DOKEZO Mdau – Mpanda: Watoza Ushuru Stesheni ya Mpanda wanapiga dili sababu mizigo ya treni haikaguliwi njiani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
large-1632397519-DSC_0071.jpg

Picha kwa Hisani ya TRC

Jamani nawapongeza kwa kupaza sauti na kwa taarifa mnazozitoa Jamii Forums, nyie ndio Chombo pekee cha Watanzania ambacho mnatupa nafasi ya kueleza kero zetu kwa uwazi bila konakona.

Naomba nitoe dukuduku langu, Serikali iangalie eneo la Stesheni ya Mpanda, Katavi, Ofisi ya Watoza Ushuru wanachikifanya si haki, wanashirikiana pamoja na Afisa Mapato wa Manispaa kuwawezesha baadhi ya watu kukwepa kodi.

Mfano unakuta kuna behewa linaweza kupakia gunia hata 2,000 za mchele, kila gunia likilipia ushuru likakatiwa risiti unakuta inatakiwa ilipwe Shilingi milioni 7, lakini Watoza Ushuru wanazungumza na Wafanyabiashara wanaohusika, wanatoa Shilingi Milioni 2, mchezo unakuwa umekamilika.

Nasema hivyo kwa kuwa naona jinsi watu binafsi wanavyoingiza mkwanja wa maana huku Serikali ikipata pato kidogo, kisha sisi Wananchi ndo wa kwanza kulalamika kuwa Serikali haitufanyii hiki au kile.

Kibaya zaidi hata hicho kiwango kidogo walichoingiza yaani mfano Shilingi Milioni 2 kama nilivyosema, ingawanywa kwa Watoza Ushuru wa hapo Stesheni na Afisa Mapato.

Baada ya kuwa michezo hiyo imefanyika wanajua yule mwenye mzigo atakuwa salama hadi kituo anachofika kwa kuwa hakuna mtu wa kusimamisha treni njiani ili kukagua, hivyo hapo mwenye mzigo nacheza dili pia na wale wanaopokea, yaani katik kituo cha upande wa pili.

Kodi inakuwa ndogo au wakati mwingine haipo kabisa kutokana na kuwa wanaamini hakuna Afisa wa Kodi au Askari anayeweza kusimamisha Treni njiani ili kague kama wanavyofanya kwenye mabasi na magari mengine.

Wito wangu ni kuwa sisi Wananchi tunataka maendeleo ya maeneo yetu, ili kuibana vizuri Serikali na mamlaka zilizopo eneo la tukio basi uchunguzi ufanyike na ikibainika kuna michezo michafu hatua zichukuliwe ili haki itendeke na mapato yapatikane, ukimya wetu ndio umasikini wetu.
 
Weka Details vzur.
Serikal haiwez kufanyia kaz mifano yko. Neno kwa Mfano. Lina maanisha huna uhakika
Speak with Evidences
TAja majina ya hao wahusika
 
Back
Top Bottom