Feyanga
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 223
- 89
Wakuu, Habari za muda huu?
Leo nakuja kwenu na hii mada ama sijui niite tabia ama vipi. Yaani kumekuwa ni kawaida sasa ya makundi haya: Wapiga picha, watu wa make up, ma-MC, mafundi nguo etc. Yaani wao wanakupa huduma na unalipia na bado wataku-post kwenye Mitandao ya Kijamii (Social Media) kila sehemu.
Kama alikuwa mpiga picha basi utajikuta kila mahali, au kama alikuwa MC wako basi naye atapost picha za sherehe nzima kwa jinsi alivyopiga picha yeye au kuchukua video. Inafika wageni waalikwa mnajikuta huko mitandaoni. Kama alikushonea nguo vivyo hivyo, kama alikupaka makeup naye ni yale yale.
Na kuna wale umenunua nguo, kiatu etc basi kwa kuwa anakujua, siku ukivaa tu hicho kitu labda ukapost bila hata kuwatag. Watakuja hapo “asante kwa kutuchagua” “asante kuturuhusu tukuhudumie” au watachukua picha wakapost kwao na maneno kibao. Je, kama mwenyewe nilikuwa sitaki watu wajue nimenunua kwenu?
Ni nadra kukutana na wanaokuuliza/muuliza mwenye tukio lake kabla hawajapost.
Kwa kweli hii tabia inakera sana, bora hata pangekuwa na makubalino au punguzo la bei katika huduma zao. Mkubaliane kabisa kwamba atatumia picha zako kutafutia wateja hivyo mkubaliane bei kabisa. Sio nakulipa kila kitu halafu mara paaa! picha zimejaa mtandaoni au ukiamka siku inayofuata unakuta familia nzima mpo mtandaoni.
HOJA YANGU:
Jamani hii ni sawa?
Ulinzi wa data upo wapi? Hivi watu wanajua kwamba wana haki juu ya picha/taarifa zao? Hivi wenye matukio wanajua kwamba wanaweza kataa kupostiwa, wanajua ni haki yao kuruhusu au kukataa? Na hao wanaoposti wanajua ni kosa bila ridhaa ya mhusika?
Nini maoni yako?