Tatizo siyo waraka wa Waebrania, Tatizo ni uelewa wa waraka huo
Nyinyi mnautafsiri out of context kwa kuungaunga maana.
Ngoja Niquote Maandiko
SOURCE:
https://www.biblegateway.com/passage/?search=Waebrania+7&version=SNT
Yesu Na Melkizedeki (Waebrania 7:11-17)
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”
Ni dhahiri:
Kwa mujibu wa andiko hilo katika msitari wa mwisho nilioupigia msitari unaosema "
WEWE NI KUHANI MILELE KAMA MELKIZEDEKI" inaonysha kuwa YESU ni YESU na MELKIZEDEKI ni MELKIZEDEKI ila wote wana Ukuhani wa Milele!.
Neno "
Kama" limetumika kwenye hilo andika KULINGANISHA watu wawili, Nikisema Mtu X kama Mtu Y kwenye ishu Z maana yake siyo kwamba X ndiye Y bali hawa ni watu tofauti lakini wana role Z ambayo ni moja
KITU KIKISHAITWA "KAMA" MAANA YAKE KINAFANANISHWA (compared to) , KINAKUWA SIYO CHENYEWE HALISI!
Ni suala la lugha tu, Ukitaka kutumia logic yako kuungaunga visivyoungika basi bible unaweza kuitafsiri vyovyote unavyopenda na ikaleta justification zozote