Kusema ukweli babu ukisoma vizuri ule mdahalo wa kwanza utaona kuwa tulikuwa tunazungumzia vitu tofauti. Watoto wanayo nafasi yao kama watoto na huwezi kuwalinganisha/judge kwa vigezo vya spourse. Katu hatuwezisema mapenzi yako kwa mke/mume ni zaidi kuliko kwa watoto au mapenzi yako kwa watoto ni zaidi ya kwa mke/mume kwani utakuwa unalinganisha aina tofauti za upendo.
Nilikuwa tu najaribu kuwaza kwa nguvu na ni mara nyingi tunasikia wanawake wakilaumiiwa kuwa wakishapata watoto huhamishia mapenzi kwa watoto na kuwasahau wababa hali inayopelekea wababa kuseek other camps kwa ajili ya fidia. The same applies kwa wamama. Unapokutana na mtu ambaye mistakenly anachanganya upendo wa watoto na ule anaopaswa kumpa spouse wake ni wazi mahusiano yatakuwa na mushkeli na katu, nasema katu hutoeleweka iwapo utamweleza mwenzio LIVE and ON A SERIOUS NOTE kuwa unawapenda watoto zaidi ya unavyompenda yeye au ukamwonyesha kwa matendo asiumie (hata kama hatokuonyesha kuwa ameumia).
Wanawake wengi tunajinyima haki zetu, wengi tukishapata watoto na Mr akawa anawajali sana watoto kuliko anavyokujali wewe mama, tunatend kuridhika kuwa .......ah lakini anawajali watoto, anahakikisha wanakula, wanakwenda shule nzuri, analipa ada , inatosha hata kama kwangu hanionyeshi mapenzi naridhika. This is WRONG. Wewe kama mke unayo haki yako kupendwa, kujaliwa na kufurahishwa. Sio usubstitute upendo wako kwa kuwa anawapenda watoto. Sijui lakini I just feel kuwa its not right na wala hatutokuwa tunatumia scale sahihi kulinganisha watoto na spouses wetu.
Hivi tulishajiuliza utajisikiaje inapotokea Mke ambaye anao watoto wake (hukuzaa naye) halafu akakupa na ku7kuonyesha live kuwa anawapenda wanae zaidi ya anavyokupenda wewe kama spouse wake? Will you be comfortable with that? I think confessions nyingine ni bora zikaungamiwa tumboni kwa kweli. Its a damage in the relationship.
Ni mtazamo wangu tu huu, and not under the influence of any alcohol.