jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,990
- 22,523
Nakubali in one way na kukataa in another.Tangu historia ya kale Visiwa vya Zanzibar zimeishi na kufanikiwa kwa kutegemea bara (eneo la mwambao wa Afrika ya Mashariki) na hata maeneo ya ndani ya Afrika. Kufanikiwa kokote kule kunakotajwa kuhusu Zanzibar kumetokana daima na mahusiano yake ya karibu na bara. Bila Bara Zanzibar haiwezi kufanikiwa hata leo hii. Lakini zaidi mafanikio yake ya huko nyuma yalitokana sana na Zanzibar kuwa na ukuu wa kutawala maeneo ya bara. Haijawahi kufanikiwa bila kuwa na nguvu ya kiutawala au kisiasa huko bara. Hili linaonekana hata leo hii katika MUungano wetu ambapo Zanzibar bado wanaonekana kuwa na maamuzi mengi kuhusiana na bara na wanafanikiwa zaidi kwa mgongo wa bara na sasa wapo wanaotaka izidi kufanikiwa kwa kile wanachokiita "kuondolewa kero za Muungano".
Hata Muungano ukivunjika bado Zanzibar itajikuta inaitegemea bara kwa namna nyingi zaidi - kiuchumi, ongezeko lake la watu, kiusalama n.k Hii ni kweli isiyopingika.
Kubali au kataa.
Nadhani zenji imekuwa ikiitegemea na kunufaika na bara kutokana na ukweli kuwa Sultan under "Zanzibar Sultanete",alikuwa akimiliki maeneo makubwa ya mwambao wa pwani ya afrika mashariki.Kwahiyo utegemezi hata wa kiuchumi,kisiasa na kiutawala ulikuwepo na bado upo ndo maana kulikuwepo na mapinduzi nk,ambapo wanamapinduzi hao waliwategemea wabara.
Binafsi naamini tunategemeana,na nina amini pia tutaendelea kufanya hivyo hata kama muungano ukivunjika leo.Ni siasa tu lakini hatuwezi kuacha kutegemeana.
Kwa kumalizia,just kwa wasomaji,ungetuwekea hayo mafanikio yaliyoonekana kuwa yamepatikana kutokana na utegemezi huo,hilo lingesaidia zaidi badala tu ya kuwa vague kusema "mafanikio yao mengi yalitegemea bara"