Mchungaji mwivi!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Baada ya mahubiri marefu,mchungaji aliwaambia waumini wafunge macho ili waombe.Wakiwa wamefumba macho,alizama kwa kapu la sadaka na kuibua pesa kibao,akazitia kwenye mfuko wa koti la suti yake.Alipoinua uso wake,alikutana macho kwa macho na mzee mmoja mchelewevu ambaye ndo kwanza alikuwa ameingia kanisani anatafuta kiti cha kukaa.Mchungaji akasema;HERI YAKE YULE ASIYESEMA KUHUSU YALE ALIYO SHUHUDIA KWA MACHO YAKE.Mzee naye akajibu;MAANA ATAPATA MGAO WAKE BAADA YA MISA KUISHA!
 
ahahahaaaa, hao wote wezi. Bila shaka waumini pasipo kujua waliitikia.....Ameeen.
 
Hahahaha umeifanya Jumapili yangu iwe njema mapema leo hahaha
Code:
.Mchungaji akasema;HERI YAKE YULE ASIYESEMA KUHUSU YALE ALIYO SHUHUDIA KWA MACHO YAKE.Mzee naye akajibu;MAANA ATAPATA MGAO WAKE BAADA YA MISA KUISHA!
:becky::becky:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom