Nasikitika kuwatangazieni nyote kuwa mwenzetu LiverpoolFC amefiwa na Baba-Mkwe wake hapo jana, na muda huu ndio yupo kwenye maandalizi ya safari kuelekea huko jirani na Ngorongoro kwa shughuli za maandalizi ya mazishi.
Kwa harakaharaka amenijuza kuwa huenda mazishi yakafanyika kati ya Alhamis au Ijumaa hii.
Pia amenieleza kuwa chanzo cha kifo cha huyo baba ni ajali ya baiskeli, ambapo vijana wawili waliokuwa wamepakizana kwenye mteremko walimparamia na bike yao, wakimwangusha chini ambapo alipigiza kichwa kwenye lami.
Juhudi za kumwahisha Hospitali hazikuzaa matunda, maana alifariki kabla ya huduma yoyote.
Mungu ailaze roho ya arehemu mahala pema peponi.
Pole sana LiverpoolFC kwa maswahibu hayo na tuko pamoja na wewe.