RayB
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 2,751
- 196
Jamani Maggid alikuwa na hoja katika jambo hili. Binafsi ningependa na wagombea wengine wawepo katika mdahalo huo.
Shida inayonipata na kuleta tofauti kwangu na Maggid ni ile ile. Uandishi wa upande mmoja.
Maggid alitakiwa kabla hajaleta mada yake hapa awe amewasiliana na waandaaji wa mdahalo huo na kuwauliza kwa nini unaitwa mdahalo wakati anayekwenda katika mdahalo huo ni mtu mmoja?
Mdahalo huu haukuwapo wa ghafla. Ulitangazwa kwa siku zaidi ya tatu nadhani. Na ilijulikana ni mtu mmoja atakayekuwepo wala haikuwa siri. Na yawezekana kuna sababu za mantiki kwa nini ni mmoja tu aliyeweza kuonekana au kuthibisha kushiriki na wengine wasishiriki. Maggid kama mwandishi msomi alitakiwa kuwatafuta waandaaji na kuwauliza kabla ya kuja na maandishi yake yasiyotenda haki. Kama Maggid ni mwandishi msomi anajua wazi uandishi wa jinsi hii haukubaliki kitaaluma.
Namshauri Maggid arudi kwanza na kuwatafuta waandaaji, awaulize maswali, then, aje hapa na malalamiko yake with evidence of what he has collected kutoka kwa waandaaji then tu-discuss. Bila hivyo, attacks zote anazopata hapa ni size yake.
Kwanza I doubt hata kama aliusikiliza manake anasema kwenye blog yake kuwa alikuwa njiani kwenda Iringa na alikutana na mlezi wake JK pale Mikumi jamaa pamoja na kuwa ni mgombea lakini Maggid akawekwa kabdo na 'msafara wa mgombea' sasa sijui msafara wa mgombea Slaa naye anaweza kukuweka kando na wewe kutoka kupiga picha.
Yaani pale umejishusha kweli, eti JK alikushangaa uliposimama porini kwenye wanyama wakali ili kumpiga picha. Kweli mapenzi ni makali hayaaa