Mdomo unaumba, jinenee mema

jamaikatz

Member
Jul 11, 2023
51
135
MDOMO UNAUMBA, JINENEE MEMA.

Miaka mitatu nyuma kulitokea kutokuelewana kati ya Jay Melody na Nandy ambapo Jay Melody alisikika akilalamika kuwa wakati Nandy hajawa msanii mkubwa Jay Melody ni miongoni mwa waandishi waliokuwa wanamuandikia Nandy nyimbo na kwenye zile nyimbo za Nandy za mwanzoni ambazo zilichangia pakubwa kumleta Nandy mjini na kumfungulia safari ya ustaa na umaarufu nyimbo hizo ziliandikwa na Jay Melody na walikuwa wanasaidiana tu wala hakukuwa na mambo ya kulipana kiivyo, lakini baada ya Nandy kuwa juu akawa mtu wa majivuno na kukataa kumpa sapoti Jay Melody.

Kwenye moja ya mahojiano yake Jay Melody alilalamika kwa kusema.

"Watu hawana shukrani kabisa ndugu yangu (Mwandishi) mimi wakati tunahaso pamoja na Nandy nilikiwa namsaidia kuandika nyimbo bure na hizo nyimbo ndizo zimemfanya afike hapa alipo leo kwasababu zilipokelewa vizuri mtaani zikamfungulia milango, lakini cha ajabu leo hii na mimi namuomba sapoti ili na mimi nitoke hataki, ananikwepa kwepa"

"Sina cha kumfanya maana siwezi kumwambia nirudishie nyimbo zangu ila hata mimi ipo siku Mungu atanijibu maombi yangu, kama alivyonipa kipaji atanipa na mahitaji mengine tutaheshimiana mtaani"- alisema Jay Melody

Baada ya maneno hayo haukupita muda mrefu, miaka miwili baadae kama sio mmoja na nusu, Jay Melody alikuja na wimbo wake wa (Nakupenda) ambao ulikuja na baraka zake, ukamtambulisha kitaifa na kimataifa, ukampa mafanikio makubwa ya ghafla, ukampa subscribers wengi YouTube na kwenye platforms nyingine, ukafanya hata nyimbo zake za zamani zisikilizwe zaidi, hadi leo ukiachilia mbali platforms nyingine kwenye YouTube pekee Jay Melody ana jumla ya viewers milioni 165 wakati Nandy akiwa na viewers milioni 200.

Hilo ni gepu dogo sana ukilinganisha na miaka miwili nyuma walivyokuwa wana utofauti mkubwa kwenye mauzo, ukimuamini Mungu, ukatia bidii kwenye kazi zako, ukaweka subra mambo yatajibu kwa wakati, hata wewe endelea kungoja usichoke, kesho utakuwa juu zaidi ya tajiri unayemuona leo.
 
Mdomo unaumba au Maneno huumba?.

Ngoja basi na mimi nikaongeze idadi ya wanaomsapoti Jay Melody. Kijana mwenzetu huyu na kiukweli ngoma zake ziko poa.
 
Kipindi Liwasa anagombea urais 2015 Kuna waziri wa kike alisema, Lowasa atakufa kwasababu Ni mgonjwa, haikupita muda kabla hata uchaguzi wenyewe, yule mama akaumwa, akapelekwa India, akafa.
Mtikila naye alimkejeli Lowasa kwa kumuita marehemu, tunajua yaliyomkuta, alipata ajali akafa akazikwa.
Tuweke akiba ya maneno hakuna ajuae kesho.
 
Kipindi Liwasa anagombea urais 2015 Kuna waziri wa kike alisema, Lowasa atakufa kwasababu Ni mgonjwa, haikupita muda kabla hata uchaguzi wenyewe, yule mama akaumwa, akapelekwa India, akafa.
Mtikila naye alimkejeli Lowasa kwa kumuita marehemu, tunajua yaliyomkuta, alipata ajali akafa akazikwa.
Tuweke akiba ya maneno hakuna ajuae kesho.
Kweli kabisa mkuu
 
NGOJA NIJINENEE MEMA

MIAKA MITANO IJAYO NITAKUWA TAJIRI, MLIONIDHARAU MTANISALIMIA KWA HESHIMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom