Membe amesema suala la yeye kuwa ndugu na Rais Kikwete endapo ni kweli au si kweli haliwahusu Watanzania ambao asilimia kubwa wamemjua wakati huu wa kuisaka Ikulu.
Membe ameonyesha wazi wazi kushindwa kukana undugu wake na JK na hivyo kushindilia maneno yanayozagaa mitandaoni ya JK na Membe kuwa ni ndugu wa damu.
Wapo baadhi ya watu wanaodai Baba yake halisi Membe ni Mzee Mrisho Kikwete ambaye alizaa na Cecilia John Membe ambapo kwa kabila la Wamwera uchukua jina la ukoo wa Mama na kulifanya ndio jina la ukoo wa mtoto. Ikumbukwe, Wamwera ni kabila linalofuata matrilenial system ambapo Mama ndiyo mwenye dhamana kubwa na mtoto.
Watu wamefukunyua undugu huo kufuatia kuona jitihada na nguvu za wazi wazi zinazofanywa na familia ya JK katika kuhakikisha undugunization ya kumrithisha kiti cha urais Membe kwa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kisultan ya kurithishana madarakani ilihali kuna mfumo wa kidemokrasia.
SIFA ZA 13 ZA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
[TABLE="width: 477"]
[TR]
[TD]1.
[/TD]
[TD]Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika Uongozi wa shughuli za Serikali umma na taasisi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.
[/TD]
[TD]Awe mwadilifu, asiyetiliwa shaka juu ya vitendo vya uadilifu mbele ya uso wa jamii ya Watanzania na awe mwenye hekima na busara.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3
[/TD]
[TD]Awe na angalau kiwango cha elimu ya chuo kikuu au elimu inayolingana na hiyo.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4
[/TD]
[TD]Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza Muungano wetu, umoja wetu, amani na utulivu wetu na mshikamano wa Kitaifa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5.
[/TD]
[TD]Awe mwepesi wa kuona mbali, asiyeyumbishwa na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya Taifa kwa wakati unaofaa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6.
[/TD]
[TD]Awe na upeo mkubwa na usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na dunia yote kwa ujumla.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7.
[/TD]
[TD]Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteta au ufashisti, bali awe mtu anayeheshimu na kulinda Katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na taratibu za nchi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8.
[/TD]
[TD]Awe mtetezi wa wanyonge, wa haki za binadamu, mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tama ya kujitafutia umaarufu wa mtu binafsi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9.
[/TD]
[TD]Awe mstari wa mbele katika kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza sera za CCM NA Ilani ya CCM ya uchaguzi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10.
[/TD]
[TD]Awe mpenda haki na mtu jasiri katika kupambana na dhuluma na maovu yote nchini.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]11.
[/TD]
[TD]Asiwe ni mtu ambaye anatumia nafasi yake ya Uongozi kujilimbilikizia mali.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]12
[/TD]
[TD]Awe ni mtu anayekubalika na wananchi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]13.
[/TD]
[TD]Awe na mtu makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa viongozi/watendaji na asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu/wajibu waliokabidhiwa ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na ufanisi.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]