Mdahalo: Hakuna wakati katika historia ambapo Zanzibar haikuitegemea Bara

sizungumzii mapenzi ya Zanzibar kuungana na bara; ninachosema ni kuwa Wazanzibar wanaweza kwenda nje ya Muungano (na inapaswa kuwa hivyo mapema zaidi) lakini ni wao wanaojidanganya kudhania kuwa wanaweza kuishi na kufanikiwa bila bara. Sisi bara tunaweza kuishi na kufanikiwa bila Zanzibar wao hawawezi.

wanaweza wakaish bila bara,,,,,,,nje ya muungano,swala ni MIPANGO TU
 
Mkandara,
Nakubaliana nawe kuwa wanachofanya ZNZ ni kutishia ili matakwa yao yaongezeke.
Imefika mahali hakuna sababu ya kuwabembeleza. Tumejitahidi Pan Africanism unfortunate we have wrong partner.

Msimamo wangu ni kuwa tuidai Tanganyika, si kwa kutaka serikali 3 au mkataba bali kuuvunja kabisa.

At last, umefungua macho,umeona!

How do we do that?

Hiyo sasa ndio iwe kauli mbiu.
Kichwa cha habari za makala.....Tanganyika,Tanganyika, Tanganyika

Na tupeane fikra, vipi tutafika hapo tunapotaka. Kupata Tanganyika yetu. bila kuvishwa joho au koti la muungano.

Sasa mshawishi pacha wako, MJJ badala ya kuipa coverage kubwa Zanzibar sasa, ianze kuidai au kuifufua Tanganyika.
Tena aache huu msamiati wa Bara/ Tz bara.

Hata Muungano kama ulivyo tutumie jina lake la asili. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wachina wanasema safari ya maili elfu,huanza kwa kupiga hatua ya kwanza/mwanzo.

Hongera Nguruvi3.
 
Hadi leo hatujaona kampeni ya kutaka kuvunja Muungano ikianza... hakuna aliyejitokeza kusema Wazanzibar walioko kwenye serikali au utumishi wa MUungano waachie ngazi

Mimi pia sijaona waliochoka kubeba kiroba cha misumari kuchukua hatua!!!! Au ni kauli za kisanii tu kama Muungano wenyewe?

Wote wanaosema Bara(kwa maneno yako),Tanganyika kwa maneno yangu na nguruvi3 kuanzia leo inaingia hasara wanaishia kusema tudai serikali moja...kama wako laki 3.5 ni hasara sasa tuchukue milioni 1.5 zaidi ndio hasara itaondoka?

Tudai Tanganyika!
 
Kama iliwezekana hapo mwanzo kiasi ya kuzisaidia nchi za nje kwa misaada ya kifedha itashindwaje leo ? Subiri 2015 waTanganyika watakapoanza kuchinjana kama kuku ,ndipo mtakapoijua faida ya Zanzibar ,ila kama tunaweza kusimama au hatuwezi kusimama bila Ya Tanganyika ,sisi halituhusu na msimamo upo palepale tuachiwe tupumuwe,tutaanza japo kusimama dede:israel:.
 
Mkandara,

..Ikiwa watagundua mafuta au gesi basi hawatatutegemea. vinginevyo nakuhakikishia watatafuta kila namna waendelee kuwa pamoja na Tanganyika.

..kuhusu utalii, mapato ya Tanganyika ktk sekta ya utalii ni around shilingi trilion 1.4, wakati Zanzibar wanaingiza around bilion 163.

..kukumbusha tu, katika bajeti hii ya juzi ofisi ya makamu wa raisi imetengewa kitita cha shilingi bilion 32 mahsusi kwa ajili ya Zanzibar. kabla ya hapo ZNZ waligoma kulipa sh bilion 40+ ambalo lilikuwa deni la tanesco.

JokaKuu
Mambo ya Muungano yana mapato na matumizi.
Hili haliwekwi wazi. Ngapi zinaingia kama mapato na ngapi zinakwenda kwa matumizi.
Hizo ni nyeti za serikali. Ulalamishi unaanzia hapo.

Deni la Tanesco ni deni la kibiashara na lina mkataba. Anaekiuka mkataba, sheria inachukua mkondo wake lakini Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar kila kitu kinafanywa ni siasa.

Wananchi tunaachwa kwenye mataa, wajanja wanakula nchi. Wananchi wanalishana kasumba na udaku.
 
nijuavyo mimi katika karne ya 13 Zanzibar iliwa ni Empire na ikiitwa Zenji Empire, hapajatokea empire nyingine yoyote ndani ya africa yote,,sasa wakati huo hata neno tangnyika hakuna, halikuwepo na wala hathubutu mtu kujinasibu kuwa ilikuwepo tanganyika,, tanganyika katika historia ilizaliwa baada ya Berlin conference ambapo kama mataifa mengine ya afrika yaligaiwa mipaka na wazungu ili yatawaliwe na tanganyika ikaangukia ndani ya mikono ya wajerumaji chini ya Germany East Africa Company pamoja na kenya mnamo mwana 1890,,,,na kwa wakati huo Zanzibar ni dola kubwa kushinda madola yoyote africa na wala africa nzima kwa maana ya bara hakukuwa na nchi isipokuwa Egypt nyengine zote zilikuwa ni kingship or kingdoms ndogo ndogo zilizoongozwa na makabila hata neno tangnyika lilitolewa na wajerumani baada ya kuripoti serikali yao tanga manake hadi dar salama wakati huo ilikuwa sehemu ya Zanzibar na pwani yote hadi kilwa sasa ukisema hakuna muda Zanzibar haikuwahi kutegemea bara itakuwa unachekesha na wala hujui usemalo. tanganyika haiwezi kuifikia Zanzibar hata kwa asilimia 10 kama hufahamu waulize wazee wa zamani wakitangnyika wanajua hivyo,,manake historia ya tanganyika baada ya uhuru nyerere aliipiga marufuku ili watangyika wasijue asili yao wapi na badala yake wakawa wanasomeshwa ya kupigania uhuru nyerere, kinyengetile basi.

Kimsingi sikubaliam MM kwa namna alivyowasilisha mawazo yake, lakini nadhan ww hukumuelewa kabsa. Labda soma post ya Mkandara hapo juu bila shaka yy amemuelewa. Shortly, historia hii unayoijua wy itakuzidishia stress zaidi kuliko solution.
 
Solution ni serikali moja harafu baada ya hapo sasa tunaigeuza Zanzibar kama Las Vegas, Casino za kumwaga,tunaruhusu coffee shops na windows kama Amsterdam na wale hardliners wote wa Kipemba, Kiunguja, Kingazija na Kitumbatu mtapewa ardhi Sumbawanga mkaendeleze imani kali zenu
 
Jamani apa naongelea suala la security hawa jamaa wenyewe kwa wenyewe wana bifu sasa wakibaki alone si patafuka moshi
 
JokaKuu
Mambo ya Muungano yana mapato na matumizi.
Hili haliwekwi wazi. Ngapi zinaingia kama mapato na ngapi zinakwenda kwa matumizi.
Hizo ni nyeti za serikali. Ulalamishi unaanzia hapo.

Deni la Tanesco ni deni la kibiashara na lina mkataba. Anaekiuka mkataba, sheria inachukua mkondo wake lakini Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar kila kitu kinafanywa ni siasa.

Wananchi tunaachwa kwenye mataa, wajanja wanakula nchi. Wananchi wanalishana kasumba na udaku.

Nonda,

..ZNZ hawachangii ktk mapato wala matumizi ya serikali ya muungano.

..hata yale malalamiko kwamba TRA inakusanya fedha ZNZ na kuzileta D'Salaam yamethibitika kuwa si ya kweli.

..pesa zote zinazokusanywa na TRA ZNZ zinabaki hukohuko visiwani.

..YES, deni la Tanesco ni la kibiashara, lakini hata siku moja suala hilo haliamuliwi mahakamani kama ulivyo utaratibu. mara zote ZNZ hugoma kulipa kwa visingizio mbalimbali, halafu Tanganyika huamua kuwalipia. kuna kipindi Tanesco ilikuwa chini ya management ya makaburu ambao waliamua kuwakatia umeme wa-ZNZ.

. Nonda, kuna ushahidi wa research iliyofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake kuchambua utegemezi wa ZNZ na ukwepaji wa majukumu yake ktk muungano. Wasomi hao wameandika kijarida kuhusu suala hili.

..mwisho, nasimama tena kusema muungano wa Tanganyika na ZNZ uvunjwe.
 
