Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Is he right?

Habari za muda huu watanzania wa humu JamiiForums.

Mdogo wangu aliwahi kuniambia, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu wanaohudhuria "Graduation Ceremony" ni wale wenye GPA za chini. Was he right?

View attachment 1724376

Mwaka wa 2017 nilipata fursa ya kuhudhuria mahafali ya wahitimu wa elimu ya juu pale chuo cha ******** kipo huku Dar. Mimi kama mgeni mualikwa nilienda kuwavisha taji watoto wa mama yangu mdogo na mkubwa (mmoja wa kike na mwingine wa kiume).

Hawa madogo mmoja alisomea Accountancy na mwingine kama sijakosea alisomea masuala ya Ualimu hivi. Sasa siku ile ya maafali nilikuwa niende kwenye mishe zangu Kigamboni ila nikasema ngoja nikawavishe mataji hawa majamaa isije baade wakasema kaka hajui kushirikiana vema na ndugu zake.

Basi muda ulipofika mimi huuyoooo nduki mpaka chuoni kwao nikakuta watu weeengi wakiwa ndugu, jamaa na marafiki wamekuja kwa ajili ya kufurahi na ndugu zao. Ngoja nifupishe story isiwe ndefu saaaaana.

Nilifanikiwa kumvisha taji ndugu yangu mmoja huyu wa kike na kufurahi naye. Tulifurahi sana kunywa na kula ila yule mwingine baada ya kumuuliza kwanini hakuja katika sherehe hizi kuna jibu alinipa.

View attachment 1724390

Jibu alilonipa ni kwamba, "hawezi kuhudhuria "Graduation Ceremony" kwa maana GPA yake ni kubwa mno na kamwe picha za kwenye graduation haziwezi kuambatanishwa katika barua ya maombi ya kazi. Wahitimu wengi wanaopapatikia sherehe za mahafali ni wale wenye GPA za chini".

Je, huyu dogo yupo sahihi au yeye ndio wale watu wanaoitwa "anti-social" (wasiopenda kuchangamana na wenzao)?

Maoni ya wadau
=====

=====

=====

=====

=====

=====

=====
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Nimefanikiwa kuhudhulia graduation moja tu ya NBAA (CPA(T))na Yenyewe kwa sababu nilikuwa miongoni mwa wanaopewa zawadi sikujua kwenye graduation ntapewa tu mkono,pesa siku inayofuata,nilikasirika sana maana undergraduate na post graduates sijawahi kuudhulia hizi mishe niliona kupoteza gemu za weekend EPL ni hasara kubwa .
 
Mimi zote kasoro moja(mkuu wa shule alisema hamna hela-so tulivyomaliza tu mtihani,kila mtu akapita na sanduku lake)---kwanini nisifurahie na kuagana na wenzangu?
Hizi moments hazijirudii---kujipongeza,na kupongezwa ni sehemu ya hio safari.
 
kuna ambazo nimeudhuria na ambazo sijahudhuria kwa sababu mbali mbali.
sherehe ni hobby,shule tunaambiwa hatuendi kusoma tu vitabu na mapokeo pia ni sehemu ya kusoma tabia mienendo fursa mbinu na mikakati ya kupambana na maisha huku mtaani ambapo tunatarajia mhusika atakaa muda mrefu kuliko hapo chuoni.
lakini pia kuhudhuria ni hiyari,hivyo hata kutohudhuria ni hiyari ...
inawezekana mwenye gpa 5.0 akahudhuria ila mwenye 2.5 asiende pia...
kinachowafanya watu washiriki tukio sio tu linamuhusu bali kuwe na kitu cha ziada kinachomvutia kwenye hilo tukio,mfano harusi na misiba siyo yote tunashiriki japo wote wameoana au kufariki la ziada ndio linaamua ambapo kwa mfano huo kitu cha ziada ni ukaribu na marehemu au mwanandoa,kipato,umbali,muda na mahali,mitazamo binafsi nk
kuna wanaokwenda kujipongeza kufikia hatua fulani (juhudi binafsi au kusaidiwa na wengine ambao atawapa asante)na kuna wengine wanakwenda kushuhudia walio wasaidia na wakasaidika (kuna watu wanapenda kuona watu walio chini wanapanda juu/wanafurahia mafanikio ya wengine).
 
mimi nilisoma chuo sijui maana ya GpA... nachoepuka supp na kusoma vitu na kuvielewa kuvihusihs na life mtaani...maana nilitoka kitaa job kama miaka mitano ndio nikazama chuo..nilikuwa naijua supp tu unawahi kufungua chuo..kusomea gpa hapana...
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Sawa mkuu. Dogo alikuwa anaamini wenye GPA kubwa hawanaga papara na sherehe sherehe.
Ni kweli kabisa mkuu...Mimi mwenyewe nakumbuka siku ya graduation nilikuwa zangu buguruni nauza machungwa...nilisahau kabisa kama kulikuwa na gradu japokuwa nilibomoa GPA ya rekodi
 
Mimi nina rekodi ya kutoshiriki mahafali yangu mara 4. Darasa la saba sikushiriki,
Kidato cha nne sikushiriki, kidato cha sita sikushiriki na Elimu ya juu pia
 
Back
Top Bottom