Membe ajikaanga kwa mafuta yake

Membe ajikaanga kwa mafuta yake

uyu membe bwana SIJUI ALIINGIAJE usalama wa taifa aisee AWA ndo wanaibisha miiko ya idara yetu yanii kutoa rushwa ni ruksa ila anayepokea ni hatari kwake ...... sasa inakuaje anikinzana na utawala wa sheria jamani sasa anautaka uraisi ata wapambe wake mliomo umu na yeye mnaona ni sahihi uyu mgombea wa WAMA anachokifanya ni maadili gani ya nchi aliyoyapitia? anadiliki kusema anagombea kwa sababu kafundishwa na MANGULA ila sio maslahi ya taifa? ivi iyo idara ya wapi iyo aliyopitia uyu membe
 
Katika hali ambayo inaonyesha dhahiri shahiri suala la mbio za urais ndani ya CCM linampa wakati mgumu Waziri wa mambo ya nchi za nje, Mhe. Bernad Membe amezidi kutoa kauli zenye maswali mengi.

Hiyo imetokea wakati akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM mjini Dodoma Membe amesema akifanikiwa kuwa Rais atapambana na rushwa kwa kuhakikisha anawaajibisha wapokea rushwa na kuwasamehe watoa rushwa wote ambao watakiri kutoa rushwa.

Kauli ya Membe anaitoa kinyume kabisa na sheria za nchi zinavyosema, kinyume kabisa na sheria ya rushwa nchini ilivyoainishwa kisheria.

Kwa mujibu wa sheria ya PCCA sheria No. 11/2007 section 15 inaeleza wazi kuwa "Anayetoa na kupokea rushwa wote ni wahalifu". Hivi ndivyo sheria inavyosema.

Leo hii Membe anaposema akiwa Rais atahakikisha wanaopokea rushwa ndio watakuwa wahalifu, hii sheria kaitolea wapi? Ni nani amempa madaraka Membe ya kuvunja sheria za nchi zilizotungwa na Bunge? Membe anataka kutuambia akiwa Rais hatafuata utawala wa kisheria, hapo utawala bora utatoka wapi? Bila ya kuwepo mtoaji rushwa, mpokeaji angetokea wapi?

Membe anataka kutuambia atakuwa mvunja katiba ya nchi atakayoiapa kuilinda endapo atafanikiwa kuwa Rais? Ina maana hata zile ahadi zake anaweza kuja kuzipindua na kufanya anayoyajua yeye kwani ameshaanza kutuonyesha dalili za kubadilika mbele ya safari. Hakika huku ni kuchanganyikiwa kwa wazi wazi anakoendelea kuonyesha Membe.

Membe hakuishia hapo bali ametoa kauli nyingine za kuchanganyikiwa wakati akielezea suala lake kuwa na undugu na Rais Jakaya Kikwete.

Membe amesema suala la yeye kuwa ndugu na Rais Kikwete endapo ni kweli au si kweli haliwahusu Watanzania ambao asilimia kubwa wamemjua wakati huu wa kuisaka Ikulu.

Membe ameonyesha wazi wazi kushindwa kukana undugu wake na JK na hivyo kushindilia maneno yanayozagaa mitandaoni ya JK na Membe kuwa ni ndugu wa damu.

Wapo baadhi ya watu wanaodai Baba yake halisi Membe ni Mzee Mrisho Kikwete ambaye alizaa na Cecilia John Membe ambapo kwa kabila la Wamwera uchukua jina la ukoo wa Mama na kulifanya ndio jina la ukoo wa mtoto. Ikumbukwe, Wamwera ni kabila linalofuata matrilenial system ambapo Mama ndiyo mwenye dhamana kubwa na mtoto.

Watu wamefukunyua undugu huo kufuatia kuona jitihada na nguvu za wazi wazi zinazofanywa na familia ya JK katika kuhakikisha undugunization ya kumrithisha kiti cha urais Membe kwa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kisultan ya kurithishana madarakani ilihali kuna mfumo wa kidemokrasia.
[/QUO
Wewe dada umeoga? pole kwa kutumika kama ile mipira! ni mtu hatari sana,unaleta mambo ya vijiweni! hayana kichwa wala miguu,hayana impact yoyote kwa taifa, halafu id yako ni fake una id nyingine imetuma uzi!
kwa maslahi ya nani unaleta huu utumbo?
Nenda face book hapa ni akili kubwa tu!

 
unaelewa unachokisema au ? sidhani kama unatambua umasikini unatokana na nini? mazingira unayoyasema yanawezekana kuwa unaweza kuwa na mtu mchapa kazi lakini pia anakuibia.

lakini kwenye nyadhifa za uraisi wa nchi haiwezekani kuwa na raisi mwizi huku akiwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu.

raisi ukiiba ujue sio siri kwa maana wapo watendaji wa chini wanashirikishwa sasa utamkemea nani pale mwingine ameiba kwa maana na wao wanajua wewe ni mwizi.

hapa kunatokea kuogopana, utakuta raisi hawezi kumkemea waziri wala mkurugenzi wa shirika maana hawa wa juu wanamjua basi yeye anabaki kukoromea watendaji wa chini ambao hawana lolote.

matokeo yake kila kiongozi unayemtuma kuingia mkataba fulani anaweka asilima yake kwenye mkataba na ama wananchi wanakosa mapato au kutoa fedha nyingi kununua kitu cha thamani ndogo. haya ndiyo yanayowanyima watanzania maendeleo na bila ya kuyadhibiti haya nchi yetu inaweza kufilisika kama ugiriki maana kwa sasa sote tunadhani hizo ndio njia za kupata.

hivyo mzembe na mwizi wote hawafai na hawezi kutuletea maendeleo, watanzania wapo wengi wenye sifa hatuwezi kuanza kulinganisha uzembe na wizi eti tuangalie afadhali.

Afadhali Rais fisadi na mwenye maamuzi magumu atakaye tuletea maendeleo kuliko Rais mstaarabu atakayetupa umaskini,
 
Mh Membe,
Kwa kuwa unajimwaga mchezoni kugombea kiti hicho kwa fweza za ma.-----, endelea tu lakini nasema hufai. Si kwa sababu nyingine yeyote bali kwa sababu umeshaonesha weye ni mtu wa kuyumba ka mlingoti mferu.
Swala la OIC ulilivuruga kabisa kiasi kwamba kama kitu kidogo tu hivyo ulishindwa, maamuzi mazito yatakuua bp bureeee. Kuliongoza taifa si kuongoza kabila lako.
Pili utaupata wapi huo uwezo wa kuyaleta hayo mabadiliko wakati hujaweza kutuonesha jinsi ulivyo pambana na hiyo rushwa hata kwenye kata yako ulipo zaliwa tu?? Utaiweza ya taifa hili?
Ningelikuwa ni weye, ningegombea ubunge wngu tu, Uraisi labda 2025
 
Wassira mla rushwa na hukumu ya mahakama ipo.Membe ndugu yake Jk..ushahidi wa DNA hakuna.Lowassa fisadi ushahidi huo hakuna rejea hotuba yake bungeni ya kujiuuzulu.Mzee Sitta kalihujumu BMK,mgogoro viongozi wa kidini..ushahidi dhahir shahir bado yataendelea kuja...what a simple country hata student anataka kuwa Lu Presidaaa
 
watanzania wamechoshwa na kuuza sura, wanataka Kiongozi mwenye maamuzi Magumu atakayewaondolea Watanzania Umasikini wao!

hivi wewe ni mtu au shetani au roboti?hili fisadi nguli lenye magonjwa sugu lowasa awe raisi kweli!no jokes any more.
 
Huyo fisadi jamani kaiba pesa ngapi na wapi wekeni data hadharani musiishie ni fisadi kufufuata maneno ya vijiweni!??
 
Jambazi sugu na fisadi papa Lowassa kamwe hawezi kuwa Rais wa Tanzania. Ni mwizi ana fitina hana hoja hawezi kujieleza. Hana ubobezi wa aina yoyote.

Nguvu yake kubwa ni kinunua watz kwa nguvu ya pesa.


HATA membe hana hoja nae empty basket hawezi kuzunguza kuhusu ufisadi wa lowassa ni kweli lakin ccm nani sio fisadi? wanazidiana kiwango tu eg messi vs ngasa wote wanasoka
 
Kitu gani kinamuaminisha membe kuwa anaweza kuwa rais??
 
#honoget Mbona Una Weweseka? Comment Yangu Nimemtaja Lowassa?! Kumbe Lowassa anawanyima usingizi Eeeh?! Polen sana Aisee
 
in short, hakuna anayefaa urais kutoka ccm. hata waseme nini hakuna anayefaa
 
#honoget Mbona Una Weweseka? Comment Yangu Nimemtaja Lowassa?! Kumbe Lowassa anawanyima usingizi Eeeh?! Polen sana Aisee

wewe naona unawatetea wezi wa mali za umma.wote waliousika na wizi au kuleta hasara kwenye taifa letu hawafai kupata madaraka tena.Tanzania yetu inaaribiwa na vibaka na manyangau ie lowasa,tibaijuka,chenge and co.Ndio nilichomaanisha
 
Inaonekana unatumika, ni vizuri lakini next time changanua unachoandika kabla ya kupost upuuzi. Kama uko makini membe alisema atapush kuleta mabadiliko ya sheria ya rushwa na sio kuibadilisha yeye mwenyewe. That is what great leaders do, they push for changes pamoja na wananchi and not dictate them. Kwa miaka mingi tumeng'ang'ania sheria ambayo haifanyi kazi vilivyo so kwanini tuing'ang'anie. Rushwa kwa asilimia kubwa huombwa meaning asilimia kubwa ya watoa rushwa ni victims, sasa if you criminalize victims how can they come forward kureport a crime? Ni kama kusema mbakaji na mbakwaji wote ni wahalifu. Na ndicho hicho sheria ya sasa inasema. Kwa mtu yoyote mwenye akili ataona ni sheria ambayo inahitaji kubadilishwa ili kutoa incentive kwa waathirika wakuu wa rushwa ambao ni watoaji.

Kawapime membe na jk DNA alafu ndiyo uje kuongea tena. Unakalia maneno ya kilabuni.
 
Membe hawezi kuwa Rais wa Njii hii...kwa hiyo hata mada hii haina umuhimu wa kuijadili........sio muda muafa kujadili ndoto, wakati matukio ya kujadili yapo
Kweli yakhee, huyo aongee na nape kwamba aachane na mtama. yeye bado mgombea ubunge. Sasa tuendelee kujadili white hair in white house.
 
Afadhali Rais fisadi na mwenye maamuzi magumu atakaye tuletea maendeleo kuliko Rais mstaarabu atakayetupa umaskini,
Hakuna fisadi anayeleta maendeleo hata mmoja ndiyo atazidi kutuangamiza kabisa akafie mbali huko.
 
suzan lema

Atabadili sheria ili kutimiza ndoto yake. Sheria sio msahafu. Jaribu kufikiri kidogo, yaani fikiri kidogo tu.
 
Last edited by a moderator:
Ni kwasababu rais anayomadaraka mengi!! ndio maana mh membe anaweza kubadili sheria.
 
songs of Lawino and O'coll: Kila MTU ana RAIS wake mfukoni na hana uhakika kama anaweza kukimbia mbio hizi za urais na akawa mshindi, hivo kila MTU ana mshawishi mwenzi atupe RAIS wake aendelee kushabikia RAIS wa mwenzake. na wengi wemetupa marais wao ambao walikuwa wanawaamini sasa wanashabikia walio mifukoni mwawenzao. yani unakutana na MTU Leo anamshabikia lowassa kesho mwigulu kesho kutwa makongolo siku yakupiga kula anatamchagu ambae hata haja wahi kimfikilia .kwahiyo kila MTU awe mpole na RAIS wake abari za kusema watanzania wanamtaka flani yaishe sema Mimi namtaka flani basiiiiiii
 
Back
Top Bottom