Last edited by a moderator:
nijuavyo mimi katika karne ya 13 Zanzibar iliwa ni Empire na ikiitwa Zenji Empire, hapajatokea empire nyingine yoyote ndani ya africa yote,,sasa wakati huo hata neno tangnyika hakuna, halikuwepo na wala hathubutu mtu kujinasibu kuwa ilikuwepo tanganyika,, tanganyika katika historia ilizaliwa baada ya Berlin conference ambapo kama mataifa mengine ya afrika yaligaiwa mipaka na wazungu ili yatawaliwe na tanganyika ikaangukia ndani ya mikono ya wajerumaji chini ya Germany East Africa Company pamoja na kenya mnamo mwana 1890,,,,na kwa wakati huo Zanzibar ni dola kubwa kushinda madola yoyote africa na wala africa nzima kwa maana ya bara hakukuwa na nchi isipokuwa Egypt nyengine zote zilikuwa ni kingship or kingdoms ndogo ndogo zilizoongozwa na makabila hata neno tangnyika lilitolewa na wajerumani baada ya kuripoti serikali yao tanga manake hadi dar salama wakati huo ilikuwa sehemu ya Zanzibar na pwani yote hadi kilwa sasa ukisema hakuna muda Zanzibar haikuwahi kutegemea bara itakuwa unachekesha na wala hujui usemalo. tanganyika haiwezi kuifikia Zanzibar hata kwa asilimia 10 kama hufahamu waulize wazee wa zamani wakitangnyika wanajua hivyo,,manake historia ya tanganyika baada ya uhuru nyerere aliipiga marufuku ili watangyika wasijue asili yao wapi na badala yake wakawa wanasomeshwa ya kupigania uhuru nyerere, kinyengetile basi.

Mko vigeugeu mno: Mara Nyerere katufanya koloni mara alipiga WAtanganyika wasijijue. Unahisia kama za Shehe YAhaya.

Zanzibar haiwezi kuifikia Tanganyika hata kwa 10% kwenye kitu gani?? fafanua.
 
Kwa muda wote tulio kaa katika muungano,tumekuwa tukitegemeana. Tumeoleana,kufanya biashara kwa pamoja pande zote na mambo mengine chungu nzima.Tatizo si kuuvanja muungano tu. Ni namna gani utakavyovunjika. Kuna watu wanaoshinikiza muungano uvunjwe kwa kutumiwa na baadhi ya watu ndani na nje ya Zanzibar. Hakuna tofauti na mtu anayefuata ngoma ya mdundiko barabarani!

Muungano ukivunjika bado tutakuwa ndugu na kutembeleana kama kawaida. Kwani mtu akiachana na mke au mume kwa taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa kwa amani,kisha wakakutana sehemu hawawezi kuongea? Nashauri kwenye mkataba wa Muungano kuwekwe kipengele cha taraka rejea.
 
Nonda,

..ZNZ hawachangii ktk mapato wala matumizi ya serikali ya muungano.

..hata yale malalamiko kwamba TRA inakusanya fedha ZNZ na kuzileta D'Salaam yamethibitika kuwa si ya kweli.

..pesa zote zinazokusanywa na TRA ZNZ zinabaki hukohuko visiwani.

..YES, deni la Tanesco ni la kibiashara, lakini hata siku moja suala hilo haliamuliwi mahakamani kama ulivyo utaratibu. mara zote ZNZ hugoma kulipa kwa visingizio mbalimbali, halafu Tanganyika huamua kuwalipia. kuna kipindi Tanesco ilikuwa chini ya management ya makaburu ambao waliamua kuwakatia umeme wa-ZNZ.

. Nonda, kuna ushahidi wa research iliyofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake kuchambua utegemezi wa ZNZ na ukwepaji wa majukumu yake ktk muungano. Wasomi hao wameandika kijarida kuhusu suala hili.

..mwisho, nasimama tena kusema muungano wa Tanganyika na ZNZ uvunjwe.

JokaKuu

Iliwekwa thread juu ya Jussa Kumtukana/kumdhalilisha Sitta.Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071438

Hii ripoti inayotajwa na Jussa, Prof. Teddy ameigusia katika kufikia hitimisho la utafiti wake/wao?

Mimi napata tabu kuamini kuwa Zanzibar wanaweza kugoma tu kutochangia au kulipa kile walichokubaliana na Tanganyika kifanyike. Lazima kuna kitu kimejificha au kinafichwa hapa.

