Ujumbe wa Ijumaa: Omba kufundishwa na Mungu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,884
155,865
OMBA KUFUNDISHWA NA MUNGU.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tujifunze na kuyatafakari maneno ya uzima.

Wakristo wengi tunamuomba Mungu atufanikishe katika mambo yetu. Yaani atusaidie tupate mahitaji yetu,ni jambo jema kwani pia Mungu ndio anataka iwe hivyo.
Isaya 41:21” Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.”
lakini cha ajabu hatumuombi Mungu atufundishe kuvitumia vitu tunavyomuomba atupe.
Hivyo tunajikuta tunaomba kwa muda mrefu sana wakati mwingine pasipo kuona mafanikio wakati mwingine tunakata tamaa tunaona kama Mungu hatusikii. Lakini tatizo liko hapa hatuombi Mungu atufundishe namna ya kuvitumia ama namna ya kuvitunza/kukitunza pale utakapokipata ili kisije kikakufanya ukawa mbali na Mungu.

Hebu tuutafakari huu mfano kwa kina tutajifunza jambo.
Baba mwenye mtoto anaempenda sana na baba huyo akawa na magari kadhaa ya kutembelea lakini mtoto wake akamuomba baba yake ampe gari la kutembelea ampe moja na baba anajua kabisa kuwa huyu mtoto wangu hajui kuendesha gari,na anajua kabisa kama akimpa litaenda kumuangamiza maana hajui kuendesha, kama baba mwenye busara atamwambia mtoto wake je unajua kuendesha??, si kwamba hataki kumpa kwa kumuuliza swali hilo, kama baba mwema atamfundisha kuendesha gari huenda akampeleka veta akajifunze kisha akishajua ndipo atakapompa lile gari aroke nalo kokote kule pasipo kuwa na wasiwasi tena kama mtto wake anaweza kupatwa na jambo baya kwa sababu hajui kuendesha ila atakuwa na amani kwa sababu tayari mtoto anajua.

`ndivyo ilivyo hivyo pia katika roho tunapohitaji jambo Mungu atape au atufanikishe rohoni anaona kabisa huyu nikimpa hiki kitu anachokiomba hatafika nacho mbali kitamuangamiza.

Lakini ukiwa kama watu hawa wakutaka kufundishwa kwanza kabla hatupata kitu tulichomuomba ama alichotuahidi kutupa omba Mungu akufundishe kukitumia ama kukitunza.

Waamuzi 13:8” Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, ATUFUNDISHE HAYO YATUPASAYO KUMFANYIA HUYO MTOTO ATAYEZALIWA.”

Unaona hapo? Kumbe tatizo sio kupata kile unachokiomba au unachotarajia kukipata kukipata utakipata lakini je utakitumia sawa sawa na mapenzi ya Mungu?.

Ni lazima tutambue kukipata kitu su kuwa na kitu si kwamba unajua kukitumia unaweza ukawa nacho na usijue kukutumia ipasavyo. Ni lazima tukubali kufundishwa kwanza. Hatuwezi neno lolote pasipo yeye.

Yohana 15:5” Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; MAANA PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE.”

Huenda ukawa unamuomba Mungu akupe mume/mke (mwenza) na Mungu kweli akakupa lakini kwa sababu hukumuomba Mungu akufundishe namna ya kuishi na huyo mume/mke hukumuomba akufundishe kuwa myenyekevu kwa mume wako,jukumuomba akufundishe kuwa na mvumiliu katika ndoa,hukumuomba Mungu akufundishe kuyabeba madhafu ya mwenzako nk ndoa yenu haitadumu kamwe mwisho mtaishia kusema “huyu hakuwa chaguo sahihi niliemuomba Mungu” ndugu lilikuwa ni sahihi na ndio maaana mpka mkafunga ndoa sio bahati maaya hakuna kitu kinatokea chini ya jua kwa bahati mbaya.

Huenda umeomba Mungu akusaidie upate kazi na ukapata lakini pia huomba Mungu akufundishe kuwa na nidhamu,kuwa mwaminifu,nk mwisho unapoteza kazi unasema “haikuwa kazi sahihi ambayo Mungu nilimuomba” mdugu sivyo ni wewe ndio hukutaka kufundishwa.

Kwa maana nyingine ni sawa na mtu mpumbavu, mpumbavu anajua ni nini anatakiwa afanye lakini hafanyi, ni swa na mvutaji wa sigara anajua anaharibu mapafu yake na bado kaandikiwa kwenye kasha la sigara lakini anaendelea kuvuta.

Ili tutembee katika njia za Bwana lazima tukubali kufundishwa pasipo hivyo tutajikuta tunaomba, sana tunalia sana,lakini hatutaona majibu ya kile tunachokitaka maana katika ulimwengu war oho tutaonekana kama watoto wadogo tunaotaka kuendesha ndege wakati hatuna maarifa hayo. Na hata tukilazimisha sana Mungu atatupa lakini hatima yake ni kuangamia tu.
Tafakari mistari mifupi hii kwa kina kuna siri kubwa sana ambayo wengi hatuijui lakini kwa neema za Bwana tutautafakari kwa kina siku moja.

Isaya 28:24-29” Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake? Kwa maana Mungu wake ANAMWAGIZA VIZURI NA KUMFUNDISHA. Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito. Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi. HAYO NAYO YATOKA KWA BWANA WA MAJESHI,MWENYE SHAURI LA AJABU,APITAYE WOTE KWA HEIMA YAKE.”

Bwana Yesu akubariki sana.
nuru ya upendo.
Maranatha.
 
Upuuzi Mtupu yaani taarifa za kufikirika tu.

Kila nikifikiri hatujarith utajiri wa Sulemani na bali dhambi za Adam na Hawa napata tabu sana kuamini Bibilia. Yaani Hawa kala Apple moja tu kafukuzwa bustanini na kaambiwa utazaa kwa Uchungu sasa wale Ng'ombe wetu hapa Tarime mbona na wao Wanazaa kwa uchungu wamekula nini ? Halafu bibilia inasema msamehe Mtu saba mara sabini lakini huyohuyo Mungu kashindwa kumsamehe Adam kula Apple moja ? story za Bibilia hazipo sawa, WanaIsrael walikuwa utumwani Misri kwa miaka 400 kilitokea nini Mpaka Waafrika kugeuka wao ndiyo Watumwa?,
Katika Historia ya Misri hatuoni sehemu yoyote kuwa Yusuph aliwahi kuwa kiongozi pia Pyramid zote zile pale Misri hatuoni hata moj ikizungumziwa kwenye Bibilia.
Story za Bibilia ni kama za sungura na fisi tu yaani hairakuja ingia akilini eti nyoka aliongea na Hawa wakati tunajua wazi nyoka haongei , Mke wa Ruthu aligeuka mwamba wa chumvi swali nani alimuona maana walipigwa marufuku kigeuka nyuma,, Eti Samson aliuwa Simba kwenye jangwa la Palestina toka lini Simba anaishi Jangwani? . Hiko kitabu bado sana story zake nyingi ni kutunga tu na kwenye uhalisia .
 
OMBA KUFUNDISHWA NA MUNGU.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tujifunze na kuyatafakari maneno ya uzima.

Wakristo wengi tunamuomba Mungu atufanikishe katika mambo yetu. Yaani atusaidie tupate mahitaji yetu,ni jambo jema kwani pia Mungu ndio anataka iwe hivyo.
Isaya 41:21” Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.”
lakini cha ajabu hatumuombi Mungu atufundishe kuvitumia vitu tunavyomuomba atupe.
Hivyo tunajikuta tunaomba kwa muda mrefu sana wakati mwingine pasipo kuona mafanikio wakati mwingine tunakata tamaa tunaona kama Mungu hatusikii. Lakini tatizo liko hapa hatuombi Mungu atufundishe namna ya kuvitumia ama namna ya kuvitunza/kukitunza pale utakapokipata ili kisije kikakufanya ukawa mbali na Mungu.

Hebu tuutafakari huu mfano kwa kina tutajifunza jambo.
Baba mwenye mtoto anaempenda sana na baba huyo akawa na magari kadhaa ya kutembelea lakini mtoto wake akamuomba baba yake ampe gari la kutembelea ampe moja na baba anajua kabisa kuwa huyu mtoto wangu hajui kuendesha gari,na anajua kabisa kama akimpa litaenda kumuangamiza maana hajui kuendesha, kama baba mwenye busara atamwambia mtoto wake je unajua kuendesha??, si kwamba hataki kumpa kwa kumuuliza swali hilo, kama baba mwema atamfundisha kuendesha gari huenda akampeleka veta akajifunze kisha akishajua ndipo atakapompa lile gari aroke nalo kokote kule pasipo kuwa na wasiwasi tena kama mtto wake anaweza kupatwa na jambo baya kwa sababu hajui kuendesha ila atakuwa na amani kwa sababu tayari mtoto anajua.

