Meli ya Kisasa Kuzinduliwa Karibuni na Kampuni ya Azam Marine

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1]
484472_470947526248722_551314_n.jpg
[/h]

Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20
Chanzo: Zanzinews
 
Hii labda itaenda Pemba tu ,huku Tanganyika itakuwa weshafunga mipaka na wamenuna.
 
Sasa hapa ndo swali la kuwa huyu mwenye kampuni ya Azam ana uwezo zaid ya serikali huwa linarudi akilini mwangu kila ninapojitahidi kuweka uwiano wa vitega uchumi vyake na rasilimali za nchi hii...........

Well let me let it go ...............ntapata wazimu bure !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sisi wa Ziwa Victoria (Bukoba-Mwanza) tunasubiri ahadi ya Mh. JK sijui ni lini itatekelezwa.
 
Jamani hii ni hatua ya kupongezwa ya Said Bakhressa.

Mimi ninashauri hiyo Meli ikaguliwe na kusajiliwa na SUMATRA maana hao ZMA wameshaingiliwa DUDUMIZI.

Lakini pia hii isiwe kichaka cha kutomuwajibisha huyo waziri Hamoud Massoud!
 
Sasa hapa ndo swali la kuwa huyu mwenye kampuni ya Azam ana uwezo zaid ya serikali huwa linarudi akilini mwangu kila ninapojitahidi kuweka uwiano wa vitega uchumi vyake na rasilimali za nchi hii...........

Well let me let it go ...............ntapata wazimu bure !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

kwa vyovyote vile ni kampuni yenye mafanikio makubwa inastahili kuwa case study elimu ya biashara. Nini siri ya mafanikio ya Azam wana MBA?
 
sisi wa Ziwa Victoria (Bukoba-Mwanza) tunasubiri ahadi ya Mh. JK sijui ni lini itatekelezwa.

Muangukieni Bakhressa! Baniani mbaya kiatu chake dawa.

Kama wewe una muani JK, the you will believe anything in this world.

Hata watu wa KIGOMA wanasubiri KIGOMA ifanywe kuwa Dubai ya Tanzania.
 
Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20
Chanzo: Zanzinews

Kauli ya waziri inatatanisha na ina harufu ya ufisadi. Kwani yeye ni msemaji wa kampunu ya Azam? Azam watoe huduma bila faida wamekuwa serikali? Kwa kauli kama hii mnategemea serikali itaifanyia ukaguzi meli hiyo kubaini kama inakidhi vigezo vya ubora kabla ya kuruhusu ianze kazi?

Imetengenezwa lini na wapi kabla ya kuletwa nchini?

Watatueleza itakapozama,
 
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Chanzo: Zanzinews
Kutokana na kichwa cha habari, ama habari imechelewa kutolewa au tarehe imekosewa kwani leo ni tarehe 22 Julai. Kwa mnaojua hili tukio, siku hiyo ya terehe 15 Julai ilizinduliwa?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Lakini pia hii isiwe kichaka cha kutomuwajibisha huyo waziri Hamoud Massoud!
Huyu awe Hamuod, Humud au Mahmoud, Hamadi, Hamad, Muhamadi.....Nilianza kumchukia baada ya ajali ya mwaka jana na ninmezidi kumchukia baada ya ajali ya mwaka huu.
 
Back
Top Bottom