Avatar
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 11,128
- 11,938
Unaandika kwa chuki kama mtu mwenye stress zake zilizo jaa kifuani unaedhani unaweza kupata auheni kwa kutukana mainjinia.Kwanza, ulichokisema hakinishawishi hata kidogo mkuu. Uwezo na ujuzi wako ni mtaji tosha kabisa. Show your ability/skills the world will support you. Sasa jitu linakaa ndani na kulalia mavyeti yake. haliwezi hata kuweka ujuzi wake into practice ila anapambna na theories tu ambazo hazina manufaa yoyote.
Pili, unaposema utayari wa serikali unamaanisha nini? kama wewe haupo tayari kuonesha ujuzi na uwezo wako kivipi serikali itakuwa tayari na wewe?
Tatu, Umesoma taaluma ya Uhandisi, Udaktari/Phamsia bado unataka uajiriwe? huo ni uoga wa maisha na uzwazwa na kutokuamini uwezo na ujuzi wako ulioupata huko mshuleni. Smart and intelligent people cannot be employed kwa sababu hawatakuwa huru kuonesha uwezo na ujuzi wao na ndiyo maana huwa wanataka wawe huru na siyo kutumikishwa.
Nne, sitaki uje na lame excuse kwamba mfumo wa elimu yetu mbaya. Kama mfumo mbaya ulienda shule ili iweje? ulienda kupoteza muda wako au? Maana ya mtu msomi ni kwamba ukishapata maarifa yatumie vyema kuisaidia jamii, rekebisha na kuyaweka sawa yale mambo ambayo hayko sawa.
Tano, ukiona msomi mwenye shahada ya uhandisi, Udaktari n.k analalamika kuhusu mfumo wa elimu tambua kwamba wewe bado ni mjinga wa kutupwa na ulienda shule kupoteza muda wako huko shuleni kusoma kitu ambacho hakikusaidii.
Ugua pole
Sent using Jamii Forums mobile app