Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Is he right?

Dah,mm graduation ya mwisho kuhudhuria Ni ya form 6,na Ni ya sababu ilikuwa boarding sikuwa na pa kukimbilia,halafu graduation za sekondqri huwaga kabla ya kumaliza mtihani, kuanzia degree,masters Wala professional board sijawah kufanya graduation,Sasa hoja za waty wanasemaga huna picha ya joho?? Nawaambiaga kwani elimu hupimwa kwenye joho??mahafal za vyuo hazijawahi kuniimpress kabisaa sijui kwa sababu hufanyika siku nyingi Sana mbele bqada ya kumaliza masomo??

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
Upo kama mdogo wangu, yaaani hana interests kabisa na visherehe sherehe
 
Habari za muda huu watanzania wa humu JamiiForums.

Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Was he right?

View attachment 1724376

Mwaka wa 2017 nilipata fursa ya kuhudhuria mahafali ya wahitimu wa elimu ya juu pale chuo cha ******** kipo huku Dar. Mimi kama mgeni mualikwa nilienda kuwavisha taji watoto wa mama yangu mdogo na mkubwa (mmoja wa kike na mwingine wa kiume).

Hawa madogo mmoja alisomea Accountancy na mwingine kama sijakosea alisomea masuala ya Ualimu hivi. Sasa siku ile ya maafali nilikuwa niende kwenye mishe zangu Kigamboni ila nikasema ngoja nikawavishe mataji hawa majamaa isije baade wakasema kaka hajui kushirikiana vema na ndugu zake.

Basi muda ulipofika mimi huuyoooo nduki mpaka chuoni kwao nikakuta watu weeengi wakiwa ndugu, jamaa na marafiki wamekuja kwa ajili ya kufurahi na ndugu zao. Ngoja nifupishe story isiwe ndefu saaaaana.

Nilifanikiwa kumvisha taji ndugu yangu mmoja huyu wa kike na kufurahi naye. Tulifurahi sana kunywa na kula ila yule mwingine baada ya kumuuliza kwanini hakuja katika sherehe hizi kuna jibu alinipa.

View attachment 1724390

Jibu alilonipa ni kwamba, "hawezi kuhudhuria "Graduation Ceremony" kwa maana GPA yake ni kubwa mno na kamwe picha za kwenye graduation haziwezi kuambatanishwa katika barua ya maombi ya kazi. Wahitimu wengi wanaopapatikia sherehe za mahafali ni wale wenye GPA za chini".

Je, huyu dogo yupo sahihi au yeye ndio wale watu wanaoitwa "anti-social" (wasiopenda kuchangamana na wenzao)?

Maoni ya wadau
=====

=====

=====

=====

=====

=====

=====
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mimi sikuhudhuria
 
Mwambie mdogo wako aache uongo na uzandiki.... Asitake kupotosha jamii.. Kwa Hiyo hata wale Maprofesa na ma Dr wanaohudhuria mahafali za wanafunzi wao nao wana GPA ndogo?


Mdogo wako ni mjinga tu kama wajinga wengine....
Mbona unamtukana tena mkuu?
 
Kweli kabisa, mm huwa naona ni kupotezeana muda, niliyohudhuria ni ya form4 tu... form 6 niliamua kutoka mapema kwenda kulala, first degree na MSc sikuibuka kabisa licha ya kwamba zote GPA top 3 ya class yangu haikukosekana... na hata jamaa zangu kama 3 hivi tuliokuwa vizuri class hawakuibuka
Sawa...
 
Tulio ishia memkwa wanatukosoa hatari, kazi tunayo hadi mtu kucomment unaogopa, mtu baada ya kuchangia mada anaanza nae, kuanzisha Uzi wake kwenye Uzi wako, jamani maisha atufanani kama wewe, ulibahatika kuzijua, Nomino Na vivumishi, Ni wewe Na maisha yako, ko tushindwe kupost kisa, Nomino atuzijui? Wewe changia tu kama umeelewa sio kukosoa mwandiko, utazani yupo kwenye imla
Huyo jamaa hapo juu bado ni mjinga sana kwa maana hata mimi mwenyewe nimemshangaa sana
 
Back
Top Bottom