KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,174
Ndio maana kuna watu walishauri angalau kwa sasa asirudi haraka. Afanye kazi hiyo mhimu kwanza akiwa huko huko aliko.Mumgu msaidie, lakni kwa hali tuliyonayo hapa kwetu, sijui kama yuko hai. kama international community haitaingilia, basi tutauawa wengi! Lisu nakupa mzigo huo uubebe. Huku nyumbani usije zunguka dunia ukiihimiza iingilie kati katika gross violation of human rights in Tanzania! Likifanikiwa hilo, basi nakuapia you are the next president!
Huo utakuwa mchango mkubwa zaidi ya ule ambao anaweza kuufanya akiwa katika mazingira magumu zaidi.
Zaidi ya kumtegemea yeye pekee, inabidi hivi vyama vyetu vya siasa vilivyopo - CHADEMA na ACT- Wazalendo waweke mkazo mkubwa sasa kushirikisha Jumuia ya Kimataifa kuiangalia kwa karibu zaidi hali yetu hii inayotukabili.
Mbinu za kupambana na watawala hawa kwa kudhani wananchi pekee ndio watakaoweza kuibadili bila ya msaada toka nje, inaonekana haitawezekana. Wananchi wanatiwa woga, hasa hivi vyombo vyetu vya kuwalinda wananchi vinapoamua kuwa sehemu ya kuwakandamiza.
Ndio, ni jukumu letu sote, wananchi raia wa nchi hii kujikomboa, lakini itabidi tuombe msaada wa kutuwezesha kujikomboa, vinginevyo haitawezekana.