Mdee,Mnyika,Slaa,Lema ndani uwanja sahara-mabibo leo

Mdee,Mnyika,Slaa,Lema ndani uwanja sahara-mabibo leo

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
956
Reaction score
120
Filimbi imelia ccm leo inazikwa rasmi viwanja vya sahara mabibo kuanzia saa 9 mchana.
UPDATE
Watu wameanza kumiminika uwanjan natumia nokia E63 nifundishen namna ya kuapload picha.
UPDATE
Mkutano umeanza nawaona viongozi wa jimbo na mbunge mnyika na Henri kilewo wakina mdee,slaa na wengine bado hawajafika natafuta taarifa kamili kwann hawajafika.
Mnyika amevaa baraghashia
Henri kilewo anaongea sasa jukwaan anaongea juu yaliyojiri kukamatwa kwake.
Alihojiwa na makamanda sita wa polisi aliulizwa ni viongoz gani walikuwepo kwenye uchaguz wa igunga akawataja mkapa na magufuli polisi wakakataa kumsikiliza wakamjibu si hao tunataka utaje viongoz wa cdm sio wa ccm. Difenda 4 zilimpeleka uwanja wa ndege kwa siri interpol wakawakatalia polis wa tz kumsafirisha kilewo akiwa na pingu pamoja na bastola zao wakaamriwa wazisarende bastola zao watazikuta mwanza airport polisi wa tz wakataka kubisha interpol wakasimama kidete wakawaambia muiten mkubwa wenu yeyote yule lkn hatutawaruhusu kusafiri na bastola zenu na pingu. Anasema itafika mahali wakiua wananchi 10 nanyi ueni 100.Siku hz jela kwa cdm ni bedroom na polisi ni sitting room.
UPDATE
Mnyika kapanda jukwaan, John Heche mkiti wa bavicha anaingia ndani ya mkutano.
Mnyika anamnadi mgombea wa cdm wa'serikal ya mtaa wa mabibo sahara.
John Heche sasa jukwaan anamwaga sera. Anasema mnyika ni sawa na wabunge 100 wa ccm. Rais wa tz anapishana na wazungu angani yeye anatuletea net wazungu wanaondoka na dhahabu. Obama alikuja barabara zikapigwa deki na ommo. Nilikuwa sifahamu kama Mkiti wa Bavicha ana punch nzito kias hiki huyu jamaa kweli anafaa.
Picha zipo tatizo namna ya kuzupload ndo nashindwa
Mnyika anasema CCM wameleta muswada wa kisheria kwamba Rais amepewa mamlaka ya kuteua wabunge 166 kutoka katika asasi za kiraia na za kidini kuingia katika bunge la katiba.
Mnyika anasema akirudi bungen analianzisha tena suala kutekwa ulimboka maana kesi imeisha mahakaman. Kama samaki wa magufuli walikuwa ushahidi waligawiwa kwa watu ikiwa kesi bado ipo mahakaman kwann fedha za DECI zisirudishwe kwa wananchi wakati kesi ikiwa bado ipo mahakamani.
UPDATE
Spika alimwamuru mnyika apeleke muswada wake kwenye kamat ya chenge na alipofika kwa chenge. Chenge akamwamba mnyika hii kodi ya simu ni ndogo sana mnyika akakumbuka kuwa kumbe anaongea na mzee wa vijisenti wa bn 3.
Mkutano umefungwa rasmi.
Ni mimi Ripota wenu Jasho la damu kutoka Radio ya JF-Mabibo.
 
Peoples.....power leo lazima yaibuliwe makitu huko

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Filimbi imelia ccm leo inazikwa rasmi viwanja vya sahara mabibo kuanzia saa 9 mchana.

Tunayasubiri mabomu tena yalipuliwe na polisi kama kawaida unavyokuja mkutano wa MAKAMANDA.
Je leo anarushiwa nani bomu kati ya hao waheshimiwa? Yangu macho!!!
 
Acheni watu wafanye kazi, mnawapeleka watu kwenye maandamano, ikifika jioni nyie mnapokelewa na sukari na mkate NA WATOTO WENU, alafu sisi tunaingia nyumbani kwa kujificha na ukuta tukiwa tumechoka mpaka kitandani, huku nikiwaacha watoto wangu wakipiga miyao sebuleni wanamsubiri baba atoke kazini.
 
One day i will join them. Tz must b rescued from this neo colonism
 
Kuna uzi mwingine unawataja hao wabunge kuwa wapo jimbo la hai kwa mbowe na wanafanya mikutano kumi kila siku. Sasa tujue wakoi wapi, dar au hai?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Acheni watu wafanye kazi, mnawapeleka watu kwenye maandamano, ikifika jioni nyie mnapokelewa na sukari na mkate NA WATOTO WENU, alafu sisi tunaingia nyumbani kwa kujificha na ukuta tukiwa tumechoka mpaka kitandani, huku nikiwaacha watoto wangu wakipiga miyao sebuleni wanamsubiri baba atoke kazini.

afadhali hao wanaokwenda kwa miguu yao na nauli yao kutafuta ukombozi,je ninyi mnaopelekwa kama punda kwenye mikutano yenu kwa kupewa elfu kumi mkn ukiisha mnaachwa kama yatima?
 
Mbona kuna uzi mwingine unasema wabunge wote wa cdm wako jimboni kwa mbowe?
 
Makamanda muwe karibu na polisi maana imani kwa umma imeondoka
 
Acheni watu wafanye kazi, mnawapeleka watu kwenye maandamano, ikifika jioni nyie mnapokelewa na sukari na mkate NA WATOTO WENU, alafu sisi tunaingia nyumbani kwa kujificha na ukuta tukiwa tumechoka mpaka kitandani, huku nikiwaacha watoto wangu wakipiga miyao sebuleni wanamsubiri baba atoke kazini.
Acha kuweweseka gamba wewe, tulia dawa ikuingie vizuri.mkisikia mkutani wa chadema mnaweweseka tulia .
 
Duh ama kweli eneo hilo linapata mapumziko mema sana kumpata Slaa na Mdee wakiwa wageni very nice .
 
Filimbi imelia ccm leo inazikwa rasmi viwanja vya sahara mabibo kuanzia saa 9 mchana.
UPDATE
Watu wameanza kumiminika uwanjan natumia nokia E63 nifundishen namna ya kuapload picha.

​Kumbe Dar, CDM haiwezi kupata watu hata ifanyeje , dar ina wenyewe watakao kwenda pale ni wahamiaji wa mikoa ya kaskazini waliopo dar. Dar ina watu wanaojitambua, ndio maana humu JF wasio penda Amani hua wanailaumu dar kuwa inawaangusha.
 
Makamanda muwe karibu na polisi maana imani kwa umma imeondoka
Red brigade ulinzi uimarishwe, maana policcm lazima waje na mabomu.lindeni kama ule mkutano wa kuwashukuru wana arusha
 
Thats whatsup...M4C lazima iwe intensified... hakuna kuwapa pumzi CCM, Mwanzo Mwisho ... taratibu wananchi watajenga roho ya ujasiri na ujemedari... coming 2015 watajua pa kukimbilia hawa wezi wauza unga wakubwa ...
 
​Kumbe Dar, CDM haiwezi kupata watu hata ifanyeje , dar ina wenyewe watakao kwenda pale ni wahamiaji wa mikoa ya kaskazini waliopo dar. Dar ina watu wanaojitambua, ndio maana humu JF wasio penda Amani hua wanailaumu dar kuwa inawaangusha.
Wewe endelea kuota tuu! :target:
 
Back
Top Bottom