Meditation: Kufungua Chakra Ya Tano(Koo la Chakula) Rakims


Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
2,696
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
2,696 2,000
Habari,
Kwa Wale Wanaofahamu Kuhusu Mada Zangu Basi Hii Ni Random Inayoendelea Na Chakras
maxresdefault-jpg.416155

"Maajabu Ya Koo La Chakula Au Kidaka Tonge"

"Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno, Nae Neno Alikuwa Kwa Mungu Nae Neno Alikuwa Ni Mungu" John 1:1

"Na Alikuwa Na Nyota Saba Mkono Wake Wa Kulia, Na Nje Ya Mdomo Wake Kulikuwa Na Upanga Mbili Zilizokali"
Revelation 1:16


2:1 Msuguano Wa Koo

Hili Ni Zoezi Ambalo Pia Baadae Husaidia Kuamsha Jicho La Tatu, Chini Kidogo Ya Koo La Chakula Kwa Nyuma Mtetemeko Wake Unatokea Unapopumua Ndani Au Nje Hutokea.. Huunda Kiupepo Aina Ya Sauti.. Sauti Hiyo Yaweza Kuwa Humming Au Buzzing, Sauti Hiyo Yatakiwa Iwe Ile Ile, Wakati Wakuinhalling na exhalling.. Kama Utaweza Jaribu Kutumia Sauti Ndogo: Itakuwa Ni Rahisi Kukufanya Uweze Kufanya Kwa Muda Mrefu, Kabla Sijatoa Mbinu Za Kufanya Throat Friction... Ngoja Niwawekee Pointi Chache Ambazo Ni Sahihi Zaidi..

Usifanye Na Usianze Jitihada kwa Throat Friction Iliyo Kamili..
Fanya Tu Kiaina Iache Yenyewe Itajisogeza Na Muda..
Kama Ukijaribu Kuifanya Kikamilifu Na Kwa Jitihada Zaidi Basi Mwisho Wake Utakuwa Unakosea Kabisaa...
We Pumua Tu Nje Ndani Kwa Sauti Za Ajabu Ajabu Utaona Zenyewe Zinajipanga Sawiya..

Zifuatazo Ni Mbinu Za Kucheza Na Throat Friction Next Time Tutaunganisha Third Eye Na Throat Utaona Mambo Yanavyoenda Poa..

Ukitaka Uende Fasta Fasta Itabidi Utafute Chuo Pale Utakuta Vitabu Vya Kila Aina Vya Throat Friction Sounds Za Kila Aina Lakini Never Loose Hope Wakuu "Wherever Theres A Will Theres A Way"

Kule Waweza Kukuta Aina Nyingi Za Sauti Za Throat Friction Lakini Tambua, Sauti Yoyote Inafaa Kukuwezesha Kuamsha Jicho La Tatu..

Haijarishi Utapumulia Mdomo, Pua Au Vyote Kwa Wakati Mmoja.. Mdomo Tu Unatakiwa Uwe Wazi Kidogo Taya La Chini Liwe Limekosa Mtetemo Na Limetulia.. Ili Sasa Uweze Kupata Mtetemo Utakao Fikia Consciousness Yako..

Chukulia Mfano:
N - sehemu ya juu kwa nyuma ya koo la chakula,

F- Eneo La Mdomo Kwa Mbele

M- Eneo La Kati Hapa Kabla Hujafikia Matundu Ya Pua

L- Eneo La Nyuma La Koo ambapo msuguano hutokea


Msuguano Wa Koo Ni Sahihi Zaidi Ukitokea Eneo L Nyuma Ya Koo. Usitokee mbele Eneo La M, wala Eneo Karibu Na Mdomo Kwa Mbele F, 0&[HASHTAG]#8240[/HASHTAG];4kitoa Sauti Yako Kuitengeneza Kwa Eneo F Au M Basi sauti Itakuwa Kubwa Na Huwezi Kuivuta Kwa Ndani,
Sauti Inayotoka Kwenye Eneo L Ukifanya Hata Mara Ishirini, In Out In Out Utahisi Kama Kuna Mzigo Ulikuwa Nao Mwilini Umeutua...
Kosa lingine linaloweza Kutokea Ni Kutoa Sauti kutokea Eneo Eneo N Katika Hali Hiyo Ambayo Sio Ya Usahihi sauti Itatoka Kama Mtu Anaekoroma Kwa Kutumia Pua..
Kusibitisha Hili Tafuta Watu Wawili Ambao Wakilala Wana Koroma, Muangalie Anaekoromea Pua Akiamka Kachoka Hana Raha Hadi Baadae, Mcheki Jembe Aliekoromea Koo, Yupo Fiti Ndoto Alizoota Zimemfurahahisha Mwingine Yule Hana Jipya Za Kutisha tu.. kwa Anaekoroma Kwa Vyote Yeye Huwa Hakumbuki Kaota Nini,.. Asie Koroma Akiamka Yupo Kawaida Hana Makuu Na Anakumbuka Pointi Zote Alizoota Na Mwili Upo Vile Vile,

Pia Unapoendelea Kufanya Throat Friction Utajiskia Kimtetemo Kidogo Kwenye Kidaka Tonge Kinagusa Tufaha La Adam.. Tufaha La Adam Ni Ule Uvimbe Wa Wanaume Katikati Ya Shingo.. Ipo Sana Kwa Wanaume Zaidi Ya Wanawake.. Mwanzo Mtetemo Huonekana Kupatikana Zaidi Wakati uKivuta Pumzi Zaidi Kuliko Kutoa.. Hata kama Ni Sauti Ile Ile Inayotoka, Ni Ndani Kiasi Gani Hewa Inatakiwa Iwe? inatakiwa Kuwa Kawaida Tu.. Itakuwa Ngumu Kidogo Kwa Mara Ya Kwanza, Lengo Pia Ni Kuactivate Nguvu Ya Koo Kwa Kulisugua, Lengo Sio Kupumua Staili Gani, Lengo Ni Kuamsha Nguvu Ya Koo...

Faida Ya Throat Friction Ni Kureinforce Your Connection With The 'Energy', itakuwa Ni Ya Ajabu Ajabu Kwa Wanaoanza Mara Ya Kwanza Lakini Itakuwa Zaidi Na Zaidi Ya Maana Kama Utaendelea Kuiamsha Kwa Jicho La Tatu, Kadri Utakavyozidi Kuifanyia Mazoezi Ndio Itakavyozidi Kukufungua Uweze Kucontrol Power Inayokuzunguka Mwilini Kukulinda Wakati Wa Meditation,, Faida Nzuri Ni Kutembea Na Energy Zinazokuzunguka Sio Zinaenda Kulia Wewe Kushoto...
Zaidi Unavyozidi Kuvuta Pumzi Ndani Ndio Zaidi Power Za Throat Chakra Zinavyovujishwa, mdomo Umebaki Wazi Ni Muhimu Kuhakikisha Mdomo Upo Wazi Uwazi Ambao Unaweza Kupitisha Ulimi Katikati Ya Meno Ya Juu Na Chini... Na Muhimu Taya La Chini Liwe Limetulia Kuhakikisha Haliingilii Zoezi.. Maana Hapo Utahamia Chakra Ingine.. Vibration Itakapofika Kwenye Eneo La Jicho La Tatu, Ndio Ujaribu Kuanza Kupractise Huku Umefumba Mdomo,
Wanaoanza Mara Nyingi Huhisi Makoo Yanawakauka Au Yanakuwa Mabichi Zaidi, Waweza Kutumia Asali Kula Kila Siku Mara Mbili Itasaidia Tatizo Hilo Vijiko Vi3 Vya Chai.. Baadae Kila Kitofauti Kitapotea Na Utaanza Kuwa Mjuzi Zaidi.. Hii Pia Inakufanya Uwe Na Sauti Nzuri Sana Wakati Wa Maongezi Na Utaskia Watu Wanasema Jamaa Au Yule Sister Anasauti Ya Kipekee..

Swali:
Kwanini Uvimbe Wa Koo Unaitwa Tufaha La Adam?

Jibu:
Inasadikika Pindi Ilipofika Zamu Ya Adamu Kulishwa Tunda Na Hawa(Ever/Eva) Lilimkwama Kwa Muda Na Kutokea Hiyo Alama...


2.2 Faida Na Athari Za Msuguano Wa Koo..

Msuguano Wa Koo Ni Sauti Ya Nguvu..

Inakusaidia Kuelewa Wapi Uangalie Kwenye Third Eye..

Baadae Inaweza Kukupa Uwezo Wa Kuangalia Chakra Zote, Ndio Chakra Kubwa Ya Kwanza Kujifunza, Maana Itakujuza Kwa Mtetemo Wake Kwamba Hapa Kuna Crown Chakra Uangalie Vipi Hapa Kuna Third Eye Chakra Uangalie Vipi N.k

Itaanza Kujiweka Kama Kikisu Ikiwa Unataka Kungua Chakra Fulani Itafanya Kama Shoti Eneo La Chakra Hiyo Na Wewe Kuifikia Kirahisi,..

Pia Ina Maajabu Mengine Kibao Kama Inaweza Kuku Cure Na Magonjwa na Inatengua Sumu Mwilini..

Mara Zingine Hufanya Seli Hai Nyeupe Ziongezeke Na Kukufanya Uwe Fiti Muda Wote,

Pia Ina Tabia Ya Kurejesha Baby Skin Unaweza Kuonekana Kama Kijana Mbichi Wakati Ni Kabibi...

Ni Nyingi Naachia Hapo..

2.3 Maajabu Ya Koo

Ni Kubadili Sauti Katika Historia Kuna Historia Ya Wanasauti Anasemekana Alikuwa Na Psychic Powers MbaliMBALI, Ambapo Mmoja Kati Yao Aliitwa Vac- Siddhi (vac- voice) ambapo alikuwa akisema kitu kinatokea kweli,.. Ilifika kipindi wakavamiwa Na Wandugu Wa Kiume Wa 5 Wakataka Kwa Usalama Wao Wawaoze Yule Mwanasauti Mmoja Wakamuoza Na Kumwambia Kwa Uzuri Wa Sauti Yake Hamuwezi Kuishi Nae Milele, Wakamchukua Wakasema Harusi Itafanyika Kwao Wakishamwambia Mama Yao Wakafika Kwa Mama Yao Akawaambia Wote Mmempenda Binti Huyo Hivyo Mtamuoa Wote, Wakamuoa Akawa Mke Wa Mtu 5, Kila Akiulizwa Yule Wa Kike Umekubali Kuolewa Akisema Ndio Kwa Uzuri Wa Sauti Yake Ndugu Wale Wakagombana Na Kumkosa Wote..

The creative power of the voice was clearly expressed in Sanskrit, where vac, voice is often regarded as a synonym for sakti which is the creative Energy, the power of manifestation,

Kigiliki kuna Neno Linaitwa Logos, Mwanzo Wa tafsiri logo ni word, baadae Tunakuja Kuona mwanzo kulikuwako neno nae neno........??? John 2.1)

Na Pia Tukiangalia Katika Kitabu Cha Mwanzo Mungu Aliumba Ulimwengu Kwa Nguvu ya Neno Kuumba,

"Na Mungu Akasema, Pawe Na Mwanga, Na Pakawa Na Mwanga" genesis 1:3, 1:6, 1: 24 and so on..

Kumbe Kuna Nguvu Pia Katika Maneno Yetu, Hapa Ndipo Tunampata Yesu Pia Kwa Kusema Ikiwa Mnaimani Mwaweza Kuamuru Milima Ihame..

Kusema Hivyo Sikaribishi Walokole Hapa Nimetumia Tu Mfano....
Naomba Niachie Hapo

Jinsi Ya Kufanya:

2.4 Humming Sound And The Magic Of Bees..

Kaa Katika Mtindo Wa Meditation, Mgongo Wako Ukiwa Umenyooka Sawiya, Kuwa Muelewa Kati Ya Eneo La Spine Katika Shingo, Na Kunyoosha Mgongo Inatakiwa Wote Uwe Umenyooka,

Fumba Macho Yako..
Paelewe Kwenye Koo..
Anza Kutoa Sauti Ya Kukoroma, Ifanye Koo Yako Itetemeke, Ifanye Sauti Itoke Wakati Wa Kuingia Na Kutoka Kwa Hewa,..

Fanya Kuvuta Pumzi Kwa Ufupi Na Itoe Kwa Kireefu,
Endelea Kuielewa Mitetemo Inayotoka Kwenye Koromeo Kwa Kukoroma, Endelea Kufanya Zoezi Hili Kwa Dakika Kadhaa, Halafu Ukae Kimya Na Usijitingishe.. Sikilizia Koo Linavyoendelea Kutetemeka...

throat_chakra_vishuddha_puzzle-r07714630d3bf463ba37c6cde6fb4e13e_ambn9_8byvr_630-jpg.416156

To Be Continued....!

Takuja Kumalizia Halafu Tutaendelea Topic Ya Tatu,

AWAKENING THE THIRD EYE

Hiyo ilikuwa ni Awake The Throat Chakra, Tunakuja Third eye Tutaenda Crown

Rakims
 
GOLDGREEN9

GOLDGREEN9

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2016
Messages
353
Points
250
GOLDGREEN9

GOLDGREEN9

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2016
353 250
Aiseeee! hii chakra ukiizoea ni hatare , Minashauri wageni wa hizi mambo wafanye wakiwa alone kwa sababu watu watasema uchiz unakuingia.In short Balancing chakra ni kitu kingine cha kuzingatia ili kuepusha negative energies.
 
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
2,696
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
2,696 2,000
Aiseeee! hii chakra ukiizoea ni hatare , Minashauri wageni wa hizi mambo wafanye wakiwa alone kwa sababu watu watasema uchiz unakuingia.In short Balancing chakra ni kitu kingine cha kuzingatia ili kuepusha negative energies.
Yah, ni kweli maana wengine huona meditation ni stori tu za kale na wachina waliopinda zamani, lakini ni elimu pana sana yenye kumfanya mtu awe vile alivyoumbwa awe...

rakims
 
Alban makoa

Alban makoa

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2016
Messages
239
Points
250
Alban makoa

Alban makoa

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2016
239 250
Mkuu [HASHTAG]#rakims[/HASHTAG] mimi nimejalibu medition ya pumzi nmeshindwa na je nitaijuaje aura yangu.......au utanisaidiaje???
 
Mbulajee

Mbulajee

Member
Joined
Jun 2, 2017
Messages
74
Points
95
Mbulajee

Mbulajee

Member
Joined Jun 2, 2017
74 95
Aiseeee! hii chakra ukiizoea ni hatare , Minashauri wageni wa hizi mambo wafanye wakiwa alone kwa sababu watu watasema uchiz unakuingia.In short Balancing chakra ni kitu kingine cha kuzingatia ili kuepusha negative energies.
Balancing chakra ndio unafanyaje
 
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
2,696
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
2,696 2,000
Mkuu [HASHTAG]#rakims[/HASHTAG] mimi nimejalibu medition ya pumzi nmeshindwa na je nitaijuaje aura yangu.......au utanisaidiaje???
Ukiamka asubuhi sogeza mguu wa kulia kwenye mwanga wa dirisha utizame juu kidogo kwa muda utaiona aura yako, hiyo ndio rahisi zaidi

Rakims
 
I

islam23

New Member
Joined
Aug 23, 2018
Messages
2
Points
20
I

islam23

New Member
Joined Aug 23, 2018
2 20
Mkuu [HASHTAG]#rakims[/HASHTAG] mimi nimejalibu medition ya pumzi nmeshindwa na je nitaijuaje aura yangu.......au utanisaidiaje???
Kiuhalisia meditation nzur ni kutumia vitu vyenye kukustimulate brain kwa sabab itakupelekea kukutoa katika haya mazingira uliyoyazoea na kukupeleka katka ulimwengu mwengne kabisa .na kiukweli kama ni mtu unaependa sana dunia nakuhakikishia utaujuwa ukweli kwa nini sayansi imetufikisha hapa ? Maendeleo yako ila tambua ni mtego wako na ukishaiingia ni tabu kukwamuka this world is bullshit fanya meditation ujue ukweli uwe karibu na aliekuumba.
 
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
2,696
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
2,696 2,000
Kiuhalisia meditation nzur ni kutumia vitu vyenye kukustimulate brain kwa sabab itakupelekea kukutoa katika haya mazingira uliyoyazoea na kukupeleka katka ulimwengu mwengne kabisa .na kiukweli kama ni mtu unaependa sana dunia nakuhakikishia utaujuwa ukweli kwa nini sayansi imetufikisha hapa ? Maendeleo yako ila tambua ni mtego wako na ukishaiingia ni tabu kukwamuka this world is bullshit fanya meditation ujue ukweli uwe karibu na aliekuumba.
Together
 
Mtayarishaji

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
302
Points
250
Mtayarishaji

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
302 250
Mkuu, ulisema hapo juu kuwa uTakuja Kumalizia Halafu Tutaendelea na Topic Ya Tatu Ambayo Bila Shaka Ni AWAKENING THE THIRD EYE. Tuendelezee mkuu.
 
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
2,696
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
2,696 2,000
Mkuu, ulisema hapo juu kuwa uTakuja Kumalizia Halafu Tutaendelea na Topic Ya Tatu Ambayo Bila Shaka Ni AWAKENING THE THIRD EYE. Tuendelezee mkuu.
Nikipata nafasi naliendeleza mkuu
 
joely sandu

joely sandu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2017
Messages
1,476
Points
2,000
Age
22
joely sandu

joely sandu

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2017
1,476 2,000
Duuuuuuh
 
Mhandisi Mzalendo

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Messages
4,037
Points
2,000
Mhandisi Mzalendo

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2010
4,037 2,000
Vyoncept
 

Forum statistics

Threads 1,293,761
Members 497,728
Posts 31,152,646
Top