Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, hawa kina Maggid ni wengi sana kwa sasa. Wametapakaa kila kona. Ukifuatilia vyombo vya habari vilivyoripoti leo kuhusu ile 'TV Show' ya Dk Slaa unaweza kusikia kichefuchefu na hasa magazeti ya Habari Leo, Jambo Leo na lile la Uhuru. Ameibuka mtu mmoja anayeitwa Ngeleja kujaribu kujibu hoja za Dk Slaa zinazohusu madini. Msomaji wa Magazeti pale TBC Taifa yeye ndiye alienda mbali kwa kusema, "Gazeti la Mtanzania Daima limeandika Slaa aumbuliwa" Sina uhakika kama upotoshaji huu ulikuwa wa makusudi au 'ukanjanja' wa mtangazaji huyo maana toka nizaliwe sijawahi kuliona gazeti la Mtanzania Daima.

Kuhusu Maggid, kama mtakuwa mmefuatilia tangu wiki iliyopita alianza kumtajataja Profesa Lipumba. Kwenye makala yake katika gazeti la Raia Mwema aliandika 'Mbio za Urais: Lipumba anakuja, chupa ya maji mkononi!' Aliandika mengi lakini akionyesha kuwa Watanzania wamemsahau Lipumba na kujikita zaidi kwa wagombea wengine, humo ndani akimpa 'misifa' Prof Lipumba. Maggid anacheza na akili za watu kujifanya yeye si mshabiki wa CCM. Nadhani lengo lake ni kuwa wale ambao hawataki kusikia 'madudu' ya Meneja Miradi wa CCM ambaye pia ni mgombea Urais kupitia chama hicho wamwone mbadala wake ni Profesa Lipumba na kwa kuwa huyu mgombea wa CUF sio 'dili' zaidi ya kupunguza kura za Slaa kutoka kwa wapinzani.

Kwenye Blogu yake Maggid ameshaandika mkataba wake wa kazi anayofanya sasa unaisha mwezi wa 12 mwaka huu. Maggid hata kama unafukuzia 'u DC' ndugu yangu macho yako yawe na aibu! Kuna faida gani kushusha Integrity na credibility yako kwa vivyeo vya 'kipuuzi' Maggid inaonekana Makala hii ya mdahalo wa Slaa ulishaiandika kabla hata Slaa hajaongea na kibaya zaidi hukufuatilia hata ule mjadala kwenye TV. Laiti kama ungefuatilia nina imani usinge post hiyo 'Makala Uchwara' yako. Kinachoendelea hivi sasa ni wewe kung'ang'ania kuwa ule haukuwa mdahalo na unachotaka watu wajadili kuwa ule ulikuwa mdahalo au la! Na kwa hakika umefanikiwa kwa sababu humu ndani tumeacha kujadili mambo ya muhimu aliyoyaongea Dk Slaa juzi.

Maggid kwa kuacha kumsikiliza Dk Slaa umepitwa mengi ikiwemo majibu ya yale maswali aliyoiliza yule 'mpuuzi' kwenye Blogu yako kuhusu Makaratasi Feki ya Kura kule Tunduma. Dk Slaa alijibu kwa ufasaha. Maggid nani asiyejua sasa hivi kuna mbinu chafu zimekuwa zikifanywa ili kuzuia yale anayoyasema DK Slaa kwenye mikutano yake yasiripotiwe?.

Maggid wewe endelea na ushabiki wako kwa CCM lakini ungewaonea huruma wale ndugu zako wa kule Kinyeregete. Ambao umekuwa ukitoa picha zao mara kwa mara kwenye Blogu yako wakiwa wamevaa 'masempele' na vile vijumba vyao ambavyo unajiuliza ni mabanda ya kuku au ni mapango ya kufugia ndezi. Wale wanao machotara uliowapeleka kule Kinyeregete huwezi kuniambia maswali waliyokuuliza lakini nadhani waliona kama vile wako 'Mikumi' ya wanyama wanaoitwa Binadamu! Picha zako zote za kule Kinyeregete sijawahi kuona nyumba yako au hata ya baba yako zaidi ya zile za wale unawaita shangazi zako, wajomba zako. Niambie mara ya mwisho ulimaliza usiku mzima pale Kinyeregete lini kama sio kupita dakika moja na kuwaachia ndoo za vitunguu na nyanya zile unazotuonyesha kila siku! Acha bana! Halafu najiuliza huku kwa JK umekuja lini? Najua mwaka 1995 ulikuwa wapi na mgombea wako unakumbuka alivyochafuliwa jina na hawa 'wahuni' Jamani!

Maggid wanao wanasoma International School na huenda hata maisha yao ya baadaye yanaweza yasiwe pale Kinyeregete au hata Kinondoni Biafra. Sasa mwache Slaa aje asomeshe watoto wa Kinyeregete bure na kuangalia afya zao bure, sio kuwapiga picha na vitambi vyao huku wakiwa na umri mdogo wa miaka sita na kwenda kuziuza Sweden. Acha bana!
 
KWA HIYO KUAMUA WA KUMPIGIA KURA BAINA YA DR. SLAA NA MWAKITWANGE? KWANZA NI NANI ALIYEKUOMBA UWASILISHE, AU UNADHANI UNAWASILISHA DOKEZO LA KUFISIDI NCHI. Rudi tena shule haraka! uchambuzi wako non-sense kabisa.
 

So what about it?.....mbona hao wengine walihudhuria?Ansbert tumeambiwa ni MD haimaanishi kuwa ndiye mmiliki...kwani Kiondo Mshana anamiliki IPP Media Ltd?
 

Hii ndiyo ilikuwa nia yako, wewe ni mtu hatari sana watu hawajui tu, tuwekee scan ya pasipoti yako hapa kama unaubavu, Tuache wapiga kura halali tuchague..wewe ni mtalii tu.
 
Nothing can be further from the truth. CCM walikataa tangu mwanzo kuhusu midahalo kwa wangombea wake kuanzia ubunge hadi urais. Inavyoonekana Prof. Lipumba yuko so busy na kampeni kiasi kwamba hata mahojiano kati ya ITV na wagombea Urais yanayoendelea katikati ya wiki hajaonekana ( Kina Dovutwa na Mziray na Dr. Slaaa) tumewaona. Inawezekana kwa vile Lipumba anatumia usafiri wa gari muda wake kwa mahojiano ni finyu sana. Sasa sijui Majjid alitaka Mdahalo Dr. Slaa afanye na nani? Hata mahojioano kati ya Star TV Dr. Slaa alifanya na Col. Kinana kana kwamba Kinana ni mgombea! Watu walimuuliza kwa nini JK hayupo Kinana akagwaya!! Sasa ITV wangefanyaje??
 

Nakubaliana na wewe kabisa....Mdahalo ITV Bila JK kwa nini? Maggid naomba jibu
 
Ndugu Zangu,

Kwanza kabisa , niweke wazi, kwamba kwa staili yangu nilichokoza kwa makusudi mjadala ili kutengeneza mwelekeo wa mjadala ambao ungetusaidia kuyafanya mawili haya;
Mosi, kuumiza vichwa vyetu kujadili nini haswa maana ya mdahalo na hususan mdahalo wenye kuhusu masuala ya msingi ya kitaifa. Kufanya kazi ya kuitafuta tofauti ya kimsingi kati ya mdahalo na mahojiano. Hilo nilijaribu kuliandika kwa msisitizo katika majibu yangu katika baadhi ya posti zenu.
Pili, nilitarajia, baada ya kukaikamilisha kazi hiyo ya kwanza, wengi wetu tungejikita kwenye kujadili issues zilizozungumwa na Dr Slaa usiku ule wa Jumamosi. Nilishangaa, kuwa wengi wakaelekea kwenye kuniachia mimi niifanye kazi hiyo. Sikufanya hivyo, kwa makusudi kabisa. Ningefanya hivyo, mjadala huu ungemalizika jana usiku kwa watu kuandika ' thanks' zao. Tusingejifunza mengi.

