Huwa iko hivyo na huja automatically practice utajionea mwenyeweNieleweshe hapa, kwa mfanya mediation huwez kuwa na tamaa ya hivyo vitu kivipi?
Nahitaji kujua kufanya hii kitu! Napata wapi mwalimu anicoach?Kabla sijaanza kufanya meditation ingawa ninatumia Maombi; nilikuwa na wasiwasi, uoga kiasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, hasira, uzinifu na mengine mengi. Haya na mengine mengi kama chuki, usengenyaji, dharau, husuda, ugomvi, uchonganishi, wizi, wivu na zaidi kwa asilimia kubwa hufanywa pia na waumini watumiao MAOMBI.
Nilipoanza meditation nilianza kuwa na huruma, hakuna hasira, kuhisi jambo kabla halijatokea, kuota ndoto zinazokuwa kweli, kuwa jasiri (nilikuwa napita hadi maeneo ya hatari yenye wezi, vibaka, usiku mnene bila wasiwasi), hakuna kuuguaugua. Na mengine meeengi aisee.
Kiufupi, kwangu mimi kwa uzoefu nilioupitia japo sio mkubwa nimeona upo utofauti wa hali ya juu kati ya Maombi pekee na Meditation. Nilipoacha Meditation niliyumba hadi kiuchumi.
Kipindi nafanya sikuwa na tatizo la kiuchumi...nilikuwa nikiishiwa hela nikiconcetrate hata kama nipo ktk daladala siku haitaisha bila kupata ufumbuzi. Ila nilikuwa nikitumia Maombi na Meditation sio kimoja tu. Na sasa nimeanza tena.
Kwa hapa, nimekukubali Mshana Jr, huo ndio ukweli hasa kuhusu meditation.Unaweza kushangazwa na andiko langu hili.... Lakini huu ndio uhalisia... Meditation sio kwa waamini katika Mungu mmoja mwenye mamlakan na mweza wa yote....!!!!!
Meditation ni kwa wale wasioamini katika miujiza ya kiimani kupitia supernatural powers.... Meditation ni kwa wahojaji wanaosimamia katika pure practice mpaka kuweza kumiliki nguvu za asili na kutenda miujiza... Meditation ni njia ya mwanadamu kutaka kuiga matendo ya Mungu ama kujionesha kuwa naye ana uwezo wa kuweza kutenda kama Mungu...
Ukiwa mwamini mwenye imani thabiti juu ya Mungu na mamlakan yake wala huhitaji kuhangaika na vitu kama meditation kwakuwa tayari umeshaambiwa katika Neno kuwa..... 'Ukiwa na imani hata ya ukubwa wa chembe ya haradari utakuwa na uwezo hata wa kuhamisha milima... Kwa meditation hata umalize stage zote hilo hutaliweza kamwe....!!!
Haradali.. ninini? (Arabidopsis thaliana)
Haradari ni mmea ambao ndio una mbegu/punje ndogo kuliko mimea yote... Lakini yenye uwezo mkubwa wa ajabu wa kupambana na hali zote na uwezo mkubwa wa kufyonza chakula
Kwahiyo kama mwamini hutakiwi kujitesa na mazoezi magumu ya meditation yenye masharti na miiko mingi na ya muda mrefu... Unachohitaji ni IMANI THABITI... imani kipimo cha punje ya HARADALI... ukiliweza hili utafanya yaliyofanywa na meditator guru wa viwango vya juu mno.,..
Kwanini sasa tunafundishana meditation?
Jibu ni rahisi sana.... Kwakuwa hatuna IMANI kipimo cha punje ya HARADALI.... Lakini vilevile si kila mmoja wetu hapa ni mwamini katika Mungu mmoja
Meditation pia ni nzuri kwa afya ya mwili na akili pia... Na kama wewe ni mwamini unaweza pia kutumia njia hii ndefu ya meditation kwa tafakuri za kimungu... Kwahiyo inategemea unaweza vipi wewe mwenyewe kujisimamia
Mimi ni meditator hivyo siipondi meditation... Lakini ukweli ni kwamba kwenye swala zima la
Kutafuta kweli
Kujitambua na elimu ya utambuzi
Self cultivation
Makutano ya kiroho, kiungu nk... Meditation ni sawa na kutembea kwa milonje huku imani ni sawa na kupanda gari.... Ama meditation ni sawa na kutumia njia ndefu wakati imani ikiwa ni kutumia shortcut
Bado niko sahihi ndio maana hawakuwaambia ishu ya meditation, between hiyo imani ni zile imani zenye ziada ndani yakeMshana Jr habari, kuna wakati fulani nilikua kwenye mafunzo ya dini kwa ngazi fulani katika kikundi fulani ndani ya kanisa.
Kitu cha kwanza tulicho ambiwa ambacho ni kama kanuni wakati wote unapokua kwenye hicho kikundi au nje ya, kama Mkristo baada ya sala za mwanzo kinacho fuata ni kukaa ukimya kwa muda usiopungua dakika 20.
Wakati tulipokua tunaanza tiliambiwatuanze kidogo kidogo mpaka uzoefu utakapo jengeka.
Tuliambiwa ni vigumu kidogo kukaa ukimya bila kuingiliwa na mawazo ila tuwe tuna concetrate kwenye Msalaba
Japo changoto zilikua nyingi lakini kipengele hicho kiniinua kiroho sana.
Nilipokuja kusikia na kusoma baadae sana hapa jf mambo ya meditation na faida zake ndio nikajua maana ya yale mafunzo.
Sasa mkuu unaposema meditation sio kwaajili ya waamini mkuu imenichanganya kidogo.
Inawezekanaje kukaa kimya kabisa dakika 20 bila kuingiliwa na mawazo au niwe natazama nini ili nifanikiwe?Bado niko sahihi ndio maana hawakuwaambia ishu ya meditation, between hiyo imani ni zile imani zenye ziada ndani yake