Matatizo mengi ya kiafya ikiwepo upungufu wa nguvu za kiume yanatokana na mtindo mbaya wa maisha.Mf.kutokuushughulisha mwili(Mazoezi),Lishe mbovu na hasa mazoea ya matumizi makubwa ya vitu vya sukari kuliko mboga mboga na matunda.
Kama mtu atabadili mtindo wake wa maisha,kunywa maji mengi safi ya kawaida si ya baridi kama hayo yanayoonekana hapo,kula mboga mboga,karanga(nuts),na vyakula vya asili,anaweza kurudisha uwezo wa mwili kutenda majukumu yake kama kawaida.
Hata hivyo pia inatokana na jinsi unavyoyatazama maisha.Watu wengi kwa sababu ya kusoma mambo ya kiwanga wanga wanakata tamaa na kudhani Mungu amependa wawe hivyo..Mtazamo wa mwandishi wa uzi huu ulikuwa kujigamba kuwa yeye yuko vizuri na japo hafuati kanuni zinazoaminika kurejesha afya za wengine,na hivyo wengine hata wakifuata kama wana matatizo basi hayawezi kuisha.Sisiti kuita mtazamo kama huu kuwa ni uchawi..