Tukija kwenye issues, Dr Slaa alipata fursa nzuri sana ya kujieleza. ( Niligusia hilo kwenye moja ya majibu yangu ya posti ). Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, Dr Slaa angefanya vema zaidi kama angepambanishwa na mtu kama Profesa Lipumba. Na hapo, umma ungeweza kumpa alama za ziada. Na laiti JK naye angeingiza timu, basi, tungeshuhudia ' mdahalo wa karne' kati ya Profesa Lipumba, Jakaya Kikwete , Dr Slaa na akina Hashim Rungwe na wenzake. Ni katika hali kama hizo, wapiga kura tunasaidiwa kupeperusha pumba na kubaki na mchele. Niliandika, kuwa ni mkakati wa kimakosa kwa CCM kuamua kutoshiriki midahalo. Maana, huko twendako wataihitaji na kuna watakaowashangaa watakapoonyesha hitaji hilo.
Sababu kubwa ya kuwepo walau wagombea wawili kwenye mdahalo ni ukweli, kuwa wapiga kura tungepata fursa ya kusikia sera mbili tofauti au majibu mawili tofauti kwa swali moja. Hapo, tungeweza kujua nani bora zaidi.

Format ya maswali ingekuwa ni yale maswali magumu yanayohusu most controversial issues of our time. Issues kama uharibifu wa mazingira, ufisadi, mikataba mikubwa ya uwekezaji,. Rasilimali za nchi kama madini, Uongozi bora na maadili ya viongozi( Tuna mfano wa Rais aliyefungua kampuni binafsi na kwa kutumia anwani ya Ikulu)
Tuna issues kama za kuwepo au kutokuwepo kwa wagombea binafsi, Katiba, Uraia wa nchi mbili, upigaji kura kwa Watanzania walio nje, mishahara ya Wafanyakazi, nafasi ya wakulima katika uchumi wan chi (Kilimo kwanza), maradhi (UKIMWI na Malaria). Bila kusahau Kushuka kwa elimu na utitiri wa international schools na academies zilizo chini ya viwango. Na mengineyo mengi.
Kuna pia maswali ambayo hayakuulizwa usiku ule. Moja ni hili la itikadi. Mathalan, Dr Slaa na CHADEMA wanasimama katika itikadi gani kwa sasa katika kutekeleza sera zao? Na kama Jakaya Kikwete, Profesa Lipumba na wengine wangekuwapo, nao wangeulizwa swali hilo.
Mwisho, nasikitika kuwa huenda wagombea wengine wa Urais mbali ya Profesa Lipumba , hawatapata nafasi ya kufanya mahojiano kama wenzao wa CHADEMA, CUF na labda CCM. Nafikiri hawatendewi haki akina Hashim Rungwe , Kuga Mziray na mwenzao Muta wa TLP kama nao hawatapata hata robo saa tu ya mahojiano.
Huko twendako, tuwe na matayarisho ya mapema ya midahalo ya kitaifa inapofikia wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu au masuala mengine makubwa ya kitaifa, kama vile Katiba mpya. Kuwepo na taasisi huru na zenye kuaminika na umma zitakazoratibu midahalo hiyo. Kuwepo na kalenda ya midahalo. Mgombea atakayeshindwa kuhudhuria katika tarehe husika ilihali amepewa mwaliko, basi, huyo itakuwa ' imekula kwake' kama wanavyosema mitaani siku hizi.

