Mdomo uliponza

Mdomo uliponza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,638
Reaction score
220,410
Richard Mwenye asili ya Kusadika, alizaliwa wakati mama yake ana miaka 40+, wakati huo mama alikuwa na ajira katika mmoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa, New York. Baada ya kustaafu mama aliamua kusettle huko Marekani.

Richard alitamani sana kujua mila za Kusadika, akiwa kijana wa miaka 27 alifunga safari kwenda Kusadikia kwa mara ya kwanza. Alikutana na binamu zake waliompokea vizuri. Walianza kumuonyesha viwanja. Katika kuzunguka Richard alikutana na binti mrembo anaitwa Leah.

Richard na Leah walinza kudate, Richard alimpenda sana Leah, alianza hata kufiria lini atampeleka Marekani mama yake akamuone, mwenyewe alishajiona amepata mke. Leah alikuwa anabeep tu, hakuwa amefika kivile, na ile American English anayotema Richard, ilikuwa inamzengua tu. Alikuwa na jamaa yake pembeni basi na alikuwa anamwambia ngoja huyu mmarekani aondoke bwana.

Binamu zake Richard walipata habari ya ndugu yao kusalitiwa, iliwauma sana, tena Leah alijisifu hukoo, ah mimi naenjoy pesa yake tu. Mugabe alisema "hakuna kinachomzengua mwanamke kama kuwa na jamaa alosto mwenye ufundi kunako kitanda".

Richard alipopata issue nzima alimpigia simu Leah akamwambia mimi karibia ninaondoka sasa ninataka tumalize hii wiki pamoja, nikupeleke shopping, twende viwanja, tuienjoy manake. Leah alikubali, alipelekwa shopping, Richard akisisitiza anapenda kumwona amevaa nguo nyeupe wakienda club. Leah alichagua mini dress nyeupe, kiatu handbag, perfume, mambo ya fashion fair n.k

Kabla hawajaenda club Richard alinunua drink alifanikiwa kuweka laxido kwenye kile kinywaji, kutoka hapo walikula baadae wakaenda viwanja. Wakati wako kule Leah alisikia tumbo limebadilika, aliharisha mpaka gauni lake lenye rangi nyeupe lilionja kidogo. Richard alimwambia Leah nilikupenda sana, nilikupa heshima yote, kama hukunipenda ni kheri ungeniambia, ulijisifu kwa wenzako unaenjoy pesa yangu tu huna mpango na mimi, sasa nenda kawaambie wenzako umeharisha pesa yangu.
 
Ha ha ha ha ha ha , kweli kaharisha pesa.
 
Duh nishapata dawa ya wachunaji....

Jamani madhara ya kuharisha yanaweza kuwa makubwa kwenye mwili wa binadamu. Kuharisha kunasabisha mtu anapoteza electrolytes kwa haraka sana. Mwili ukikosa electrolytes unaweza kusababisha kifo cha ghafla, kidney failure au brain damage. Za kuambiwa changanya na zako.
 
Jamani madhara ya kuharisha yanaweza kuwa makubwa kwenye mwili wa binadamu. Kuharisha kunasabisha mtu anapoteza electrolytes kwa haraka sana. Mwili ukikosa electrolytes unaweza kusababisha kifo cha ghafla au brain damage. Za kuambiwa changanya na zako.
Nitahahikisha anaharisha kisawasawa ila hawezi kufa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom