Mdada kaniganda...

Mdada kaniganda...

"Nilikua sijajipanga kuishi na mwanamke kabisa"

Kwa kauli hiyo ina maana huyo mwanamke ulikua unamchezea tuu na kumpotezea muda wake? ulimfanya kua yeye ni wamajaribio? kwanini hukumwambia toka mwanzo? anakuganda coz umempotezea muda wake,

Pambana na hali yako jomba ila usirudie kabisa kucheza na hisia za mtu.
kua na mwanamke haimaanishi uamchezea unaweza ukawa nae lakini usiwe na lengo la kuishi nae kwa muda huo
 
Ilibidi niite familia, ndugu, jamaa na marafiki na balozi. Kabla ya hapo niliongea na dada akagoma kabisa kunielewa. Ilifikia mahali akaunja TV. Akavunja meza ya kioo nilivyokuwa nanyo ndan. Alianza kutoa vitu vya ndan vyote usiku huo anataka abebe aondoke navyo eti ndo malipo ya kumchezea. Nikaona hapa sio mwanamke ni kituko. Alikalishwa, balozi akasikiliza pande zote. Alikuwa muongo akaulizwa yeye kaolewa ni Mimi lini? Akashindwa jibu hajui wazazi wala ndugu zangu. Sijui wazazi wake wala ndugu zake. Balozi akamwambia abebe begi lake aondoke kama ni kuongea au kurudiana ni sehemu nyingine. Mungu anisamehe lakin she was not a woman to marry. She was not. I hope atabadilika aendako.
 
kua na mwanamke haimaanishi uamchezea unaweza ukawa nae lakini usiwe na lengo la kuishi nae kwa muda huo
Ni kweli mkuu. Tabia zake zilinishinda. Kavunja Vitu vyangu ndan. Kapasua T.V, kapasua Meza ya kioo katoa vitu nje vyote anataka abebe aondoke navyo.
 
Jitahidi kula mayai ya kuchemsha kila siku usiku, kula maharage yale mekundu, nyama choma na vitu vya kuleta gesi tumboni.
Hii itakusaidia kutoa harufu ksli usiku.
Kwa muda wa wiki moja atachoka kwa harufu na kuondoka

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Aliondolewa na balozi na wanafamilia mkuu. Ila alinivunjia vyombo ndan. TV inchi 32, na meza. Akatoa vitu vya ndan vyote anataka abebe aondoke navyo.
 
Unaonekana ni kijana mpoleeeeee.Yamkini hujawahi hata kumkemea kwa lolote,jambo ambalo hata yeye analijua fika na mbaya zaidi anatake advantage ya hulka yako hiyo ya upole.Jifunze kuonesha hisia zako wazi wazi(epuka kuigiza).
Mkuu acha tu. Mdogo wangu mabangi ndo alikuja kumuamshia vagi. Ikabid wanafamilia waje, mabalozi, na marafiki waje pia. Alishanivunjia vyombo ndan akatoa vyombo nje vyote anataka abebe aondoke navyo.
 
Mapenzi hayalazimishwi muda aliompotezea ni upi, mara zote yeye siyo wa kwanza. Hata kama angekuwa amemuoa kama hana mapenzi naye aachane naye
Sikuoa mkuu. Mahusiano tu. Ila tabia yake imenishinda kabisa. Mwanamke Wa kuoa kweli anakunjia vyombo ndan, anatoa nje vitu vyoote anataka abebe aondoke navyo utafikiri alisaidia kununua
 
Mkuu uwe unawaambia mapema kuwa all I need is mgegedo,,.

Hayo umeyataka mwenyewe sasa..PAMBANA
Mkuu, tabia zake zilinishinda. Ikabid niishie njiani. Kanitia hasara kweli. Kapigiza vitu ndan, kavunja vyombo vyangu ndan. Katoa vitu ili abebe aondoke navyo. Mkuu kaja tolewa na balozi.
 
Sijui kwanini namhurumie huyo demu?

Inaonekane mkuu ulimpa ahadi sio?
Nilimpa ahadi. Lakin ilikuwa ni njia ya kuachana naye maana tabia zake zilishanishinda. Ningemuambia ukweli angeleta vurugu kama anazoleta sasa. Unaeza ukaingia kwenye mahusiano, lakin ukakuta kilichopo ni tofauti na unachotegemea. Akiwa kwangu amenivunjia vyombo ndan. Akatoa vitu vyangu vyote nje ili abebe aende navyo. Majirani ndo walirudisha. Huyo ni mwanamke Wa kuoa?
 
Nimeshakutana na visanga kadhaa vya demu kuniganda kama ccm alivyoiganda Tz we acha tu inahitaji akili ya ziada
 
Mahusiano yenu yana muda gani? Na huyo mwanamke ana miaka mingapi? Katika muda wa hayo mahusiano yenu ni kipindi gani uligundua kua humpendi?

Maswali yamekua mengi lakini point yangu hapa n kuona scenario ipo vp lazima kuna sababu kwanini huyo mwanamke hataki kukuacha, na hio sababu inaweza kua makosa ni yake au yako. Ukinijibu hapa nitapata cha kukushauri.
2 years now. Aliolewa akaachika. Nikakutana naye mtaani. Nikamtongoza akawa mpenzi. Lakin kwenye yale mahusiano alikuwa mtu Wa starehe, maigizo, mtu Wa kutaka kunichuna. Ananiambia ana mimba mwisho Mara imetoa. Nilichoka. Mwishoni mwishoni wakati anakaa na marafiki zake wamepanga aliniabia ana mimba. Baada ya muda akaniambia mimba imetoka kisa nimemgombeza. Hapo ndo niliamua kuacha kabisa kutaka kuwa naye. Nilitaka kumuacha kimya kimya. Ilibidi aende kwao. Nikaanza kupunguza mawasiliano. Nikakata kabisa. Karud bila taarifa sasa ndo mtiti. Juzi kavunja vyombo ndan. Katoa vitu vyangu nje anataka abebe. Ilibidi niite balozi ndugu na jamaa. Balozi ilibidi amtoe mwenyewe. Popote anisamehe maana nilishamshindwa. Alikuwa hanipendi bali alikuwa kwangu kimasalahi
 
Nimeshakutana na visanga kadhaa vya demu kuniganda kama ccm alivyoiganda Tz we acha tu inahitaji akili ya ziada
Mkuu, Mimi kavunja vyombo ndan, katoa vitu vyangu vyote nje anataka abebe aondoke navyo. Dah, ilibidi niite balozi ndugu na jamaa aise
 
Back
Top Bottom