Mdahalo wa Twaweza kuhusu Utafiti unaohusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini Tanzania

Aisee ! Hizi 'tafiti' za Twaweza zinaniacha hoi ! Sasa wanaposema 2013 CHADEMA ilikuwa inakubalika kwa 32% na kukubalika huko kukawa kunashuka mpaka 17% mwaka 2017, ilikuwaje mgombea urais kupitia CHADEMA akapata zaidi ya asilimia 45 ya kura zote? Tena
matokeo ya utafiti wa Twaweza yanasema CHADEMA inakubalika zaidi miongoni mwa vijana. Kama vijana ni zaidi ya 60% ya Watanzania, inakuwaje asilimia ya wanaokubali CHADEMA iwe 17% tu? Sioni mantiki ya matokeo haya.
Jibu ni rahisi - 45% ilitokea kwa sababu mgombea aliazimwa kutoka CCM.
 
Jiunge nasi kufuatilia kinachoendelea kwenye Mdahalo kuhusu matokeo ya utafiti wa Twaweza > Utafiti wa TWAWEZA: Rushwa imepungua lakini hali ya maisha imezidi kuwa ngumu ambao unazinduliwa LIVE kutoka hapa Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na Chuo cha IFM).

Je, wananchi wana maoni gani kuhusu vipaumbele vya Serikali, utendaji wake na siasa nchini?

Wazungumzaji waalikwa ni wanasiasa mashuhuri nchini ambao ni;

1. Nderakindo Keesy - NCCR
2. Zitto Kabwe - ACT
3. Tundu Lissu - CHADEMA
4. Humphrey Polepole - CCM

Ungana nasi mpaka mwisho.

--------------

H. Polepole(CCM): Kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli(71%) ni juu ya wastani wa kukubalika kwa marais wengine Afrika

Dr. Nderakindo Kessy(NCCR): Mfumo wa uongozi uliowekwa na wananchi(Katiba) ni muhimu zaidi kwani kiongozi atafanya anachotakiwa kufanya

Dr. Nderakindo Kessy: Wananchi wanaposema rushwa si tatizo wanazungumzia rushwa ndogondogo, rushwa kubwa za kitaifa bado zipo

Dr. Nderakindo: Umaarufu wa vyama vya siasa umeshuka sababu vyama vimefungwa midomo, umaarufu wa vyama ni kupiga domo

H. Polepole: Katiba haitakiwi kuwa hoja ya Vyama vya Siasa kujipatia umaarufu - Katiba ni suala la wananchi

Polepole: Huwezi kuzungumza Katiba ukiwa na mikono michafu - CCM tunasafisha mikono yetu kabla ya kuzungumzia Katiba

Polepole: Wenye mikono michafu wengi wako Upinzani kwa sasa, hata suala la Madini ni wao wanapinga

Polepole: Wapinzani kulalamika kufungwa midomo sio kweli, wana ruhusa ya kuandamana kwenye majimbo yao lakini hawafanyi hivyo

Dr. Kessy(NCCR): Hakuna chama kinachoitwa upinzani; si sawa kusema kila linalofanywa na chama kimoja kimefanywa na 'Upinzani'

Ado Shaibu(ACT): Ni taratibu za wapi zinazosema kuwa chama ni sharti kinawe mikono ndipo Katiba ishughulikiwe?

Anachosema Humphrey Polepole hakina mashiko maana chama chake ndicho kimeunda serikali ambayo imeingia mikataba na sheria mbovu - kwa hiyo kujikosha as if wamefanya kila kitu vizuri ni kuwadanganya wasiojitambua. Inabidi watuombe radhi sisi wananchi kwa kuingiza nchi yetu mjini kwa kusaini mikataba mibovu na kutunga sheria mbovu kwa kutumia wingi wa wabunge wao bungeni.
 
Jibu ni rahisi - 45% ilitokea kwa sababu mgombea aliazimwa kutoka CCM.

Siyo kweli. Ni kutokana upinzani kutoruhusiwa kuuza sera zao kwa wananchi. Kwenye TV tunamwona tu Rais akizindua miradi, akiongea na wananchi, nk wakati wengine wakifanya hivyo wanazuiwa tena kwa kupigwa, kuwekwa ndani na kufunguliwa kesi za jinai. Mahali ambapo hakuna fair au level political ground huwezi kutegemea kukua kwa demokrasia ya vyama vingi. Ni kama tumepiga hatua kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Pili, Polepole ameshaondoka kwenye kutoa hoja na kuanza kuwashambulia viongozi wa upinzani. Kila mara anarudia yaleyale mpaka anapwaya.
 
Je, unadhania CCM itakuwa na mkakati gani baada ya kufahamu kwa mujibu wa utafiti wa Twaweza aina ya wananchi walio wengi wanawakubali ili kuongeza kukubalika?
 
Aisee ! Hizi 'tafiti' za Twaweza zinaniacha hoi ! Sasa wanaposema 2013 CHADEMA ilikuwa inakubalika kwa 32% na kukubalika huko kukawa kunashuka mpaka 17% mwaka 2017, ilikuwaje mgombea urais kupitia CHADEMA akapata zaidi ya asilimia 45 ya kura zote? Tena
matokeo ya utafiti wa Twaweza yanasema CHADEMA inakubalika zaidi miongoni mwa vijana. Kama vijana ni zaidi ya 60% ya Watanzania, inakuwaje asilimia ya wanaokubali CHADEMA iwe 17% tu? Sioni mantiki ya matokeo haya.

fact mkuu Twaweza wanatuchanganya vichwa
 
isije kuwa umesahau mgombea wa CDM alikuwa fresh kutoka ccm na kundi lake la 'ulipo tupo'...
 
Humphrey hajui kujenga hoja, anataka kudanganya wananchi mchana kweupeee. Ado amemgalagazaje?
 
Back
Top Bottom