Mchungaji Msigwa, Kiti cha Spika, na Kanuni za Bunge

Mchungaji Msigwa, Kiti cha Spika, na Kanuni za Bunge

Huo mtaa wenu ulipatwa na sintofahamu utakuwa mtaa unaopenda sana UDAKU.

Msigwa kaongea UDAKU tupu hakuna kitu pale.

Spika hawezi kupoteza muda na UDAKU...

zemarcopolo mara nyingi nimekuwa nikikufuatilia sana kila mara unataka kila siku wewe unataka unachofikiri kwa uelewa wako wengine wakubali bila kufikiri kama wewe
 
Huo mtaa wenu ulipatwa na sintofahamu utakuwa mtaa unaopenda sana UDAKU.

Msigwa kaongea UDAKU tupu hakuna kitu pale.

Spika hawezi kupoteza muda na UDAKU...

Mkuu wangu ZeMarcopo, kwanza jikite kwenye hoja aliyoleta master peace. Lakini pia kwa hiyo hoja yako, hebu tusaidie hapa, huo udaku ambao jana nilikwambia hata Nchimbi alishindwa kuujengea hoja na kulishawishi bunge, uko wapi hapa katika hoja zenye nguvu, zikibebwa na facts kama hizi;


Mheshimiwa Spika,

Ni hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba Ofisi ya Waziri wa Maliasili na Utalii imeshindwa kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika Tangazo la Serikali tajwa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba sababu kubwa ya kushindwa huko kutekeleza majukumu ya kisheria ya Ofisi hii ni ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ambao umetapakaa katika kila sehemu ya Ofisi hiyo ukiwahusisha watendaji wake wakuu pamoja na watendaji wa ngazi za juu za Chama cha Mapinduzi (CCM) na wafanya biashara makada wa chama hicho. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba kushindwa kwa Ofisi hii kutekeleza majukumu yake hayo kumehatarisha utajiri mkubwa wa maliasili za nchi yetu kama vile wanyamapori, misitu na malikale, na kulitia aibu kubwa taifa letu kwamba ndio chanzo kikubwa cha ujangili wa kimataifa na biashara haramu ya wanyamapori. Maliasili kama wamanyapori hai na nyara nyingine za serikali zimeporwa na kusafirishwa nje ya nchi yetu kwa kupitia viwanja vyetu vya ndege vya kimataifa pamoja na bandari zetu bila hatua stahiki kuchukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,

Bunge lako tukufu limepitisha maazimio mengi kuhusu kashfa mbali mbali zilizogubika utendaji wa Ofisi ya Waziri wa Maliasili na Utalii na utekelezaji wa majukumu yake kisheria. Aidha, Bunge lako limeunda Kamati za Uchunguzi ili kuchunguza tuhuma za ukiukaji sheria na matumizi mabaya ya mamlaka katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi. Hata hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitika kuliambia Bunge lako tukufu, maazimio ya Bunge yamepuuzwa na taarifa za Kamati zake za Uchunguzi kuzimwa. Na katika hili, Mheshimiwa Spika, lawama za kwanza lazima zitupiwe katika Ofisi yako mwenyewe kwa kuwa ndio imekuwa kaburi kubwa la kuzikia taarifa za Kamati za Bunge ambazo pengine Ofisi yako inaona zitaonyesha udhaifu katika utendaji wa Serikali hii ya CCM!

Mheshimiwa Spika,

Tarehe 27 Aprili mwaka 2006 aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Anthony Diallo aliunda Kamati ya Maalum ya Uchunguzi Kuhusu Uboreshaji wa Tasnia ya Uwindaji wa Kitalii Tanzania. Lengo la kuundwa kwa Kamati hiyo lilikuwa ni “… kuchambua na kubaini matatizo yanayoikabili tasnia ya uwindaji wa kitalii na … namna ya kuyatatua matatizo hayo na kuboresha tasnia hiyo.” Kamati ya Diallo iliwasilisha Taarifa Kuhusu Uboreshaji wa Tasnia ya Uwindaji wa Kitalii Tanzania mwezi Juni 2006. Pamoja na mengine, Kamati hiyo iligundua kwamba licha ya biashara ya uwindaji wa kitalii kutakiwa kuwa “… ni chanzo kikubwa cha mapato ya fedha za kigeni, (biashara hiyo) inaingiza fedha kidogo, wastani wa dola za Kimarekani milioni tisa tu kwa mwaka wakati wenzetu wa Zimbabwe, (biashara) hii inawaingizia dola milioni thelathini kwa mwaka.”

