Mchungaji na mkewe wanusurika kuuawa

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Kweli duniani kuna mengi. Ni ajabu mwanadamu anamuwinda mwanadamu mwenzake utafikiri tunaishi katika mbuga za wanyama.

Siku kadhaa zilizopita, mimi na Mchungaji wangu pamoja na mke wake, tulinusurika kuuawa. Ilikuwa alasiri, mimi na Watumishi hao wa Mungu, tulienda kufanya huduma katika mji mmoja. Barabara inayokwenda katika mji huo ilikuwa ya vumbi na ilikatisha katika pori kubwa lenye miti mirefu.

Baada ya kufika katika mji huo, tulifanya kile kilichotupeleka kisha tukaanza safari ya kurudi. Wakati huo ilikuwa inakaribia saa 12 jioni. Tulivyolifikia lile pori tukaona mbele yetu vijiti vyenye futi kama mbilimbili vimesimikwa chini kwa karibu karibu, mstari mmoja. Mchungaji wangu ndiye aliyekuwa anaendesha gari, akaona sio vema kuvikanyaga vile vijiti akatafuta upenyo pembeni ya vijiti hivyo tukafaulu kupita bila kuvikanyaga. Kwa mawazo yetu tulifikiri labda ni watoto walikuwa wanacheza kwenye barabara hiyo wakaona wasimike vijiti hivyo. Kwa sababu hiyo tuliendelea na safari bila kuhisi chochote kibaya mbele yetu. Siku hiyo hakukuwa na magari wala pikipiki tulizoziona zikipita barabara ile.

Kabla ya kulipita lile pori, tukaona kikwazo kingine kikubwa mbele yetu. Gogo kubwa, refu, lilikuwa limelazwa barabarani kuzuia gari lisipite. Gogo hilo lilikuwa nene sana hivyo kulikuwa hakuna uwezekano wa kulivuka kwa gari. Pembeni ya barabara hiyo hapakuwa na upenyo kama ilivyokuwa pale mwanzoni hivyo ilibidi Mchungaji asimamishe gari. Tulipoangalia kulia kwa barabara, mita kama kumi kutoka kwenye gogo hilo, tukaona mtu ameshika upanga mkononi. Ghafla tulipaza sauti na kuanza kumuomba Mungu atupiganie huku tukimkemea shetani ashindwe kwa Jina la Yesu, sawasawa na Neno la Mungu katika Yakobo 4:7-10. Tulikemea sana, kisha Mchungaji akaniomba nishuke niliondoe lile gogo. Mungu alinipa ujasiri usiokuwa wa kawaida, nikashuka kutoka kwenye gari nikaliendea lile gogo. Nilitumia nguvu nyingi kulivuta na kuliondoa barabarani; kisha nikapanda tena gari, tukaanza kuondoka. Tulivyomtazama yule mtu mwenye upanga, alikuwa bado amesimama palepale alipokuwa. Naamini Mungu alimpiga upofu, kama alivyofanya wakati wa Elisha(2Wafalme 6:18) ndio sababu hakuweza kusogeza unyayo wake kutukaribia. Tuliendelea na safari kwa furaha kubwa huku tukimsifu Mungu aliyetuvusha salama eneo lile.

Kazi za Ibilisi ni kuiba, kuchinja na kutafuta kuharibu maisha yetu(Yohana 10:10), lakini Mungu anapokuwa upande wetu, shetani na majambazi yake yanashindwa na kulegea.
 

iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,667
2,000
Mtu anakuteka na panga we unamkemea shetan unaakili kweli bro? Utakuja kufa kijinga acha uboya
Ndo maana mchungaji alikufanya kimbola wake akakutuma ukatoe gogo jamaa wa panga angeanza na ww ndo ungejua mchungaji aliwahi kushiriki mbio za magari
 

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Mtu anakuteka na panga we unamkemea shetan unaakili kweli bro? Utakuja kufa kijinga acha uboya
Ndo maana mchungaji alikufanya kimbola wake akakutuma ukatoe gogo jamaa wa panga angeanza na ww ndo ungejua mchungaji aliwahi kushiriki mbio za magari
Duh, una maneno! Ngoja nikalale kwanza!
 

Mr Devil

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
4,302
2,000
ona ili boya lingine lina tuchekesha usiku huu.mta pigwa na dole siku nyingne mkiwa mme fumba macho mna kemea
 

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
kwa nini mchungaji yeye hakushuka
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima(Warumi 13:7).

Sio heshima Mchungaji ashuke, aondoe gogo, mimi nibaki nimekaa tu ndani ya gari.
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,488
2,000
Mambo yahusuyo Mungu hupingwa tuu..... hapo ungesema ulikutana na mtu mrefuu kavaa nguo nyeupe ungeeleweka

Huyo mtu na wenzie walioweka hilo gogo hakuna ajuaye yaliyowapa ila miujiza ya Mungu bado inatendeka japo sisi tunaamini miujiza ya pesa tuu🤑🤑
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,864
2,000
Mtu anakuteka na panga we unamkemea shetan unaakili kweli bro? Utakuja kufa kijinga acha uboya
Ndo maana mchungaji alikufanya kimbola wake akakutuma ukatoe gogo jamaa wa panga angeanza na ww ndo ungejua mchungaji aliwahi kushiriki mbio za magari
We ni pimbi kama wavaa makobazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom