Kwanza, sipo kwa ajili ya kukejeli taaluma ya mtu hapa bali kukumbushana tu kwamba hata kama uwezo wa kufanya mambo makubwa hawana kwa sababu ya mtaji n.k basi waoneshe ujuzi wao hata kwa kutengeneza vifaa ambavyo havihitaji mitaji mikubwa sana.
Pili, scope ya uzi huu ni wahandisi waliosoma nchini Tanzani tu. Wahandisi hao siyo competent, hawana soko hata kidogo. Kama wana uwezo kwanini msiuoneshe katika mambo madogo tu ambayo hayahitaji mtaji mkubwa?
Tatu, msomi ushindwe kutengeneza mazingira yako mwenyewe unasubiri serikali ndiyo ikutengeneze na ikupe ujuzi. Si ndiyo? we have to change our mind. Uwezo na ujuzi ni mtaji tosha kabisa. na ukionesha uwezo na ujuzi hakika Dunia itakusapoti.
Nne, Wahandisi wa U.S walianza kuonesha uwezo wao ndipo serikali ikaamua kuwawasapoti kutokana na jitihada zao.
Sasa utukejeli mara ngapi,threads nzima unawakejeli engineers.
Ila wewe si umesema Lawyer ni noble proffession,sasa Wanasheria na wahasibu ktk thread wamefuata nini? Au umesahau kama wewe ndio umewaingiza.
Nani kakwambia wanasayansi US wameanza kuonesha uwezo wao,alafu serikali ikawasupport hebu nipe mfano mmoja tu?
Wenzenu ulaya serikali yao imewawekea Lab kuanzia elimu ya awali mpaka chuo na bado final year project wanafunzi wanapewa hela ya kutosha na kama serikali wakiiona nzuri wanaisupport.Wana center kibao ya kitafiti za maswala ya kisayansi leo TBS kuna bidhaa nyingine wanazipima kwa macho sababu hawan maabara inayojitosheleza.Sasa ikiwa TBS yenyewe hali mbaya vipi huyo Engineers atakuwa na hali gani.Mack Zuckerburg,Bill gates,Steve Jobs tokea wadogo wanazijua Computer,huku TZ mtu Computer anaijulia chuo .
Najua unapayuka payuka siku tembelea kwenye final year presentation pale CoET au CoICT
wakiwa wanafanya projects zao zile za final years tena kwa gharama za mifuko yao ,lkn serikali yako haioni.Hizi mashine ndogo ndogo za kusaga nafaka na kukoboa Watoto wa Mechanical Engineer wamezitengeneza kibao,hizi mashine za kupukuchua mahindi zipo kubao pale CoET,serikali yako inashindwa hata kuzipromoti wahisani wazione.CoICT kuna systems kibao pale ambazo zinaweza kuwa solution kwa taasisi za kiserikali,tena zimefanyiwa tafiti ktk taasisi hizi za kiserikali lkn taasisi na serikali hawazioni,washazoea system ya kawaida wanainunua kwa bilion 1 huku nyingine washapiga,wakati wanafunzi ukiwapa milion 100 wanakutengenezea system uitakayo ww na wataisupport kwa gharama nafuu kuliko hiyo uliyoinunua toka nje.
Kuna madogo wa Computer science UDOM 2014 wamebuni system ya kusimamia kesi mahakamani,ili kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na kuondoa mfumo wa kuhifadhi taarifa kwenye mafile mahakamani,wameenda mpaka mahakamani kufanya research lkn mwisho wa siku si mahakama wala serikali yako haijathubutu kuwatafuta wale vijana kuboresha uendeshaji wa mahakama.
Sasa jiulize ikiwa watu historia wanashindwa kufanya research hizi kwenye makabila yetu 126 mila na tamaduni zao,machifu wao na zana walizokuwa wakitumia, je huyu mtu wa Science ndio ataweza.Watu wana idea kibao kuna dogo Mzanzibar kasoma UDOM anaitwa Salim kamaliza 2014 katengeneza Compiler kwa designed zake,lkn serikali yako imeshindwa kumwona.
Wewe siku ukipata muda zamia kwenye hizi fainal year presentation za Engineers CoET,CoICT,DIT,UDOM (Informatics and Virtual Educations) alafu angalia idea za wanafunzi wanavyo ziwasilisha practically,utakuja kugundua idea zipo ila tatizo serikali yako haioni wameng'ang'ania siasa..
Eti Lawyer noble professional,wanashindwa kufanya mambo yao msingi kwa ajili ya taifahili,wamejificha kwenye siasa,kutwa kudai katiba mpya na kulamba miguu ya wanasiasa.Mwisho wa siku wakapigwa Mlimani City kuanzia wanafunzi mpaka maprofesa wao hawajui walicho kisaini.
Hao wahasibu wako wenyewe mda si mrefu watu wa Computer Science,Software Engineering,Computer Engineering,Business Information system watazichukua kazi zao.