Aidha, Kamati iligundua kwamba “… makampuni mengi ya uwindaji hayaajiri wataalam wa ndani ila huwatumia wananchi kwa kazi ndogo ndogo wakati wa msimu wa uwindaji. Makampuni haya pia yanawatumia wawindishaji kutoka nje ya nchi badala ya kutumia wawindishaji bingwa wa Kitanzania.” Vile vile, Kamati ilibaini kwamba licha ya kuwepo makampuni mengi yanayomilikiwa na raia wa Tanzania, makampuni machache ya kigeni yanamiliki idadi kubwa ya vitalu vya uwindaji ambavyo vina “… wanyama wengi ukilinganisha na vitalu vya makampuni ya wananchi ambavyo viko kwenye maeneo ambayo hayana wanyama wengi.”

Na mwisho, Kamati ilibaini kwamba “Idara ya Wanyamapori haisimamii kikamilifu tasnia hii kwa maana haina taarifa muhimu kuhusu vitalu na thamani halisi ya vitalu hivi.” Kwa kadri ya taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Taarifa hii ya Kamati ya Diallo haijawahi kutolewa hadharani na wala kuwasilishwa kwenye Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika,

Inaelekea Kamati ya Diallo ilitokana na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005-2010, iliyokuwa imewaahidi Watanzania kwamba Serikali ya CCM itaendelea “... kuelekeza nguvu zake katika kuhifadhi, kulinda, kuendeleza, kudumisha na kuvuna maliasili kwa manufaa ya Taifa letu.” Ahadi hiyo ilirudiwa kwa karibu maneno hayo hayo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010-2015. Aidha, tuliambiwa na CCM katika Ilani yake ya 2005 kwamba Serikali yake itahimiza “... miji ianzishe bustani za ufugaji wa wanyamapori (zoos) kwa maonyesho.” Hakuna bustani ya wanyamapori hata moja iliyoanzishwa katika kipindi hicho na ndio maana ahadi hiyo ilipotea kabisa katika Ilani ya CCM ya 2010!

Na kama tutakavyothibitisha, Serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Diallo. Badala yake, Serikali hii imeelekeza nguvu zake katika kudidimiza na kudhoofisha uhifadhi, ulinzi na uendelezaji wa maliasili za nchi yetu. Aidha, Serikali ya CCM sio tu imeelekeza nguvu kubwa katika uvunaji haramu wa maliasili za nchi yetu, bali pia imefanya hivyo kwa manufaa ya wafanya biashara wa kigeni wakishirikiana na wafanya biashara wachache ndani ya nchi na viongozi waandamizi wa CCM na makada waandamizi wa chama hicho.

Mheshimiwa Spika,

Mwaka 2009 Bunge lako tukufu liliunda Kamati ya Uchunguzi ili kuchunguza matukio ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu za wananchi wa Liliondo katika Wilaya ya Ngorongoro ambapo wananchi walidaiwa kuchomewa nyumba zao na wanawake kudhalilishwa na Jeshi la Polisi. Taarifa ya Kamati hiyo, iliyoongozwa na Naibu Spika wa sasa wa Bunge lako tukufu, Mhe. Job Ndugai, haikuwasilishwa Bungeni na, kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imezikwa kwenye kaburi la Ofisi ya Spika. Matokeo yake, mgogoro kati ya wananchi wa Loliondo kwa upande mmoja, na Serikali ya CCM na Kampuni ya Orthello Business Corporation (OBC) inayomilikiwa na mfanyabiashara kutoka Oman kwa upande mwingine, umezidi kuwa mkubwa kama inavyothibitishwa na maasi ya wananchi wa Loliondo dhidi ya CCM yaliyoshuhudiwa mwezi uliopita na viongozi na makada wa CCM waliopo ndani ya Bunge hili.

Mheshimiwa Spika,

Mwaka jana Kamati Ndogo ya Kamati ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Mazingira iliwasilisha taarifa ndani ya Bunge lako tukufu kuhusu utoroshwaji wa wanyamapori hai. Kufuatia kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, Bunge lilipitisha azimio, pamoja na mengine, kwamba Serikali itengeneze kanuni za uwindaji ili “… iweze kubana mianya ya rushwa inayoikosesha mapato (na kanuni hizo) ziwe tayari ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.” Bunge lako liliazimia pia kwamba wale wote waliohusika na utoaji wa kibali cha kutorosha wanyama hai wachukuliwe hatua za kinidhamu. Aidha, Bunge liliitaka “… Serikali kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watumishi waliohusika kutoa kibali hicho.” Mwisho, Bunge lako lilirudia mapendekezo ya Kamati ya Diallo ya kuunda mamlaka maalumu kwa ajili kushughulikia masuala ya biashara ya wanyamapori na uwindaji wa kitalii. Bunge lako liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja kutekeleza maazimio hayo. Hadi wakati wa kuwasilisha Maoni haya Serikali imepuuza utekelezaji wa maazimio ya Bunge lako tukufu kuhusu jambo hili. Aidha, licha ya Mheshimiwa Waziri kutoa ahadi kwa Bunge lako tukufu kuwa wanyamapori hai waliotoroshwa nje ya nchi watarudishwa nchini, hadi leo ahadi hiyo haijatekelezwa na Bunge hili halielekei kutaka kuchukua hatua stahiki kwa Mheshimiwa Waziri kwa kupuuza kutekeleza ahadi ya Serikali ya CCM kwa Bunge.

Mheshimiwa Spika,

Mwaka jana Mheshimiwa Waziri alichukua vielelezo kutoka kwa Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu masuala ya ardhi Mh. Halima Mdee juu ya kampuni ya uwindaji ya Game Frontiers kukodisha kitalu chake cha uwindaji kwa ajili ya utafutaji wa madini ya urani katika eneo la Mbarang’andu katika Wilaya ya Namtumbo. Mh. Waziri aliahidi kwamba atachukua hatua stahiki kuhusiana na suala hilo. Hadi ninapowasilisha Maoni haya, Serikali haijaeleza hatua zozote, kama zipo, ilizochukua kumnyang’anya mmiliki wa kampuni hiyo ya uwindaji leseni ya uwindaji katika eneo hilo kwa kukiuka masharti ya leseni hiyo. Aidha, hadi sasa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni bado inasubiri majibu ya Serikali kuhusiana na ujangili wa tembo unaohusisha watendaji wa Serikali kwa kushirikiana na makada wa CCM.

Mheshimiwa Spika,

Tarehe 28 Julai, 2007, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Prof. Jumanne Maghembe alipatiwa taarifa ya kitafiti juu ya Uwindaji Haramu Katika Pori Tengefu la Selous na Maeneo Yanayolizunguka iliyoandaliwa na Bw. Baruani Mshale wa Shule ya Masomo ya Misitu na Mazingira ya Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani. Pamoja na mengine, taarifa ya Bw. Mshale ilidai kwamba kumekuwa na ‘maslahi haramu’ (vested interests) kati ya Serikali na wafanya biashara wa uwindaji wa kitalii wa nje ambayo yamesababisha Serikali kufanya maamuzi yasiyofaa yanayowanyima wananchi vijijini faida zitokanazo na utajiri wao wa maliasili. Mtafiti huyo anataja viashiria vya maslahi hayo haramu kuwa ni pamoja na mvutano kati ya Mkurugenzi wa Wanyamapori na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na uamuzi wa Rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii aliondolewa kwenye Wizara hiyo. Katika kile kinachoonekana kwamba ‘maslahi haya haramu ya kisiasa kwa faida ya kiuchumi ya watu wachache’ yanajulikana serikalini, Mtafiti Mshale alimwambia Waziri kwamba “inawezekana nakukumbusha kitu ambacho tayari unakifahamu”!

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba ‘maslahi haramu ya kisiasa kwa faida ya kiuchumi ya watu wachache’ katika sekta ya uwindaji wa kitalii imekithiri ndani ya CCM na Serikali yake na inawahusisha viongozi na watendaji waandamizi wa chama hicho na Serikali yake. Kwa mfano, mwaka 2009 shehena ya pembe za ndovu zenye uzito wa tani 4 kutoka nchini Tanzania na Kenya zilizoripotiwa kukamatwa na vyombo vya usalama vya Vietnam ilisafirishwa na kampuni ya wakala wa meli iitwayo Sharaf Shipping Co. Ltd. Taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (BRELA) zinaonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana anamiliki robo tatu ya hisa za Sharaf Shipping Co. Ltd., wakati robo iliyobaki ya hisa hizo inamilikiwa na mtu aitwaye Rahma Hussein. Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rahma Hussein ni mkewe Abdulrahman Kinana!

Sio tu kwamba kampuni ya Katibu Mkuu wa CCM na mkewe imehusishwa na usafirishaji haramu wa pembe za ndovu kutoka Tanzania, kampuni hiyo inaelekea kutoa ajira haramu kwa wageni. Wakati shehena ya meno hayo tembo inakamatwa nchini Vietnam, nyaraka zilizoambatana na shehena hiyo zilionyesha kwamba kibali cha kusafirisha shehena hiyo kilisainiwa na raia wa India anayeitwa Samir Hemani mnamo tarehe 13 Novemba 2008. Hemani alikuwa Meneja wa Fedha na Utawala wa Sharaf Shipping Co. Ltd. Hata hivyo, nyaraka za Idara ya Uhamiaji ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imezipata zinaonyesha kwamba wakati Hemani anasaini kibali cha kusafirisha shehena ya meno ya tembo kwa niaba ya wateja wa Kinana na mkewe, kibali chake cha kuishi Tanzania kilikuwa kimeisha tangu tarehe 7 Mei, 2008!

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli rasmi mbele ya Bunge lako tukufu kuhusu kushiriki kwa Katibu Mkuu wa CCM katika kusafirisha kiharamu nyara za serikali ambazo kwa vyovyote vile zinathibitisha kuwepo kwa ujangili wa kutisha unaohusu maliasili wanyamapori wa nchi yetu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli mbele ya Bunge lako tukufu juu ya kuhusika kwa Katibu Mkuu wa CCM katika kuajiri wafanyakazi wageni ambao walikuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria.

Mheshimiwa Spika,

Taarifa ya Tume ya Rais ya Kuchunguza kero ya Rushwa Nchini ya mwaka 1996 iliyoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba ililalamikia kile ilichokiita ‘ukaribu wa wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa’ ulioanza kujitokeza mwanzoni mwa kipindi cha pili cha serikali ya awamu pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Taarifa hiyo ilitoa mfano wa makampuni ya Kigoma Hill Top Hotel, Shenis Commercial Ltd., Tile and Tube Ltd., Royal Frontier (T) Ltd., Game Frontier (T) Ltd. nee MNM Hunting Safaris Ltd., ambayo yalikuwa yanamilikiwa na mfanyabiashara Mohsin Abdallah, mkewe Nargis Abdallah na washirika wao wengine wa kibiashara.

Mohsin Abdallah ni kada maarufu wa CCM na mjumbe wa zamani wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho. Inaelekea kuwa mfanya biashara na kada huyu maarufu wa CCM ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya Serikali ya CCM na hasa hasa katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Zaidi ya hayo, inaelekea kwamba, kama ilivyokuwa kwa Tume ya Warioba miaka kumi na saba iliyopita, ushawishi mkubwa alionao kada huyu wa CCM unatoa uvundo na harufu mbaya ya ufisadi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati ya Kudumu ya Maliasili na Mazingira iliyotolewa ndani ya Bunge hili tukufu, “Kampuni tatu zenye majina yanayoelekea kufanana na zina Ofisi katika jengo moja, Royal Frontiers of Tanzania Ltd., Game Frontiers of Tanzania Ltd., Western Frontiers of Tanzania Ltd., … zinaonyesha kuwa wanahisa wa Kampuni hizo wana nasaba za kifamilia hivyo kuleta hisia kuwa lengo la Sheria na Kanuni kuzuia mtu mmoja kumiliki vitalu zaidi ya vitano linapuuzwa kwa ujanja wa kusajili Kampuni mpya kwa malengo fulani…. Kamati ilipata ushahidi wa Maelezo ya Kampuni zinazofanya biashara ya uwindaji wa kitalii kuwa mmiliki wake ni mmoja, na hata maelezo ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kumshauri Waziri kuhusu Ugawaji wa Vitalu yanaashiria kuwa kampuni zote hizo zinamilikiwa na mtu mmoja, hali inayoweza kusababisha mtu huyo kupata vitalu vingi kinyume cha Sheria.”

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa kauli mbele ya Bunge hili tukufu juu ya mahusiano yake na mfanya biashara na kada huyu wa CCM ambayo yamepigiwa kelele kwa karibu miaka ishirini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua kama huu sio mfano wa wazi wa ‘maslahi haramu ya kisiasa kwa faida ya kiuchumi ya watu wachache’, basi Serikali iliambie Bunge lako tukufu kuna maslahi gani ya umma katika mahusiano haya.

Mheshimiwa Spika,

Mohsin Abdallah sio mfanya biashara na kada pekee wa CCM mwenye maslahi yenye mashaka katika sekta ya uwindaji wa kitalii. Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Diallo, makada waandamizi wa CCM wenye maslahi ya aina hii ni wengi na baadhi yao wako humu ndani ya Bunge lako tukufu. Taarifa hiyo inayataja makampuni ya Coastal Wilderness (Tz) Ltd., ambayo wakurugenzi wake wanatajwa kuwa Napono Edward Moringe Sokoine na Namelok Edward Moringe Sokoine; Enzagi Safaris (Tz) Ltd., yenye wakurugenzi Makongoro Nyerere na Mh. Muhamed Seif Khatib; Said Kawawa Hunting Safaris yenye wakurugenzi Chande Kawawa na Hassan Kawawa; na M.S.K. Tours & Hunting Safari Co. ya Mh. Muhamed Seif Khatib.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati ya Maliasili na Mazingira, mengi ya makampuni haya yalipewa vitalu vya uwindaji wakati hayana uzoefu wala mtaji wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii katika vitalu hivyo. Matokeo yake ni kwamba makampuni hayo yalishindwa kusimamia uhifadhi wa wanyamapori katika vitalu vyao na kusababisha tatizo la ujangili kushamiri katika vitalu hivyo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa kauli mbele ya Bunge lako tukufu ni kwa nini Serikali hii ya CCM imekuwa ikitoa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa makada waandamizi wa CCM ambao wanajulikana kuwa hawana weledi wala uwezo wa kibiashara wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii na hivyo kusababisha tatizo la ujangili kuwa kubwa zaidi na kuleta hasara kwa taifa letu.

Mheshimiwa Spika,

Nchi yetu imeanza kufedheheshwa katika mikutano ya kimataifa ya uhifadhi kwa sababu ya Serikali hii ya CCM kukumbatia makada waandamizi wa CCM wanaojihusisha na ujangili. Kwa mfano katika Mkutano wa 16 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) uliofanyika Bangkok, nchini Thailand mwezi uliopita, Mohsin Abdallah alitajwa na Shirika la Upelelezi wa Masuala ya Mazingira (Environmental Investigations Agency, EIA) kuwa ni mmoja wa majangili wakubwa wanaojihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo lakini Serikali ya Tanzania imeshindwa kumchukulia hatua za kisheria kwa sababu ya ushawishi wake mkubwa katika siasa za ndani ya chama tawala na Serikali hii ya CCM. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni fedheha ya aina gani kimataifa itakayoiamsha Serikali hii ya CCM katika usingizi wake wa pono ili iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makada wa CCM wa aina hii?
 
Kamanda Tumaini Makene, Tatizo kubwa la hawa vijana wa Lumumba zemarcopolo inclusive, kwanza kabisa hawana uwezo wa kujenga hoja, ni wavivu siyo wa kufikiria tu bali hata kusoma. Ndo maana wao wakisha soma heading tu, wanaanza kuporomosha matusi bila kujua content ya hiyo heading.
 
Mkubwa naomba kama uko Arusha nitafute au kama haupo huku basi naomba unitafute! Katika wachangiaji wakubwa katika kuijadili hotuba ya kutoka kambi ya upinzania iliyosomwa na Mchungaji Msigwa mimi nilikua number moja! sitaki kubishana na watu kuhusu hotuba ile bali ni ukweli usiofichika na uko wazi kua kuna viongozi katika taifa hili wamelihujumu sana kwakujinufaisha kwa nyara za serikali, halafu anasimama kiongozi wa kitaifa kumtetea mtu mmoja na kumuita Mchungaji Msigwa ni muongo???

Naapa kua Emanuel Nchimbi kizazi hiki kinachokuja kupiga kura mwaka 2015 kitawahukumu! Nwatakia sikukuu njema kwa waajiriwa wote! Happy Labor Day.


Mkuu Ndallo, nashukuru sana kwa mchango wako.

Ndugu yangu nipo Dar es Salaam kwa sasa; tuombeane uzima, nkifika A-town ntakutafuta kwani huwa napita mara kwa mara katika harakati za kutafuta mkate wangu wa kila siku.

Ulicho kiongea ni kweli kabisa, kwani kwa wale wenye akili timamu tulisha jiuliza maswali mengi kutokana na nguvu nyingi itumiwayo na CCM kuhakikisha jimbo la Arusha mjini linalo shikiliwa na Kamanda Lema linarudi mikononi mwa Magambaz. Mbinu zote wazitumiazo CCM mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hadi sasa zimezua sintofahamu kwa Watanzania tulio wengi. Tumeshuhudia hujuma na vitimbwi anavyofanyiwa kamanda Lema kila kukicha, tumeshuhudia bongo movie ya meya wa Ki-china wa jimbo la Arusha mjini, bila kusahau filamu ya Magesa Muongo ya hivi majuzi.

Hayo matukio yamezua gumzo kwa wapenda mabadiliko walioko nchini na nje ya Tanzania, kwa nini CCM hawa hangaiki na jimbo la Musoma mjini, Iringa mjini, Mbeye mjini, Ilemela, Kawe, Singida mashariki, Karatu na majimbo mengine mengi mbayo yamekaliwa na CHADEMA? Kuna nini Arusha, Why Lema ?

Hivyo tuki-connect dots tunagundua ya kuwa kuna siri kubwa nayo siyo nyingine bali ni ufisadi uliotamalaki na kukita mizizi mjini Arusha unaolindwa na mfumo uliopo, hivyo basi mafisadi na viongozi wa CCM wameshikwa na taharuki kuona jimbo hilo liko mikononi mwa CHADEMA kwani wanajua siri zao zitaumbuka mda siyo mrefu, ndo maana wana struggle usiku na mchana CHADEMA ipotee Arusha ili waweke vibaraka wao watakao endelea kulinda interest zao, Lakini kwa vile Mungu yupo upande wetu wameshindwa na ndiyo hivyo tunaendelea kuanika maovu yao.
 
hawa viongozi weng wa ccm ni mabilionea wa kutupwa kwa jasho letu aisee wanatunyonya sana tani arobaini ya meno ndovu ina maana ni wastan wa tembo wangapi:
na kwa muda gani hawa wanyama wamekufa:
je ccm itawaeleza nini watu wanaotumikia vifungo kwa kukutwa na pembe moja tu la ndovu leo mtu mmoja tu na mkewe wana tani arobain?:
duh! balaa zaid pale waziri anaposimama na kumtetea sababu tu ni katibu wa chama kinachoongoza nchi:
aibu ingine pale spika wa bunge anaposema 'mtaskia mengi kwenye hotuba hii lakini nyie waacheni tu 'na sijui aliyasema haya kwa maslahi ya nani?
 
Mkuu Ndallo, nashukuru sana kwa mchango wako.

Ndugu yangu nipo Dar es Salaam kwa sasa; tuombeane uzima, nkifika A-town ntakutafuta kwani huwa napita mara kwa mara katika harakati za kutafuta mkate wangu wa kila siku.

Ulicho kiongea ni kweli kabisa, kwani kwa wale wenye akili timamu tulisha jiuliza maswali mengi kutokana na nguvu nyingi itumiwayo na CCM kuhakikisha jimbo la Arusha mjini linalo shikiliwa na Kamanda Lema linarudi mikononi mwa Magambaz. Mbinu zote wazitumiazo CCM mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hadi sasa zimezua sintofahamu kwa Watanzania tulio wengi. Tumeshuhudia hujuma na vitimbwi anavyofanyiwa kamanda Lema kila kukicha, tumeshuhudia bongo movie ya meya wa Ki-china wa jimbo la Arusha mjini, bila kusahau filamu ya Magesa Muongo ya hivi majuzi.

Hayo matukio yamezua gumzo kwa wapenda mabadiliko walioko nchini na nje ya Tanzania, kwa nini CCM hawa hangaiki na jimbo la Musoma mjini, Iringa mjini, Mbeye mjini, Ilemela, Kawe, Singida mashariki, Karatu na majimbo mengine mengi mbayo yamekaliwa na CHADEMA? Kuna nini Arusha, Why Lema ?

Hivyo tuki-connect dots tunagundua ya kuwa kuna siri kubwa nayo siyo nyingine bali ni ufisadi uliotamalaki na kukita mizizi mjini Arusha unaolindwa na mfumo uliopo, hivyo basi mafisadi na viongozi wa CCM wameshikwa na taharuki kuona jimbo hilo liko mikononi mwa CHADEMA kwani wanajua siri zao zitaumbuka mda siyo mrefu, ndo maana wana struggle usiku na mchana CHADEMA ipotee Arusha ili waweke vibaraka wao watakao endelea kulinda interest zao, Lakini kwa vile Mungu yupo upande wetu wameshindwa na ndiyo hivyo tunaendelea kuanika maovu yao.
Asante sana Master Peace! Nimezaliwa Arusha na maisha yangu yote yako Arusha! Historia ya nchi hii kabla ya Uhuru Jimbo la Arusha mjini CCM wameshindwa na hawatakaa kuja kuchukua jimbo hili japokua Abrahamani Kinana na Felix Mrema kutawala kupitia chama chao lakini yote ilikua ni nguvu ya hela! Lakini ilani ya Chadema tunasema Money is not everything! And also Money can't buy happiness!
 
Asante sana Master Peace! Nimezaliwa Arusha na maisha yangu yote yako Arusha! Historia ya nchi hii kabla ya Uhuru Jimbo la Arusha mjini CCM wameshindwa na hawatakaa kuja kuchukua jimbo hili japokua Abrahamani Kinana na Felix Mrema kutawala kupitia chama chao lakini yote ilikua ni nguvu ya hela! Lakini ilani ya Chadema tunasema Money is not everything! And also Money can't buy happiness!

Asante mkuu kwa taarifa njema zenye chembe chembe za ukombozi wa ki-fikra. Ni wakati muafaka wa kuwaonyesha Magambaz na ulimwengu mzima ya kuwa CCM - Haikubaliki katika uchaguzi wa madiwani unao tarajiwa kufanyika kata nne mapema mwezi wa sita. Wana Arusha msisahau kauli mbiu yetu " Kula CCM,kura CHADEMA".
 
Mkuu jifunze kujenga hoja kwani hili ni jukwaa la GT, siyo kuandika kila kitu as if unajifunza kusoma na kuandika.
Na siyo lazima uchangie kila mada, wakati mwingine jifunze kuficha uwezo wako mdogo wa kufikiri kwa kukaa kimya itakusaidia maishani mwako.
sasa ataonekanaje nkuwa amefanya kazi/lazima atupie bandiko ndiyo aende Lumumba
 
Back
Top Bottom