Mei Mosi 2018: Rais Magufuli atapandisha Mishahara miradi mikubwa ya Serikali ikikamilika, Mwaka jana alinukuliwa Vibaya

Atawazidishia kula rushwa,hakuna namna nyengine na rushwa itawakoma maana hakuna namna yoyote itakayomfanya mfanyakazi wa sekta yoyote ktk nchi hii kutokupokea rushwa.

Shida zote anazo yeye,deni la mkopo wa elimu,deni la Vitz sijui Passo huko vijijini nako kuna wazazi wanamtegemea madogo nao wanategemea mkubwa awasomeshe na mshahara wenyewe ndo huo huo miaka rudi miaka nenda.

Poleni sana ndugu zangu ila mkipata fursa na nyie pigeni maana hakuna serikali itakuja chini ya ccm iseme imeboresha maslahi yenu never ever!!!
 
Mimi ni mtumishi wa umma, pato langu ni dogo lakini kwa maslahi mapana ya taifa hili naunga mkono hotuba ya rais Magufuli 100%. Ni ukweli usiopingika kuwa hata katika ngazi ya kaya mtu ukitaka kupiga hatua kimaendeleo lazima ufanye sacrifice kwa baadhi ya mambo ndani ya familia. Magufuli kaongea ukweli mchungu sana ambao wengi hatuupendi. Hata mimi napenda kuongezewa mshahara but i have to accept these.
Kama hutojali kwa kuanzia miradi aliyokuwa anasema ni mradi upi au kiwanda kimekua angalau sucsseful
Ajira ndo ameban
elimu ndo kabisa walimu siku hiz awaajiri
kingine ingia mtaani uone maisha yalivyo
Mara nyingine tuacheni unafiki jmn
Tumwogope Mungu
 
Mmemuona yule mtu asiyejulikana aliyemtolea Nape bastola? Huyu hapo kati.
66f767a2-9c94-4e25-aacd-896f4790f99e-jpeg.762666
 
Kama hutojali kwa kuanzia miradi aliyokuwa anasema ni mradi upi au kiwanda kimekua angalau sucsseful
Ajira ndo ameban
elimu ndo kabisa walimu siku hiz awaajiri
kingine ingia mtaani uone maisha yalivyo
Mara nyingine tuacheni unafiki jmn
Tumwogope Mungu
Mkuu, hali ni ngumu sana hata mimi sikatai hilo. Lkn baba ndani ya nyumba ndio kashasema kuwa hakuna kula wali na nyama hadi sikukuu, utafanya nini? Ni kuendelea kuosha vyombo na kuteka maji kwa moyo mkunjufu hadi baba atakapoamua au vinginevyo uiasi familia au utafute maisha binafsi ukajitegemee.

Lazima tukubali hali na tujipange namna ya kupata pato nje ya ajira. Kipindi hiki cha Magufuli wapo watu watafanikiwa kutoboa kwasababu wameamua kubadilika na kuangalia maisha mbadala nje ya ajira zao na wapo watu wataendelea kulia hadi siku Mwenyezi MUNGU atakapowachukua. Mkuu tubadili mindset zetu. Mimi nishaongea na wife tuanze kuuza "vitumbua", hamna namna.
 
Waache kazi kama pesa haitoshi, wajinga Sana watumishi hivi anajua wakulima na wafanyabiashara wanaoendesha nchi hii wanahali gani

Eti ehh

sasa hawa wakulima watamuuzia nani chakula kama wote tukiwa wakulima na wafugaji.

anyway mimi ki senti changu inabidi nikipangie bajeti ya kujinyima alafu tuone mtafanya nini?
 
Tukileta mandege mengi tutapata mahera tutapandisha mamishahara...Sitawaangusha maana nitapandisha kwerikweri...Subirini mandege yajae angani kwanza! Kupanga ni kuchagua.
Ili kusudi inflation ishuke..
 
halafu kuna mijitu mingine inakuja kupinga waraka!! https://jamii.app/JFUserGuide them!! angetoa hii hotunmba tar 24/4 tar 26 ningeandamana
 
Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa, nimekusikiliza na kukutazama. Binafsi, sikufanikiwa kuwa Iringa. Lakini, nilifuatilia na kusubiria neno lako jema kwa wafanyakazi-hasa watumishi wa umma. Nakubaliana nawe kuwa kupanga ni kuchagua. Nakubaliana nawe kuwa kwako wewe vipo vitu vya kuanza navyo na vingine kusubiri.

Lakini, amini nakwambia, watumishi wa umma ni kila kitu. Katika ulimwengu wa kisiasa na kiutawala, matumizi ya kwanza ya Serikali ni malipo ya mishahara na mengineyo ya watumishi wa umma. Zipo sababu za kuanza na hao. Zipo sababu za kuwapandishia mishahara. Nitataja chache bila hata kuzipanga.

Kwanza, watumishi wa umma ndiyo wasimamizi wa miradi ya Serikali. Kuanzia ndege, barabara, madaraja, elimu bure, mradi wa umeme wa maji, na reli itumiayo umeme vyote husimamiwa na watumishi wa umma. Watasimamia vyema wakiwa na amani, furaha na matumaini. Kila jambo la Serikali hunyooka wanaponyooka watumishi wa umma.

Watumishi wa umma wanapaswa kuanza. Vitu vinafuatia. Mishahara yao ni muhimu kuongezwa ili kuongeza morali na utendaji kazi. Ni kazi bure kuwa na miradi bila kuwa na wasimamizi wasio na furaha, amani na matumaini. Wanaoishi katika lindi la umaskini na tabu kubwa. Kutowapandishia mishahara yao ni kuwachoma hadi kuwapa homa.

Amini nakwambia Rais na Mwenyekiti wangu, watumishi wa umma ni uti wa mgongo wa mipango yote ya Serikali na mafanikio yake. Ni uti wa mgongo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na kadhalika. Hawawezi kuwekwa nyuma. Hawapaswi kuwekwa akiba na kusubiri. Wanapaswa kuanza. Wao ni kila kitu. Wakinuna, mambo yanabuma!

Mei Mosi, TUCTA imeshindwa vibaya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam


Wakimkwamisha si ndio gain kwenu sasa iweje ikuume tena?
 
Wakati wa kuongea lugha moja u karibu. Ni imani yangu hata wale wenye jukumu la 'kutoa kichapo cha mbwa koko' nao ni watumishi wa umma.

Na naamini pia mshahara wanaolipwa kwa sasa ni mkubwa tu sana, wanao uwezo wa kupanda bombadia
 
Top side down prioritisation plan, right vision, terribly wrong approach!
Workers in Tanzania can kiss salary hike good bye, kwa sababu hiyo miradi mikubwa mpaka ikamilike haijulikani ni lini na itauacha uchumi wa nchi katika hali gani! Ni miaka 18 au 48 ijayo?! Yajayo yanatia mashaka!
 
Back
Top Bottom