DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,152
Shauri lililofunguliwa na Bodi ya Wadhamini la kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima linaendelea kusikilizwa leo Julai 14, 2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Bodi ya Wadhamini inaiomba Mahakama kutupilia mbali zuio la kanisa hilo kuendesha shughuli zake za kidini. Tangu shauri hilo lilivyofikishwa Mahakamani mbele ya Jaji Juliana Masabo kikwazo kikubwa kilichojitokeza ni barua husika ya kufuta usajili ambapo barua iliyowasilishwa Mahakamani kutoka kwa msajili ilikuwa na jina la Glory of Christ Church badala ya jina Glory of Christ Tanzania Church, jambo ambalo hata mawakili wa serikali waliita barua hiyo uzushi na haipo.
Soma Pia: Kesi ya Gwajima yaahirishwa mpaka Julai 14, 2025
Hata hivyo Wakili wa Kanisa hilo, Wakili Peter Kibatala aliweza kuwasilisha vielelezo vipya, na shauri hilo kupangiwa kusikilizwa Julai 11, 2025 na kuahirishwa hadi leo Julai 14, 2025 saa nane Mchana