Meet singapore-based tanzanian it whizz kid alvin

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na mwanafunzi wa kidato cha pili huko Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya wataalamu wa application katika moja ya makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications ambazo anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia. Kwa idhini ya mama yake. Msikilize.

MEET SINGAPORE-BASED TANZANIAN IT WHIZZ KID ALVIN - YouTube
 

Attachments

  • IMG_2016.JPG
    IMG_2016.JPG
    39.7 KB · Views: 420
Ninampa hongera zake huyo kijana! Utaalamu wake autumie huko huko, vinginevyo akija hata nchini atafanyiwa mizengwe kama yule mtaalamu wa moyo ambaye ametangulia mbele ya haki hivi karibuni.
 
hofu yangu maccm wasije wakamrubuni arudi bongo ili wamuingize ktk kitengo cha watoa kucha na macho kwa koreo.
 
Bado mnajipa moyo kuwa huyo ni raia wa Tanzania? Wapo wanaojua umuhimu wa ubunifu tayari watakuwa wamempa uraia wa kudumu kwenye nchi zao.

Sisi mtu akitengeneza kitu cha kisanyansi zaidi kesho anapelekwa mahabusu kwa kutishia usalama wa nchi.
 
Mazingira yanasaidia sana kunoa vipaji,
Ninaamini kabisa huyu mchagga angekulia kwenye elimu ya Universal Primary Education (UPE) asingeweza kuwaza hata App inatengenezwaje.
 
Big Up mchaga Mwenzangu,,,,Komaa fursa unayo... Mimi wakati nina Umri kama wako nilikua Njuka kule Iringa (Tosamaganga) Akili inawaza Ulanzi 24/7.
 
Sijui kama watawala wetu wana orodha ya vichwa kama hivi vilivyo ughaibuni!
Samahani Mr,,,ujue nimemsikila dogo Youtube Na application anazotengeneza ni za kawaida sana na Nokia wanazitumia for free hawamlipi chochote,Na dream ya dogo ni kuwa programmer hapo baadaye.
Mtoto yeyote mwenye akili timamu ukimchukua ukamfundisha anachofanya Walter Makundi ni rahisi sana kujifunza na kuelewa
 
Mbona wapo wengi tu? unafikiri wazungu ni wajinga kuwapa zile scholarship za bure? vichwa havirusi huku vinang'ang'aniwa huko huko, wanaorudi ni wale mazumbukuku tu, waliofika huko wakaacha kusoma wakaingilia kubeba maboksi.

Na huyo mtoto hawamuachi, akija huku ni kutembea tu, sasa hivi watampa ma scholarship kibao. Mtanambia.
 
Back
Top Bottom