Kabla sijaanza kufanya meditation ingawa ninatumia Maombi; nilikuwa na wasiwasi, uoga kiasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, hasira, uzinifu na mengine mengi. Haya na mengine mengi kama chuki, usengenyaji, dharau, husuda, ugomvi, uchonganishi, wizi, wivu na zaidi kwa asilimia kubwa hufanywa pia na waumini watumiao MAOMBI.
Nilipoanza meditation nilianza kuwa na huruma, hakuna hasira, kuhisi jambo kabla halijatokea, kuota ndoto zinazokuwa kweli, kuwa jasiri (nilikuwa napita hadi maeneo ya hatari yenye wezi, vibaka, usiku mnene bila wasiwasi), hakuna kuuguaugua. Na mengine meeengi aisee.
Kiufupi, kwangu mimi kwa uzoefu nilioupitia japo sio mkubwa nimeona upo utofauti wa hali ya juu kati ya Maombi pekee na Meditation. Nilipoacha Meditation niliyumba hadi kiuchumi.
Kipindi nafanya sikuwa na tatizo la kiuchumi...nilikuwa nikiishiwa hela nikiconcetrate hata kama nipo ktk daladala siku haitaisha bila kupata ufumbuzi. Ila nilikuwa nikitumia Maombi na Meditation sio kimoja tu. Na sasa nimeanza tena.