Lakini leo nikubali hitimisho la Prof. Teddy kuwa Zanzibar ndiyo tegemezi au inayonufaika na Muungano/ inapata faida.
Sasa tuone upande mwengine wa hoja, Tanganyika inaibeba Zanzibar(inaipa faida Zanzibar) na kwa hivyo, Tanganyika inajiingiza hasara/ inapata hasara na inaendelea kufanya hivyo.

Kuna hoja ya kuwa Zanzibar wanang'ang'ania muungano. Kama hitimisho la Prof. Teddy ni sahihi basi inaingia akilini kuwa Zanzibar yenye kupata faida(inayofaidika) kung'ang'ania muungano.
Je kwa Tanganyika ambayo inapata hasara kwa nini mbali na umaskini uliopo(inakopa, misaada na ufadhili) inaendelea kuipa Zanzibar faida huku yenyewe inapata hasara, na tuseme,hainga'ng'anii muungano?

Kitu ambacho mimi sikifahamu, au hakiingii akilini ni kwa nini Tanganyika iingie hasara na iendelee kubeba kiroba cha misumari? Je huu si ndio hasa ungefaa kuitwa ung'ang'anizi wa muungano?

Lakini, Hasara yote hii ambayo Tanganyika inapata katika Muungano badala ya kudai kuvunja muungano, inafanya kila mbinu kuleta serikali moja. Pia wanatokea watu wenye mawazo kuwa tudai serikali moja. Je hili ndio suluhisho la kutoingia hasara? Au kukiwa na serikali moja ndio faida itapatikana(Manufaa ya muungano yatapatikana)? Kwa vipi?

Na mfumo huo wa serikali moja utakuwa ni mfumo wa aina ipi ya Muungano?

Mimi nasimama kuwaomba wabunge wa Tanganyika wapeleke Mswada binafsi wa kutaka Zanzibar ifukuzwe katika Muungano. Au wabunge wote wa upande wa Tanganyika (bara) wanabariki mazingaombwe ya muungano unaoutia Tanganyika hasara? Uzalendo uko wapi?
 
At last, umefungua macho,umeona!

How do we do that?

Hiyo sasa ndio iwe kauli mbiu.
Kichwa cha habari za makala.....Tanganyika,Tanganyika, Tanganyika

Na tupeane fikra, vipi tutafika hapo tunapotaka. Kupata Tanganyika yetu. bila kuvishwa joho au koti la muungano.

Sasa mshawishi pacha wako, MJJ badala ya kuipa coverage kubwa Zanzibar sasa, ianze kuidai au kuifufua Tanganyika.
Tena aache huu msamiati wa Bara/ Tz bara.

Hata Muungano kama ulivyo tutumie jina lake la asili. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wachina wanasema safari ya maili elfu,huanza kwa kupiga hatua ya kwanza/mwanzo.

Hongera Nguruvi3.

Ha ha ah ah haa...! Hatimaye Nguruvi3 aungama....LET ZNZ GO!
 
JokaKuu

Iliwekwa thread juu ya Jussa Kumtukana/kumdhalilisha Sitta.Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071438

Hii ripoti inayotajwa na Jussa, Prof. Teddy ameigusia katika kufikia hitimisho la utafiti wake/wao?

Mimi napata tabu kuamini kuwa Zanzibar wanaweza kugoma tu kutochangia au kulipa kile walichokubaliana na Tanganyika kifanyike. Lazima kuna kitu kimejificha au kinafichwa hapa.

Lakini leo nikubali hitimisho la Prof. Teddy kuwa Zanzibar ndiyo tegemezi au inayonufaika na Muungano/ inapata faida.
Sasa tuone upande mwengine wa hoja, Tanganyika inaibeba Zanzibar(inaipa faida Zanzibar) na kwa hivyo, Tanganyika inajiingiza hasara/ inapata hasara na inaendelea kufanya hivyo.

Kuna hoja ya kuwa Zanzibar wanang'ang'ania muungano. Kama hitimisho la Prof. Teddy ni sahihi basi inaingia akilini kuwa Zanzibar yenye kupata faida(inayofaidika) kung'ang'ania muungano.
Je kwa Tanganyika ambayo inapata hasara kwa nini mbali na umaskini uliopo(inakopa, misaada na ufadhili) inaendelea kuipa Zanzibar faida huku yenyewe inapata hasara, na tuseme,hainga'ng'anii muungano?

Kitu ambacho mimi sikifahamu, au hakiingii akilini ni kwa nini Tanganyika iingie hasara na iendelee kubeba kiroba cha misumari? Je huu si ndio hasa ungefaa kuitwa ung'ang'anizi wa muungano?

Lakini, Hasara yote hii ambayo Tanganyika inapata katika Muungano badala ya kudai kuvunja muungano, inafanya kila mbinu kuleta serikali moja. Pia wanatokea watu wenye mawazo kuwa tudai serikali moja. Je hili ndio suluhisho la kutoingia hasara? Au kukiwa na serikali moja ndio faida itapatikana(Manufaa ya muungano yatapatikana)? Kwa vipi?

Na mfumo huo wa serikali moja utakuwa ni mfumo wa aina ipi ya Muungano?

Mimi nasimama kuwaomba wabunge wa Tanganyika wapeleke Mswada binafsi wa kutaka Zanzibar ifukuzwe katika Muungano. Au wabunge wote wa upande wa Tanganyika (bara) wanabariki mazingaombwe ya muungano unaoutia Tanganyika hasara? Uzalendo uko wapi?

Nonda,

..wa-Tanganyika wengi hawana habari kwamba kuna kitu kinaitwa muungano.

..kwa mfano: wananchi wa kigamboni wako more concerned na matatizo ya kivuko kuliko suala la muungano.

..mbunge wa kigamboni anapata umaarufu zaidi kwa wapiga kura wake kwa kuzungumzia kivuko, kuliko kuzungumzia muungano.

..muungano is not an election issue kwa wanasiasa wa Tanganyika. mtanganyika wa kawaida haoni kama muungano unaathiri maisha yake ya kila siku.

..zaidi, matatizo yakitokea huku Tanganyika, wananchi hawaanzi kusingizia kwamba chanzo ni muungano.

..wenzetu wa ZNZ tatizo lolote lile likitokea huwa hawajiulizi chanzo chake, wao moja kwa moja husingizia muungano. kama umeangalia video za uamsho utaona wananchi wanaodai kwamba popobawa ametokana na muungano.

..ukweli ni kwamba Tanganyika ni kubwa na ina matatizo mengi sana, na kwa bahati mbaya[nzuri kwa wengine] muungano does not feature that high kwenye mlolongo wa matatizo ya wa-Tanganyika.

NB:

..wanasiasa wa ZNZ nao wanaficha uzembe wao kwa kisingizio cha muungano.

..uzalishaji wa karafuu umepungua na hivyo kupelekea uchumi wa ZNZ nao kuporomoka. sasa wanasiasa kama Ismail Jussa, badala ya kueleza ukweli, na kutafuta mbinu za kufufua uzalishaji wa karafuu, wanasingizia kuwa muungano ndiyo umeangusha uchumi wa ZNZ.
 
nionavyo mimi ndo na wewe umeling'amua hilo,MM yeye anataka kuupalilia kwa kuonyesha kuwa zenji wananufaika na muungano,lakini mimi naweza kusema wakijitenga watapata akili ya KUHANGAIKIA MAISHA YAO
Mkuu kuhangaikia maisha yao ni kweli kabisa akili wataipata na kitakachowaongoza ni ule Ukweli wao. wazenji si wanafiki kama sisi wabara. ni waumini na wanaisimamia kweli daima.hawaruhusu kuufunika ufisadi hata kama umetendwa na ahali wake katu hawavumilii. ona sisi tunavyouana wenyewe,mikataba ya ovyo ya enzi za mangungo nchi inaliwa na tulowapa dhamana ya kutukwamua lakini walaaa baridi kabisa roho zetu.acha wende wakaijenge nchi yao sie tubaki na unafiki wetu wa kugawa bure gas yetu na akanti yetu uswiss izidi kunona. dhana ya ipo siku!!!!! Lini hiyo siku???
 
hivi muungano ukivunjika hawa akina mwinyis, jumbes, bakhresas, amours, Karumes na other zanzibari political and economic elites waliolowea na wanaoishi Tanganyika tutawafanya nini?
 
Dhana hii ya Zanzibar kuitegemea Bara na kwamba bila bara Znzibar haiwezi sidhani kama ni sahihi.

Zanzibar inaweza ikawa inaitegemea sana bara kwa sasa kwasababu tu ya aina ya muungano uliopo lakini wakiwa nje ya muungano wataitegemea bara kwa maana ya kibiashara na pengine makazi kama ilivyo swazland na kwa south africa nk

Nchi kutegemea nchi nyingine kwa shughuli za kiuchumi ndio utandawazi wenyewe
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom