Mdude Chadema awaanika waliomteka

Mdude Chadema awaanika waliomteka

Huwa najiuliza sana hapa huwa mnafikiria nini? Kwamba askari mwenye mafunzo aache kituo aje kwako kusikiliza umbea? Au aache kuimarisha familia yake aje kusikiliza makelele yako ambayo anayapiga kwa ukijisikia tu!
Basi hao siyo polisi bali ni mabodigadi wako, na kama ulikuwa na akili hiyo bora ukakae mbali tu
Hizo ndizo akili za kiform 2 wanazosema. Yaani alitaka asikari akisikia kelele mitaani anatimuka tu kutoka ofisini kwenda kunako hizo kelele. Polisi hawafanyi kazi hivyo. Wakampime akili huyu!
 
..Mdude amefungua kesi dhidi ya IGP, AG, na askari watatu wa jeshi la Polisi.

..anawatumu kwa kuhusika na kumtesa na kumshikilia[ kumuweka rumande] kinyume na sheria.

..kesi hiyo imesajiliwa Mahakamani. Na askari anaowatuhumu amewataja kwa majina na force number zao.

Cc falcon mombasa
Kuwataja kwenye nyaraka/hati ya mashtaka (yaan "PLEADING") sio udhalikishaji/kumshushia mtu heshima) ila kumtaja kwny media ni kinyume chake.
 
Kuwataja kwenye nyaraka/hati ya mashtaka (yaan "PLEADING") sio udhalikishaji/kumshushia mtu heshima) ila kumtaja kwny media ni kinyume chake.

..Kweli.

..Na Mdude aliwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Haki za Binaadamu lakini tume wamekuwa wakimzunguza tu.

..Tusubiri kesi yake itakapotajwa. Natumaini atapata HAKI yake.

NB.

..Mdude amewahi kushtakiwa mara mbili kuhusu uchochezi. Na mara zote ameshinda kesi, na serekali imeshindwa ku-prove madai yake dhidi ya Mdude.
 
Huyo ni kama marehemu kambona na zitto walivyotuahidi kutaja watu wenye account tukajazana kwenye mkutano hakuna la maana walilolisema. Kijana wameshamuharibu bora Nondo aliwahi kuachiwa akiwa na akili zake huyu ni msukule tayari

Yeye ametekwa na wasiojulikana; sasa atawatajaje watu asiowajua?
 
Hiki kikosi cha ulinzi wa heshima ya rais kinachohangaika na akina Mdude ni hovyo sana. Hivi hawajui kuwa matendo yao yanasababisha madhara makubwa mara elfu kwa nchi yetu kuliko madhara yanayosababishwa na maneno ya akina Mdude? Very primitive! Nchi ya Nyerere sasa imekuwa kituko katika jumuia ya kimataifa! Hope kuna siku hawa watapata haki yao.
 
Naona huijui maana halisi ya ushujaa
Yaani huyu bwana mdogo anatukana viongozi hovyo ndio mnamuita shujaa?
Tumieni basi hata akili kidogo jamani

Kwa hiyo adhabu ya kutukana viongozi ni kutekwa na kuumizwa? Very primitive.
 
View attachment 1102777

Up Date
===
"Vyama vya siasa ama siasa ni kama ilivyokuwa dini, isipokuwa tunafofautiana tu katika itikadi lakini lengo letu ni moja tu kuhakikisha tunaleta maendeleo"

"Kwanza nilikuwa nawaza ni maaskofu gani wataweza kuvaa viatu vya Desmond Tutu aliyepata tuzo ya Nobel, sasa naanza kuona kumbe Tanzania wapo maaskofu hao."

"Kwanza natoa shukrani kwa viongozi wa dini waliofanya kazi ya kupiga kelele kubwa sana baada ya tukio langu kutokea."