Nihitimishe kwa kuwashukuru nyote. Nimesoma kila kilichoingizwa kwenye mjadala huu. Kuna mlionishambulia kwa matusi, nimeyasoma matusi yenu, mengine yamenivunja mbavu. Kuna mliotoka nje ya mada na kunishambulia mimi binafsi badala ya kuikabili hoja iliyowasilishwa. Hilo nalo ni pungufu la kawaida. Na kwa kuchokoza mjadala huu kuna wanaojisikia nimewakwaza, basi, haikuwa dhamira yangu. Sijaufunga mjadala.

Ahsanteni Sana.
Iringa,
Jumatatu, Oktoba, 25, 2010
 

wewe huna akili hujaona kipindi ila unakijadili ndio maana kuna mtu kasema hapo kwanza uliandika kabla .....shame on u
 
Next?
 
Baregu hawezi kumruhusu Slaa kukaa jukwaa moja na Lipumba kwenye mdahalo. Anajua kilichompata Mrema Mwaka 1995.
 
Baregu hawezi kumruhusu Slaa kukaa jukwaa moja na Lipumba kwenye mdahalo. Anajua kilichompata Mrema Mwaka 1995.

La hasha....Mrema mwenyewe ndie alijiharibia...vile vitu walivyomwambia wakina Baregu azungumzie akavidaharau na kuweka pembeni..akakazania Chavda..Chavda...nusura nimpopoe mawe.....sasa wewe unataka kusema tafauti ngugu?
 
Baregu hawezi kumruhusu Slaa kukaa jukwaa moja na Lipumba kwenye mdahalo. Anajua kilichompata Mrema Mwaka 1995.

Lipumba is a professor (Dr) na kwa mtazamo wangu he is no where near Dr. Slaa kwenye uwezo wa kujenga hoja.
 
mengi in nature mbaguzi na hakuna sumu mbaya kwa taifa kuliko ubaguzi

Wewe ni mbaguzi kama chura.......Mzee mengi angekuwa mbaguzi asingekusaidia wewe na wengine kupeleka watoto wakatibiwe moyo india!!
 

Kwa maneno hayo kwenye red, hata kama Magid ni Mchmia tumbo namba moja, atatokwa machozi. Haya maneno ndiyo yaliyomfanya Yuda ajinyonge, baada ya kugundua kuwa, pesa si kila kitu. Baada ya kuona mtu wake aliyekuwa anampenda kweli kweli anasulubiwa kwa vipande thelathini vya fedha.
Maggid Pesa si kila kitu. Wala ufuasi was dini haukufanyi uwe mtakatifu. Ni ukweli tu ndiyo utakufanya uishi huru, kwenye jamii ya watu huru, ambao wanakuona wewe ni mwenzao. Jina la Nyerere litaishi milele, lakini sijui kama jina la Kingunge Ngombare Mwiru litadumu hata mwezi mmoja ndani ya masikio ya Watanzania siku Mungu akimchukua!
Usiuze utu, kwa ushabiki na pesa kwa vile tu umelipwa talanta mia. Maisha ni zaidi ya fedha!
 
Mkuu, Wale wasiojiamini, wemegomea mdahalo, wanaogopa maswali ya papo kwa papo. Mfano Mh. makamba alisema ukitaka washiriki wapewe maswali kabla. wampe Kinana awatafutie majibu kwanza ndo watashiriki. Dr. Wakweli Slaa amefikisha ujumbe. Kama una hoja sema kwa yale aliyojibu. Ulikuwa mdahalo, mahojiano, au majibizano haijalishi, Ujumbe umefika.
 
mengi in nature mbaguzi na hakuna sumu mbaya kwa taifa kuliko ubaguzi

Sasa huko ni kuchanganyikiwa! Waliojirani wamnusuru asijejitundika kamba! Hafla ile na nyingine zitakazofuata zimeandaliwa na asasi maalum ikiwemo vox media, kazi ya ITV ni kurusha matangazo... Kutamka ulicho na hakika nacho ndio busara yenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…