`ndivyo ilivyo hivyo pia katika roho tunapohitaji jambo Mungu atape au atufanikishe rohoni anaona kabisa huyu nikimpa hiki kitu anachokiomba hatafika nacho mbali kitamuangamiza.

Lakini ukiwa kama watu hawa wakutaka kufundishwa kwanza kabla hatupata kitu tulichomuomba ama alichotuahidi kutupa omba Mungu akufundishe kukitumia ama kukitunza.

Waamuzi 13:8” Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, ATUFUNDISHE HAYO YATUPASAYO KUMFANYIA HUYO MTOTO ATAYEZALIWA.”

Unaona hapo? Kumbe tatizo sio kupata kile unachokiomba au unachotarajia kukipata kukipata utakipata lakini je utakitumia sawa sawa na mapenzi ya Mungu?.

Ni lazima tutambue kukipata kitu su kuwa na kitu si kwamba unajua kukitumia unaweza ukawa nacho na usijue kukutumia ipasavyo. Ni lazima tukubali kufundishwa kwanza. Hatuwezi neno lolote pasipo yeye.

Yohana 15:5” Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; MAANA PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE.”

Huenda ukawa unamuomba Mungu akupe mume/mke (mwenza) na Mungu kweli akakupa lakini kwa sababu hukumuomba Mungu akufundishe namna ya kuishi na huyo mume/mke hukumuomba akufundishe kuwa myenyekevu kwa mume wako,jukumuomba akufundishe kuwa na mvumiliu katika ndoa,hukumuomba Mungu akufundishe kuyabeba madhafu ya mwenzako nk ndoa yenu haitadumu kamwe mwisho mtaishia kusema “huyu hakuwa chaguo sahihi niliemuomba Mungu” ndugu lilikuwa ni sahihi na ndio maaana mpka mkafunga ndoa sio bahati maaya hakuna kitu kinatokea chini ya jua kwa bahati mbaya.

Huenda umeomba Mungu akusaidie upate kazi na ukapata lakini pia huomba Mungu akufundishe kuwa na nidhamu,kuwa mwaminifu,nk mwisho unapoteza kazi unasema “haikuwa kazi sahihi ambayo Mungu nilimuomba” mdugu sivyo ni wewe ndio hukutaka kufundishwa.

Kwa maana nyingine ni sawa na mtu mpumbavu, mpumbavu anajua ni nini anatakiwa afanye lakini hafanyi, ni swa na mvutaji wa sigara anajua anaharibu mapafu yake na bado kaandikiwa kwenye kasha la sigara lakini anaendelea kuvuta.

Ili tutembee katika njia za Bwana lazima tukubali kufundishwa pasipo hivyo tutajikuta tunaomba, sana tunalia sana,lakini hatutaona majibu ya kile tunachokitaka maana katika ulimwengu war oho tutaonekana kama watoto wadogo tunaotaka kuendesha ndege wakati hatuna maarifa hayo. Na hata tukilazimisha sana Mungu atatupa lakini hatima yake ni kuangamia tu.
Tafakari mistari mifupi hii kwa kina kuna siri kubwa sana ambayo wengi hatuijui lakini kwa neema za Bwana tutautafakari kwa kina siku moja.

Isaya 28:24-29” Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake? Kwa maana Mungu wake ANAMWAGIZA VIZURI NA KUMFUNDISHA. Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito. Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi. HAYO NAYO YATOKA KWA BWANA WA MAJESHI,MWENYE SHAURI LA AJABU,APITAYE WOTE KWA HEIMA YAKE.”

Bwana Yesu akubariki sana.
nuru ya upendo.
Maranatha.
✅🙏🙏🙏
 
MUNGU akubariki kwa andiko jema. Hapo kwenye kuomba mme/mke Nina ushuhuda. Mama yangu mkubwa aliomba MUNGU ampatie mme, kweli Mungu akamleta sasa aliyeletwa ni mtu kutoka kijijini mshamba tena kazi ni mkokozi.kulichotokea mama mkubwa akamkataa. Lakini Mungu akamjibu kwamba umtakae utampata lakini hamtadumu. Kilichofuata akamwomba mungu ampatie upendo kweli mpaka sasa wapo wanaishi vizuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom