Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Wana JF waliandaa Mchapalo (Cocktail Party) kwa ajili ya kusherehekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwake.
Hapakuwa na kadi za mwaliko bali kuna namba ulitakiwa utaje baada ya kutajiwa namba na mtunisha misuli Bwana figganigga aliyekuwa mlangoni…
Katika Mchapalo huo kulikuwa na Mdowezi mmoja aitwaye Bujibuji ambaye alitaka kuzamia lakini alijichomeka katikati ya mstari wa kuingia ili kusoma mchezo apate namna ya kuzamia.
Mtu wa Kwanza kufika mlangoni alikuwa ni snowhite.
Mtunisha misuli figganigga: Sabini na moja
snowhite: Kumi na mbili
Akaambiwa aingie
Mtu wa pili Bwana Asprin akafika mlangoni
Mtunisha misuli figganigga: Kumi na moja
Bwana Asprin: Kumi
Akaambiwa aingie
Mtu wa tatu Bwana Nyani Ngabu naye akafika mlangoni
Mtunisha misuli figganigga: Ishirini
Bwana Nyani Ngabu: Nane
Akaambiwa aingie
Mtu wa nne Dada AshaDii akafika mlangoni
Mtunisha misuli figganigga: Sitini
Dada AshaDii: Sita
Akaambiwa aingie
Mtu wa tano Bwana Bujibuji akafika mlangoni
Mtunisha misuli figganigga: Themanini
Bujibuji: Nne
Mtunisha misuli figganigga alimnyanyua Bwana Bujibuji na kumpa ngumi za chembe kabla ya kumsukumia mbali na kumwambia asije akaonekana kwenye eneo la tukio na apotee mara moja…..
Je Bujibuji alitakiwa ataje namba gani ili aingie kwenye Mchapalo?