"Kutoka ofisini kwangu hadi Kituo cha Polisi ni mita 300 na kutoka ofisini kwangu hadi kwenye makazi ya polisi ni mita 50 na wakati askari wanafanya gwaride nikiwa ofisini kwangu nawasikia na lengo la mimi kupiga kelele ilikuwa ni kutaka msaada"

"Wale watu hawakuwa na hoja walichokifanya mmoja wa wale watu akawaambia wenzake shika kwanza simu na begi lake hivyo ndivyo vitu vya muhimu, hapo ndipo nikaanza kuwatilia shaka"

"Mtekaji mmoja akajitambulisha kuwa yeye ni Polisi wamekuja kunichukua ili wakanihoji. Unajua mimi siku zote ni mdadisi na nikamhoji yule bwana, unanichukua kwa kosa gani, akasema wewe unatuhumiwa kwa kumtukana na Rais na Serikali huko mitandaoni"

"Mh. HecheJohn na godblesslema waliwahi kunifanyia mpango nikaishi Nairobi, kutokana na aina ya maisha ambayo naishi lakini nikakataa kwa sababu ninayofanya ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi"

"Tangu Rais ameingia madarakani mimi nimekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali na ndiyo maana nawaambia kutekwa kwangu ni kutokana na itikadi za kisiasa

"Katika Ofisi yangu nimetengeneza grili ili nikuhudumie ukiwa nje ya grili na nilifanya hivi ili polisi wakija kunikamata bila kufuata utaratibu wa kisheria nitoe taarifa na niripoti kwenye mitandao ya kijamii"

"Mimi sikupotea, nilitekwa na kutekwa kwangu kumetokana na masuala ya kisiasa kutokana na itikadi yangu"

"Sisi hatuamini katika kutekana, tunaamini katika kujenga hoja"

"Mmoja wa wale watekaji akanishikia bastola na mimi kwakuwa nilishaanza kuona harufu ya kifo nikasukuma ile bastola"

"Kitu cha kushangaza kelele zangu za kutaka msaada zikaishia kujaza watu na siyo askari"

"Nikiwa kwenye gari watekaji walinipiga kwa chupa za bia, wakawa wanasema unatuuliza maswali ya kijinga! unatuomba vitambulisho sisi"

"Nikiwa ndani ya ile gari nikawa naendelea kupambana, na ili kujua kama kulikuwa na gari mbili mmoja alimpigia simu dereva wa gari nyingine akimwambia kuwa hiyo gari inayotufuatilia iwekwe kati"

"Mmoja ya wale watu watatu akatoa silaha aina ya bastola halafu akaikoki na ikatoa mlio ili kuwatisha wananchi waliokuwa wanataka kunipa msaada ili waogope"

"Nilipigwa mpaka macho yakavimba na kichwa kikavimba kama mapapai ya Tukuyu maana kile kipigo cha Polisi sijui kinaingia mara ngapi kwa kipigo cha hawa jamaa"

"Wale watekaji wakasema sisi siyo wale wa mara ya kwanza waliokuchukua wakakutesa uchi na kukupeleka Oysterbay na tutakuonyesha sasa"

"Tunapozungumzia Uchumi hatuzungumzii barabara, hatuzungumzii Ndege, Mwalimu nyeree aliomba Uhuru ili sisi tuwe na uhuru wa kuhoji, uhuru wa kujitawala sisi wenyewe"

"Vitu vinavyothibitisha kuwa tukio langu la kutekwa ni la kisiasa, ni tweets zangu za mara ya mwisho kuhusu yule wakili aliyepotea, Ziara ya Rais Mbeya alipokuwa uyole na kuhusu ripoti ya IMF"

"Mimi nilikata tamaa ya kuendelea kuishi na nilishaomba sala ili Mungu aipokee roho yangu, mwacheni Mungu aitwe Mungu, Mungu ni fundi"

"Wasamalia wema walivyonipeleka kwa mwenyekiti wa kijiji, kitu cha kwanza niliomba maji, mwisho wa siku wakesema umekula nikasema nimekula jioni ya leo nikijua ni siku hiyo hiyo, wakasema wewe si umepotea toka juzi, wakaniandalia kwanza uji"

"Moja ya vitu ambavyo vinashangaza, sikuguswa maeneo mengine zaidi ya kupigwa kichwani, lakini cha kushangaza baada ya kupata fahamu nikakutwa nina majeraha mikononi na kwa mujibu wa wataalamu ni majeraha yaliyotokana na kufungwa pingu"

"Mpaka napoteza fahamu sikuwa na majeraha mgongoni lakini nilipofika hospitali nikakutwa nina vidonda mgongoni"

"Je mimi kuhoji tu pesa iliyotumika kutengeneza vitambulisho vya wajasiriamali imetoka wapi ndiyo natumika na Mabeberu kweli?"

"Kama siyo tukio la kisiasa kwanini wang'ang'anie begi langu ambalo lina nyaraka zangu nilizowashtaki Polisi, kwanini waniambie niwaite Umoja wa Mataifa waje wanisaidie, kwanini waniambie Mbowe aje anisaidie"

"Kama kuhoji kuhusu matumizi Serikalini ni kutumika na Mabeberu wacha nitumike"

"Mtu ambaye mimi kwangu ni mtuhumiwa namba moja kutokana na tukio langu la kutekwa ni RPC wa Songwe ambaye sasa kwa sasa amehamishwa, na huyu yupo kwenye orodha ya watu niliowashtaki"

Kuhusu kubadili msimamo wake Mdude amesema, "Kazi ya sikio haiwezi kuwa kazi ya pua, sikio litabaki kufanya kazi yake na pua itabaki kufanya kazi yake, siwezi kubadili msimamo wangu mimi ndivyo nilivyo"

"Mwizi huwa hajichunguzi, kama kweli wanalichukulia kwa uzito suala la kutekwa kwangu kwanini wasiite FBI waje kuchunguza mara moja?"
Pole sana kijana ila Acha kuzunguka sana.....

Advice.
Weka wazi tukio la kutekwa kwako but with Evidence siyo mambo ya kuhis maana kwenye Taaluma ya Sheria Mambo yakuhisi sijui fulan...... Nilimshitaki hivyo huenda alihusika na tukio langu la kutekwa, hicho kitu hakipo!!!!


Endelea kutoa Maneno ya Mafumbo wakushughulikie jumla...

Nchi hii inajitaj mtu uishi kwa misingi ya kisheria na siyo kuropoka ropoka hovyo without evidence eti uwe Maarufu.

Tulia jenga hoja na uliza swali sehem husika na siyo mtandaoni utaonekana una MAJUNGU MKUU hata kama swali lako linamaana kwa Maslai Mapana ya Taifa...

Serikali haifanyi kazi informal angalia hoja zako unaziwasilisha wapi?
Je Kwenye Social Media(Fb etc) au unaandika document yako na kuiwasilisha OFISI husika...

Mytake. Watanzania wenzangu tujifunze namna bora ya kufikisha ujumbe/hoja/swali kwa wahusika ili upate ufafanuzi..
 
Atazunguuuka weee ila kuwataja kwa majina hatoweza japo ndio kiu yetu kubwa.....naweza sema atatupotezea muda tu.wabongo hawana ujasiri huo
Atajuaje majina yao?

Na kama kweli atayajua, kutoyataja majina hayo itamsaidia vipi, asitekwe tena?

Nadhani ni sahihi kusema, hayajui majina. Huyu kwa jinsi alivyo, sio mtu wa kutotaja.
 
Unaonekana mtoto wewe . Mambo hayawagi rahisi hivyo. Labda kwa lugha kama za membe anaweza kupandikiza ujassusi wa namna hiyo . Ila sio logic yoyote hapo
Mshanza kuweweseka mara hii acha hawataje mnafikiri mdude Sawa na kina mo hyo kidume haswaa
 
Back
Top Bottom