Kwa mtazamo wangu haya ndo yaliyonifanya niachane na iPhone (IOS) na kurudi kwenye Samsung (ANDROID)
Ukitumiwa wimbo au voice note kupitia app ya WhatsApp wimbo huo au voice note zinabaki mulemule katika conversation na ikitokea ukafuta zile conversation na nyimbo pamoja na voice note vinapotea.
Ukitoka wimbo mpya Kama unataka kuupakua Kuna namna tofauti Kama vile udownload wimbo kupitia PC Kisha udownload iTunes kwenye PC ndo upakue nyimbo Kisha uiingize kwenye simu kupitia itune au udownload special app kwenye simu Kisha udownload wimbo unaoutaka. Lakini wimbo utabaki kulekule kwenye app hutouona wimbo mahala pengine popote.
Kwa wale wapenda photoshoot mapicha ya location umepiga zako picha cameraman kaweka kwenye PC anataka akurushie unaanza ooh! Mie natumia iPhone wewe weka kwako afu unitumie wassap inakua Sasa usumbufu.
Kuna wale wenzangu na Mimi tunapenda kudownload app nyingi nyingi kama vile app za kununua bidhaa au za kutizama nyimbo mpya zinazotrendi Sasa baadhi ya hizo app hazipatikani katika appstore inakua shida.
Matumizi ya Bluetooth pia yamekua Ni changamoto. Bluetooth ya iPhone inakazi moja tu nayo ni ku connect katika device kama vile radio au headphones Ila hutoweza kushare na mwenzako chochote kile.
Kingine app nyingi za kawaida kwamfano Facebook ambayo kwenye Android Ina mb 20 mpaka 25 kwenye iPhone inamb 100 Hadi 500 na bahati mbaya uwe umeweka autoupdate aisee GB 2 zitaisha fesibuku pekee.
Pia ukitaka udownload moja kwa moja nyimbo kupitia iTunes Ni mwendo wa dollar tu.
NB: Sisi wa tandale kwa mtogole unanunua tu ili mtaani wajue Fulani ana iPhone
YANGU NI HAYO TU...
Sent using
Jamii Forums mobile app