Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Jiunge nasi kufuatilia kinachoendelea kwenye Mdahalo kuhusu matokeo ya utafiti wa Twaweza > Utafiti wa TWAWEZA: Rushwa imepungua lakini hali ya maisha imezidi kuwa ngumu ambao unazinduliwa LIVE kutoka hapa Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na Chuo cha IFM).
Je, wananchi wana maoni gani kuhusu vipaumbele vya Serikali, utendaji wake na siasa nchini?
Wazungumzaji waalikwa ni wanasiasa mashuhuri nchini ambao ni;
1. Nderakindo Keesy - NCCR
2. Zitto Kabwe - ACT
3. Tundu Lissu - CHADEMA
4. Humphrey Polepole - CCM
Ungana nasi mpaka mwisho.
--------------
H. Polepole(CCM): Kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli(71%) ni juu ya wastani wa kukubalika kwa marais wengine Afrika
Dr. Nderakindo Kessy(NCCR): Mfumo wa uongozi uliowekwa na wananchi(Katiba) ni muhimu zaidi kwani kiongozi atafanya anachotakiwa kufanya
Dr. Nderakindo Kessy: Wananchi wanaposema rushwa si tatizo wanazungumzia rushwa ndogondogo, rushwa kubwa za kitaifa bado zipo
Dr. Nderakindo: Umaarufu wa vyama vya siasa umeshuka sababu vyama vimefungwa midomo, umaarufu wa vyama ni kupiga domo
H. Polepole: Katiba haitakiwi kuwa hoja ya Vyama vya Siasa kujipatia umaarufu - Katiba ni suala la wananchi
Polepole: Huwezi kuzungumza Katiba ukiwa na mikono michafu - CCM tunasafisha mikono yetu kabla ya kuzungumzia Katiba
Polepole: Wenye mikono michafu wengi wako Upinzani kwa sasa, hata suala la Madini ni wao wanapinga
Polepole: Wapinzani kulalamika kufungwa midomo sio kweli, wana ruhusa ya kuandamana kwenye majimbo yao lakini hawafanyi hivyo
Dr. Kessy(NCCR): Hakuna chama kinachoitwa upinzani; si sawa kusema kila linalofanywa na chama kimoja kimefanywa na 'Upinzani'
Ado Shaibu(ACT): Ni taratibu za wapi zinazosema kuwa chama ni sharti kinawe mikono ndipo Katiba ishughulikiwe?