Mdogo wangu kanisaliti

ulisikia vicheko au miguno?....nafsi ilisita au ulitonywa tu?....si ndiye aliyekubali "kuishi kwa kuvumiliana" mmmh kashindwa kuvumilia humfikishi ndo maana kaamua kutafuta mikuyati.....anayekusaliti si rafiki, je ni nani?...jibu unalo
 

Mimba usitoe ila kuhusu kukaa nae au ww ndi muamuzi,sijui kuhusu viapo vya kikristu lakini kama kosa si tayari limeshaonekana na ushahidi unao. so kama unataka kumuacha muache sasa na kama umeamua kuwa nae jaribu kusahau kila kitu na msonge mbele
 
Dah yani kama nakuona vile jinsi unavyoumia. Pole sana mkuu, ila mkeo hajafanya vizuri na kama alidiriki kutembea na ndugu yako, ni wazi alikua au atatembea na ambao sio ndugu zako. Inauma sana
 
i wish ungekuwa kakaangu nikutafunie yule mke wako tena ningefanya makusudi unifumanie naye manina

Stress nlizonazo ningefurahi mke wangu akiliwa Na dam yangu, kuliko kukipeleka kwa mijamaa huko buguruni, lol
 
Du pole sana jamaa yetu
ushauri mkuu ni KUMFUKUZIA MBALI maana hiyo kitu huwezi sahau maishani
km mna Watoto baki nao ila huyo wa mdogo wako watajuana hukohuko
 
Kumbukumbu la torati linasema amelaaniwa aufunuaye uchi wa mke wa kaka yake maana ni kama ameufunua uchi wa kaka yake. Na kumbuka kisasi ni juu ya BWANA. Mkeo na kaka yako wameshapokea hukumu yao. Wewe angalia kama una upendo wa kutosha KUSAMEHE na KUSAHAU samehe uendelee na ndoa yako. Kama huna toa talaka. Ukristo wako haukuzuii kutoa talaka kwenye sakarambe kama hili. Maelekezo ya KRISTO katika hili yako wazi maana hakuongea kwa lugha ya picha.
 
Duh mkuu suala lako ni zito ila inafaa kuwashirikisha wazee wa dini kwanza......
 
Mimi sikubaliani na watu wanaosema tusamehe na ndio maana matatizo hayaishi kila siku. Kwa hili nasema Nooo...... bora niishi mwenyewe ila aondoke ndio Amani yangu.
 
Nyie mnafukuzwaga na nani?
Ni uzinzi akifanya mwanamke akifanya mwanaume ni ulinzi enh?
Kwendeeeeni zenu!
Mpeni ushauri mnaowapa wakinadada wakija na kesi za aina hii hapa jamvini!
 
Mbona wanawake karibia wote wanafanana sema tu wanajikuta ktk fursa tofauti..
 
Kaka mtoa mada kwanza pole kwa yaliokukuta....mimi nilimfumania mume wangu na secretary nilisamehe but sitosahau..

Back to topic.... najua uko katika kipindi ma maamuzi magumu sana ila ninachokushauri usimfukuze huyo mwanamke ishi nae na kama huwezi kuishi nae chumba kimoja basi tenganeni vyumba.
Mpka pale atakapojifungua ndani ya miezi tisa utapata maamuzi ya nafsi yako inasemaje kumuacha kabisa au la.
 
Nyie mnafukuzwaga na nani?
Ni uzinzi akifanya mwanamke akifanya mwanaume ni ulinzi enh?
Kwendeeeeni zenu!
Mpeni ushauri mnaowapa wakinadada wakija na kesi za aina hii hapa jamvini!

Tena na wao wanazaa mitoto nje kibaoo wamaficha siku ukija kujua wanapiga magoti tunawasamehe
Sasa sijuhi hao watoto wanapatikana kwa njia gani ?kama sio kwa usaliti
 

Samahani mtoa mada, hivi hapa aliyekusaliti ni mdogo wako au mkeo? Mana sidhani kama huyo mdogo wako mliweka makubaliano yeyote(kiapo) but mkeo ndo unakiapo nae. So mi nahisi aliyekusaliti ni mkeo si mdogo wako.
 

mbona kama hadhithi hii, hivi in reality kweli yatokee hayo yaishe kirahisi rahisi hivyo? mmh
 
Pole sana mkuu kwahiyo mpk sasa mnalala room moja? kama ni hivyo huyo mwanamke ana moyo wa plastic ningekimbia!nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…