Membe ahusishwa kulihonga kanisa Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe ahusishwa kulihonga kanisa Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Plato, Mar 17, 2011.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Habari ya kwenye majira la leo ya mtu mmoja kutoa mil.60 kwa tukio la kusimika askofu,ni aibu.wakatoliki hatujawahi kushindwa kuendesha sherehe zetu
  hii itaharibu kabisa image ya kanisa,na ya pengo alipoongea kwa ukali juzi.mafisadi ni watu hatari.yasijetokea ya askofu kuwekwa mfukoni,naam kanisa kuwekwa mfukoni.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kama hizo 60ml sio hela safi basi ingepaswa kanisa lizikatae kama askofu wa kule rukwa alivyokataa hela za Mbunge kusaidia vigango
   
 3. K

  Kaka deo Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kanisa katoliki liko imara, wangapi 2nawafahamu kwa majina wameshatoa hela nyingi tu, lakini wakileta mambo yao 2nawapiga chini" sie pesa sio issue' ni ukweli kwanza.
   
 4. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  hii Ni ngumu sana kubaini kama pesa ni chafu au safi.
  Kumbuka biblia inasema msihukumu, Kwakua kipima mtakachotumia kuwahukumu mwenzio ndio hicho hicho mtakachohukumiwa nacho.
  Tahadhari uliyotoa ni nzuri sana, tena sana. kama zingetolewa na kasusura tungezikataa, kwakua hizo zinajulikana ni Chafu.
   
 5. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Gazeti la Majira limendika leo na kumficha Waziri anayetuhumiwa kutoa mil 60 kwa ajili ya sherehe za kusimikwa Askofu Katoliki Dodoma. Taarifa ziso na shaka ni kuwa waziri huyo ni Membe
   
 6. g

  geophysics JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Karibu mgeni ingawa hukupiga hodi...... Kama wao wameficha wewe umejuaje au unaanza kupika jungu.
  CRAAPPPP
   
 7. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli alikuwa Membe nafurahi dot connekt umesema na wengine muige hilo, ukiona wanasema jina linahifadhiwa na unalijua rusha huku kwa wana familia
   
 8. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tudhani kwamba askofu msimikwa ni rafiki yake wa karibu,
  Je kuna kosa?
  Mbona sisi pia tunachangia shunguli nyingii tuu hata kutahiri watoto na hakuna kelele?

  labda kuna la zaidi na ziada,
  Yawekwe hadharani.
  Vinginevyo ni udaku/majungu.
   
 9. CPU

  CPU JF Gold Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  I smell udini:smash:
   
 10. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hebu tupe habari zaidi zilivyoondikwa kwenye gazeti.
  Je wameandika hivyo hivyo kwamba kanisa limehongwa au hii ni conclusion ya msomaji wa gazeti? Million 60 is just about USD 40K which I can also give to a church or any religious establishment for that matter.
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mhh, angalia mkuu usijekuwa unajifunga kamba unapotembea!! Mbele waweza shindwa........
   
 12. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama aliyetoa hela anategemea kuliweka kanisa mfukoni amechemka vikari sana maana nijuavyo hata pengo hawezi kujua watu gani wapo kwenye iteligensia ya kanisa hapa tanzania. Lina mfumo mkali unaorekebisha watu wake hasa viongozi kiulaini.
   
 13. TATE

  TATE Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimesikia tetesi ni Membe, kama ni kweli basi atakua anatafuta endorsement ya kanisa, nimeona dalili hizo mwenyewe, akiuzulia misa wakati wa matangazo lazima wamrushe kuwa yupo ndani, nabaki na maswali kwani yeye ni muumini kama wengine kuna ulazima wa kumrusha mtu kwenye matangazo sababu ni waziri, doesn't make sense, mbona wakubwa kibao wanasali makanisani lakini hawatangazwi? Nimemtoa heshima.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Yadaiwa lengo ni kujitakasa kwa kanisa urais 2015
  *Waumini watofautina, wasema angetoa Gongolamboto
  *Baraza Kuu UVCCM kuwasha moto, viongozi wakamiana


  VIBWEKA vya wanaCCM wanaotajwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka
  2015 vimeanza kwa kasi huku mmoja wa mawaziri akitajwa kumwaga mamilioni ya fedha kufadhili sherehe moja ya kidini.

  Chanzo cha kuaminika kimelidokeza gazeti hili kuwa miongoni mwa mikakati inayofanywa na makada hao sasa ni kuangalia namna wanavyoweza kuteka ngome za kidini kwa lengo la kuungwa mkono kwenye uchaguzi huo.

  Mbali na hilo wanasiasa hao wanajaribu kujipanga kwa kutumia makundi mengine muhimu ndani ya jamii kwa lengo la kuhakikisha wanafanikisha mkakati huo ambao unaonekana kuwa ushindani mkali kutokana na kipindi cha rais wa sasa Jakaya Kikwete kumalizika kwa mujibu wa katiba.

  Chanzo chetu kimedokeza kwamba moja ya maeneo yanayotupiwa macho na wagombea hao katika kuhakikisha wanafanikisha mkakati wao ni kufanya kila linalowezekana ili wakubalike na dini kuu mbili zenye mtandao mkubwa nchini, yaani Waislamu na Wakristo.

  Ili kufanikisha hilo wagombea hao wanadaiwa kujaribu kufanya kila linalowezekana kugusa hisia chanya za dini hizo kwa imani kwamba wanaweza kulamba tufuru kwenye kinyang'anganyiri hicho.

  Katika kile kinachoonesha kuthibitisha mkakati huo, mmoja wa wagombea wanaotajwa kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 anadaiwa kuchangia jumla ya sh. milioni 60 kufanikisha shughuli moja ya kidini inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

  "Tumeshangaa, ni kawaida Wakatoliki tunapokuwa na sherehe mbalimbali tunatoa kadi kwa waumini wetu na watu wengine kuchangia. Michango hii ni ya kawaida kwa kadri mtu alivyojaliwa, hatulaumu lakini inatia wasiwasi kigogo mmoja anatoa sh. milioni 60 kuchangia sherehe za kuwekwa wakfu Askofu wa Jimbo la Dodoma," kilisema chanzo chetu na kuongeza;

  "Michango ya namna hii inapoteza maana yake hata kama mtoaji alikuwa na nia njema. Si makosa watu wakisema huku ni kujaribu kujipendekeza kwa kanisa ili kuungwa mkono kwa madhumuni fulani. Milioni 60 ni fedha nyingi sana kutoa kama mchango tu kwa sherehe za namna hii, kwanini mtu huyu asitoe fedha hizo kwa waathirika wa mabomu Gongolamboto?"

  Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zilisema kuwa kigogo huyo alitoa fedha hizo kwa awamu mbili, kwanza alitoa milioni 45 na baadaye alimalizia sh. milioni 15, jambo ambalo limezua maswali mengi kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo.

  "Inawezekanaje mtu mmoja kuchangia fedha zote hizi kwa shughuli hii? Inawezekana hapa pana ajenda ya kisiasa nyuma yake, ni mbinu za 'kuvalisha kanisa miwani' ili aonekane."

  Majira lilipojaribu kuwasiliana na viongozi wa kanisa hilo kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu zao hazikupatika hewani na zingine ziliita pasi kupokelewa.

  Hata hivyo mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo aliyeomba kutotajwa jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa kanisa hilo alithibitisha kupokewa kwa fedha hizo na kukataa kuzungumzia zaidi suala hilo.

  Mwanakamati mwingine alidai kuwa mchango huo 'wakutisha' kwa sherehe za kawaida kama hizo, unaweza kuligawa kanisa hilo kwa kuonekana linageuzwa kuwa jukwaa la baadhi ya watu kutafuta njia za kukidhi matakwa yao kisiasa.

  Wakati huo huo hali si shwari ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa kile kinachodaiwa kuwepo taarifa za zengwe la kuwang'oa baadhi ya viongozi wake kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja huo unaoatarajiwa kufanyika Jumamosi mjini Dodoma.

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya wanasiasa wamejipenyeza ndani ya umoja huo kwa kuwatumia baadhi ya wajumbe kuhakikisha wanawang'oa viongozi wanaoonekana vikwazo katika kukidhi malengo yao.

  "Tupo macho, ingawa kuna taarifa kwamba baadhi ya watu wana mpango wa kuvuruga UVCCM kwa kuhakikisha viongozi ambao wamekuwa kikwazo katika kutekeleza malengo yao wanawekwa kando," alidokeza mmoja wa wajumbe wa baraza hilo.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbona huyo mtoaji hajatajwa tumjue?
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Membe?
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kumbe? Waislamu ameshawaahidi OIC na sasa anadhani anaweza kuwanunua Wakatoliki? Siasa za bongo bwana!
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM 2011 NA MAKAMBI YAKE YAFANANAYO KAMA MAFUTA TAA NA MAJI:

  Katika hii sehemu ndogo tu ya makundi mbalimbali ya CCM tulizonazo hapa nchini, huyo wairi unafikiri atakua ni wa kundi gani hasa hapa chini???

  1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

  Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Msuya, Samwel Malechela, Ole Sendeka, Salim Ahmed Salim, Mzee Kisumo, na wengine wachache.

  2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

  3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

  4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

  5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli) + Zitto Zuberi Kabwe + Mbunge Kafulia wa Chigoma ...

  6. CCM-Mwandosya / Mangula / Mwakyembe / Mwakyusa (Kanda ya Juu Kusini)

  7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks aka Mzee wa Chato (Kanda ya Ziwa)

  8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini) + Lipumba + Cheyo

  9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba) + Maalim Seif

  Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM ipi hasa.
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi kupata chema toka cc nahitaji kusaitiwa kuuondo mtazamo wangu wa "haiwezekani"
   
 20. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimeelezwa na mtu aliyeko Dodoma kuhusu suala la Mh. Membe kuchangia fedha kwenye sherehe hiyo. Mtoa taarifa hakuweza kunieleza kiasi kamili alichochanga Mh. Membe.

  Jambo hilo la kupata mchango kutoka kwa Mh. Membe limepenyezwa kwa kuwatumia baadhi ya viongozi wa Walei waliopo katika kamati ya maandalizi ya sherehe bila Msimamzi wa Jimbo hilo kufahamu. Kwa vile sasa wapo katika hatua za mwisho wa maandalizi ya sherehe hakuna namna tena kwani kamati ilifanya majukumu yake bila jambo hilo kufahamika mapema. Hata hivyo jambo hilo limeonekana kumchukiza aliyekuwa Msimamizi wa Jimbo ambaye ndiye huyo huyo anayekabidhi Jimbo kwa mwenzake
   
Loading...