ukoo wa mtoto. Ikumbukwe, Wamwera ni kabila linalofuata matrilenial system ambapo Mama ndiyo mwenye dhamana kubwa na mtoto.

Watu wamefukunyua undugu huo kufuatia kuona jitihada na nguvu za wazi wazi zinazofanywa na familia ya JK katika kuhakikisha undugunization ya kumrithisha kiti cha urais Membe kwa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kisultan ya kurithishana madarakani ilihali kuna mfumo wa kidemokrasia.
 
Naogopa Nisichafue Tu Hali Ya Hewa Ila..............................
 
Jambazi sugu na fisadi papa Lowassa kamwe hawezi kuwa Rais wa Tanzania. Ni mwizi ana fitina hana hoja hawezi kujieleza. Hana ubobezi wa aina yoyote.

Nguvu yake kubwa ni kinunua watz kwa nguvu ya pesa.
 
Mafisadi mbele kwa mbeleee

Ccm ccm aaaahaa chama chama fisadi ccm number onee....
 
Udugu wao hautukhusu muhimu tunataka mchapa kazi awe Babake au shemeji yake au Mume mwenzie
tunataka maendeleo....
 
Ni bora tuongozwe na fisadi au hata mwizi lakini tusonge mbele kuliko tuongozwe na mtu kama Membe ambae atendeleza yaleyale ya awamu ya 4.
 
Hapa anazungumziwa Membe! wewe uko Busy kumchafua Lowassa!!! Usikubali kuwa Robot !!! Inaonekana umelishwa maneno na wewe unayoatoa kama umewekewa umeme... Uwizi, Ufisadi wa Lowassa kwanini msianike hadharani? Watanzania si Wajinga tena: Fitna za Joka la Mdimu, plus kafara za kimwera na kuomba kwenye Makaburi hakuwezi kuwaondolea wananchi Umasikini uliokithiri kwenye nchi TAJIRI ... Lowassa hawezi kukubali Ujinga wa nchi za Magharibi kukwapua rasilimali zetu... Ndo maana tuna muunga mkono ...
Jambazi sugu na fisadi papa Lowassa kamwe hawezi kuwa Rais wa Tanzania. Ni mwizi ana fitina hana hoja hawezi kujieleza. Hana ubobezi wa aina yoyote.

Nguvu yake kubwa ni kinunua watz kwa nguvu ya pesa.
 
Suala la undugu wa Membe na JK lipo wazi sana.
Familia zao zote zinajua hilo.
Ridhiwani na familia ya JK wanamuita Membe Baba mdogo.
Sidhani kama wana ccm wataukubali huu usultani unaotaka kujengwa na familia ya JK
 
Membe hawezi kuwa Rais wa Njii hii...kwa hiyo hata mada hii haina umuhimu wa kuijadili........sio muda muafa kujadili ndoto, wakati matukio ya kujadili yapo
 
watanzania wamechoshwa na kuuza sura, wanataka Kiongozi mwenye maamuzi Magumu atakayewaondolea Watanzania Umasikini wao!
 
suzan lema

Tanzania mpya bila CCM inawezekana ...! ...coming soon!
Wewe Bwana Membe [wa Mrisho Kikwete]; Unamaanisha Kupinga na kukamata wala Rushwa ndani ya CCM au nje? au Kwa Serikali nzima? Sasa umefanya nini au unafanya nini sasa kuhusu hilo? au Umefanya nini? Wizi wa Escrow A/c ya juzi tu, ulifanya nini? Jamani!! Wizara ya Mambo ya Nje ni chaka kuu, ruuushwa? umeweza nini? Vumbi na sarakasi tu hizi!!
- Nrerere amesema .." anayesema ataweza, ukimwangalia usoni uone kweli analosema anakusudia na ataweza"! Sio Membe kamwe, na sio ndani ya CCM ya sasa!
 
Last edited by a moderator:
Jambazi sugu na fisadi papa Lowassa kamwe hawezi kuwa Rais wa Tanzania. Ni mwizi ana fitina hana hoja hawezi kujieleza. Hana ubobezi wa aina yoyote.

Nguvu yake kubwa ni kinunua watz kwa nguvu ya pesa.

Acha kutumia ubongo wa bata kufikiria kwa kutumia ubongo wa bata.wewe ni kibaka panya road unamtukana edo!!!!!
 
Back
Top Bottom