Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,638
- 220,409
Huyu shost aliolewa na boyfriend wake wa tangu chuo. Huyu mwanaume alimpenda sana shost. Ni kaka mmoja mwenye sura ya kiume kiukweli lakini ana akili na busara sana. Tangu chuo walikuwa kama mapacha na walisaidiana na shost kwa hali na mali.
Shemeji ni mtoto wa kwanza. Ana madada wanne waliomfuata na wa mwisho ni wa kiume. Baada ya kuanza kazi alitoa posa na kumuoa rafiki yangu. Wote wakiwa waajiriwa maisha hayakuwa mabaya.
Sasa bwana katika maongezi ya mume na mke, mume wake alimhadithia mama yake alivyokuwa mtaalamu wa kwenda kwa waganga. Kuna siku alirudi na mayai ya njiwa kabla hajayafanyia utaratibu alioagizwa na mganga dingi yao akayaona. Basi walicheka yakaisha.
Dunia ni ndogo sana, mmoja wa ma classmates wetu alimchumbia dada wa mume wa shost. Basi shost alimhadithia mchumba mmh jina lako litakuwa kwa babu sasa hivi maana mama anatamani sana mabinti zake waolewe.
Mchumba aliyarudisha kama yalivyo kwa wifi. Wifi alimpelekea mama yake. Walijikusanya madada wote wanne na Mama yao wakamuita shost. Amefika kisuto kilimuangukia. Alilia sana. Kumbe wakati suluba ile unaendelea shemeji yake kitinda mimba aliyasikia na kumuita kaka yake.
Alipofika mumewe alivunja kikao akamchukua mke wake na kuwaambia hiyo mada imekwisha isikae irudiwe. Shost kunihadithia anamshukuru mume wake. Hana hamu na classmate kabisa.