Mchungaji Msigwa: Ukisema ninasubiri uteuzi unanitukana

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa thamani yake kama binadamu haijawahi na haitawahi kutegemea vyeo vya kuteuliwa au kuchaguliwa.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Neema Msafiri wa Msafiri Online, Msigwa amejibu mapigo kwa wale wanaodai kuwa alihamia CCM ili "akumbukwe" na Rais Samia Suluhu Hassan katika teuzi zinazoendelea. Msigwa ameweka wazi kuwa utambulisho wake uko imara na hautikiswi na ukosefu wa nafasi serikalini.

"Kwa hiyo kukaa hapa kusubiri uteuzi sijui hujateuliwa, hiyo siyo kazi yangu hiyo mimi. Mimi thamani yangu haitegemeani na cheo, cheo hakiongezi thamani yangu wala kutokuwa na cheo thamani yangu haipungui...cheo hakiongezi thamani yangu wala kutokuwa na cheo hakupunguzi identity yangu, identity yangu inabaki pale pale. Kwahiyo maisha yangu hayategemei niwe na cheo au sina cheo", ameeleza.

Mchungaji Msigwa amebainisha kuwa yeye si mwanasiasa wa "kuchukua chochote" kinachowekwa mezani, na kwamba ana uwezo wa kukataa uteuzi ikiwa haendani na utaalamu wake au taaluma yake.

Kwa mujibu wa Msigwa, "cheo kikubwa" anachokifurahia kwa sasa ni kuwa mwanachama wa CCM mwenye kadi, na amewataka Watanzania kumtazama kama mwanasiasa anayesimamia misingi na hoja badala ya kusaka maslahi binafsi kupitia vyeo.

wanasiasa wengi waliopoteza uelekeo na fursa za kisiasa hasa waliokua nae kabla hajajiunga ccm,
wana muonea wivu sana huyu muungwana anae chapa siasa zake kwa uhuru, amani na uwazi kupitia CCM,

yaani hua inashangaza sana watu wanachafukwa mno kuaona mwananichi anatumia na kufurahia uhuru na haki yake ya kufanya siasa zake.
kwasasa Msigwa anafanya vizuri sana kisisa Tanzania :1Head:
 
Huwa unasoma maandishi yako? Insanity is real!
 
Well said
1771701127764.jpg
 
Ukishakuwa msaliti...usaliti ni ROHO kamili,
kama YUDA aliyosaliti CHAMA CHAKE kwa vipande 30 vya fedha NA KUWACHOMESHA WENZAKE.

Msaliti hapaswi kuaminika tena POPOTE ATAKAPOKUWA NA ATAKAPOKWENDA.
 
Back
Top Bottom