Medard Kalemani & Tito Mwinuka: Collaboration Iliyoongoza TANESCO kwa Mafanikio Makubwa

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,552
Ukweli usemwe:

Enzi za uongozi wa Medard Kalemani na Tito Mwinuka kukatika kwa umeme ilikuwa ni nadra sana, ma meneja wa TANESCO wa mikoa na wilaya walikuwa matumbo joto.

Kitengo cha emergency kilifanya kazi mchana kutwa, usiku kucha, huko vijijini speed ya kuwasha umeme kwenye miradi ya REA haikuwa ya kawaida.

Kila aliye ingia kwenye 18 za waziri Kalemani alikwenda na maji.

Mheshimiwa Rais warudishe hawa watu na uwape uhuru wapige show kabambe tule maisha.

Hivi vitu ndo vinatugusa moja kwamoja. Tunamkumbuka sana JPM huu ni ukweli mheshimiwa. Umeanza kutuchosha.
 
Hizi kampeni zingine hazina hata aibu
Mafanikio yapi?
Wateja kupata umeme miezi sita baada ya kulipia ndo mafanikio makubwa?...
Uongo mkubwa, umeme ulikuwa unaunganishiwa ndani ya wiki chache labda kama wewe mwombaji hauko serious. Tena vijijini 27k tu unakula maisha saafi. Sio huyu mama yenu anatulaza gizani siku 2 mfululizo.
 
Kalemani mpishi wa takwimu aliyesema serikali ya magufuli imepeleka umeme vijiji 13,000 wakat tanzania inavijiji 11,000
Kuna vijiji ambavyo vimehamishiwa manispaa ambavyo ramani ya TANESCO inasoma kuwa bado ni vijiji. Hata hivyo hajawahi kutoa hiyo kauli, kauli aliyotoa ni kuwa vijiji ambavyo JPM alikuta vikiwa na umeme ni2000, JPM akaongeza vijiji 6000 vikawa 8000 lengo ilikuwa kufukisha vijiji vyote kufikia 2022 pia kwa vijiji vya awali kulikuwa na mradi wa kuongeza coverage.
 
Kalemani alikua analeta mzaha sawa na yule wa cherehani nne ni kiwanda.

Kalemani anasema kijiji kikipitiwa na nguzo za umeme....hadi ule wa grid...anahesabu tayari kinao umeme alipobanwa na Kamati akasingizia kwa tafsiri ya tanesco kijiji kilichopitiwa na nguxo tayari kinaumeme ila wananchi hawajaingiziwa kwenye majumba...ndo akafikisha vijiji 13,000 vyenye umeme kutoka vijiji 2,000 alivyoacha mtangulizi wake.

Hafai
 
Kalemani mchezaji maarufu wa ngoma za fisi usukumani leo ndo useme anaimudu tanescoo??

Alifeli vibaya,
 
Sasa hivi REA wakandarasi wanapigia simu madiwani na viongozi wa vijiji wahamasishe maandamano ili waonekane waletewe transformer.

Toka December 2022 zinasubiriwa transformer huku mtandao wa nyaya na wiring tayari imefanyika.
 
Ukweli usemwe:
Enzi za uongozi wa Medard Kalemani na Tito Mwinuka kukatika kwa umeme ilikuwa ni nadra sana, ma meneja wa TANESCO wa mikoa na wilaya walikuwa matumbo joto.

Kitengo cha emergency kilifanya kazi mchana kutwa, usiku kucha, huko vijijini speed ya kuwasha umeme kwenye miradi ya REA haikuwa ya kawaida.

Kila aliye ingia kwenye 18 za waziri Kalemani alikwenda na maji.

Mheshimiwa Rais warudishe hawa watu na uwape uhuru wapige show kabambe tule maisha.

Hivi vitu ndo vinatugusa moja kwamoja. Tunamkumbuka sana JPM huu ni ukweli mheshimiwa. Umeanza kutuchosha.
Nchi yenye watu 60 milioni yani hakuna wakuongoza mpaka warudishwe walewale? Acha wapewe na wengine nafasi
 
Ukweli usemwe:

Enzi za uongozi wa Medard Kalemani na Tito Mwinuka kukatika kwa umeme ilikuwa ni nadra sana, ma meneja wa TANESCO wa mikoa na wilaya walikuwa matumbo joto.

Kitengo cha emergency kilifanya kazi mchana kutwa, usiku kucha, huko vijijini speed ya kuwasha umeme kwenye miradi ya REA haikuwa ya kawaida.

Kila aliye ingia kwenye 18 za waziri Kalemani alikwenda na maji.

Mheshimiwa Rais warudishe hawa watu na uwape uhuru wapige show kabambe tule maisha.

Hivi vitu ndo vinatugusa moja kwamoja. Tunamkumbuka sana JPM huu ni ukweli mheshimiwa. Umeanza kutuchosha.
Kitendo cha kufungua redio na kusikia matangazo ya kuuza magenereta na solar kuanzia asubuh mpaka jioni hii inaonyesha kwamba tatizo la umeme ni la kutengeneza tu ili watu wafanye biashara.
 
Medard he was a corrupt... Rejea issue ya viwatulifu ile kampuni iliyokuwa contracted
 
Uongo mkubwa, umeme ulikuwa unaunganishiwa ndani ya wiki chache labda kama wewe mwombaji hauko serious. Tena vijijini 27k tu unakula maisha saafi. Sio huyu mama yenu anatulaza gizani siku 2 mfululizo.
Huku umemsifia kalemani huku unamponda mama,

Edit ' japo na mimi hapa nilipo wameufyeka toka asubuhi matarajio ni mpaka jioni
 
Back
Top Bottom